STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

Ndanda Fc yainyoa Prisons na kutoka mkiani

http://3.bp.blogspot.com/-NXJDcVCWLvU/VBRkZtkm6NI/AAAAAAAACrc/72CxWBdgpzg/s1600/20140913_160438.jpg
Ndanda
BAO pekee lililofungwa na Jacob Massawe katika dakika ya 35 imeisaidia Ndanda Fc ya Mtwara kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons Mbeya na kung'oka mkiani mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, limeweza kuifanya Ndanda kufikisha pointi 9 na kutoka mkiani wakiiachia Prisons-Mbeya wakiwapokea wakati ligi ikitarajiwa kuendelea tena wikiendi ijayo.
Kocha wa Ndanda Mewja Abdul Mingange amesema amepokea ushindi huo kwa furaha baada ya vijana wake kujituma uwanja na kuibuka washindi huku kocha wa Prisons-David Mwamaja amesema wamekubali kipigo kwa vile vijana wake walifanya makosa yaliyotumiwa na wenzao kupata ushindi huo.
Kwani katika dakika za lala salama wenyeji walipoteza nafasi ya kusawazisha bao hilo baada ya kukosa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo Prisons wamekaa mkiani wakiwa na pointi saba wakati Ndanda wakichupa hadi nafasi ya 12 katika msimamo huo wakiwa juu ya Mbeya City yenye pointi nane.

No comments:

Post a Comment