STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

Shilole aahidi makubwa 2015

MUIGIZAJI nyota wa filamu anayetamba kwenye muziki kwa sasa, Zuwena Mohammed 'Shilole' amewataka mashabiki wake kupata mambo makubwa na mazuri zaidi ndani ya mwaka 2015 kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita.
Shilole anayetamba kwa sasa na wimbo mpya wa 'Malele' baada ya kusumbua hewani na nyimbo kama 'Lawama', 'Dume Dada', 'Chuna Buzi', 'Nakomaa na Jiji' na 'Nimemchukua' alisema amejipanga kuwapa raha zaidi mashabiki wake.
"Shishi Baby halali kwa kuwaza namna ya kuwapa burudani mashabiki wake, hivyo wajiandae kupata makubwa zaidi kuliko ilivyokuwa nyuma sawia na kusubiri kuniona nikirejea tena kwenye filamu baada ya kuwa kando kwa muda," alisema Shilole.
Mwanadada huyo alisema anajiandaa kushuti filamu yake mpya itakayofahamika kwa jina la 'Shilole in Dar' ambayo atairekodia Igunga Tabora baada ya awali kutamba na filamu kama 'Shilole', 'Fair Decision', 'Bed Rest', 'Black Sunday', 'Morning Alarm' na nyingine.

No comments:

Post a Comment