STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

Kalapina auaga mwaka 2014 akitarajia makubwa 2015

http://api.ning.com/files/3QWN5yhdbaeQObObLezaYgpUwAXMvGqT*xDpp-v1dArxT1bAwibog9Yk4gMPCahJQX1EPtdr6KDsl-MHfQnB62aUwJ1fkvv5/PINA.jpg
Kalapina
RAPA na mwanaharakati, Karama Masoud 'Kalapina' amesema mwaka 2014 ulikuwa wa mapinduzi katika muziki wa kizazi kipya nchini na kutabiri mapinduzi zaidi kwa mwaka 2015 ulioanza.
Kalapina aliyeuaga mwaka 2014 kwa kuangusha shoo akishirikiana na Kikosi cha Mizinga  na wasanii wengine kama LWP, Big Dog Pose, Dopa Man na Country Boy, alisema kwa yeyote aliyefuatilia muziki wa Tanzania amebaini mwaka 2014 ulikuwa wenye mapinduzi makubwa na fani hiyo kupata mafanikio kwa wasanii walio wengi.
Hata hivyo alisema mafanikio hayo yanapaswa kuwa changamoto kwa wasanii wote kuongeza bidii ili kusonga mbele zaidi kubwa kulenga kuikomboa jamii katika hali iliyonayo ikizingatiwa mwaka 2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
"Mafanikio yaliyopatikana ndani ya 2014 ni chachu ya kupata mafanikio zaidi ndani ya 2015, muhimu tushirikiane na kuhakikisha tunaisaidia jamii katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu," alisema Kalapina.
Kalapina ambaye aliwahi kugombea udiwani kupitia chama cha CUF, aliwahi kudokeza kuwa mwaka huu atajitosa kuwania kiti cha Ubunge wa Kinondoni kwa lengo la kutaka kuwakomboa watanzania hususani wa jimbo hilo ambalo halijawahi kuongozwa na 'mzawa' wa eneo hilo

No comments:

Post a Comment