STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

RC Kandoro awaasa watanzania kudumisha amani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIdCG8q41fcHcJCPLnyMeU3MtDBoF9jTL6h2bf2OUimm7yC_Vh8ffzBmmCqMQH8sY7P4hyPtWBRisvzPY30rSrB4mKD_jgGEot7YjrNC5oCAPJreK9Jkm785v1cnjdyKu_BU4vmpn-GUk/s800/2.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
Mwandishi MaalumMKUU wa Mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wananchi wa kudumisha amani kwani kinyume na uwepo wa amani hakuna maendeleo yatapatikana katika nchi na kwa wananchi.
Kandoro amesema hayo wakati akizungumza katika mkesha wa mani ambao uliandaliwa na viongozi wa dini wa Mkoa huo kutoka makanisa mbalimbali.
Alisema amani ya Tanzania haiwezi kudumu  kama vitendo vya uvunjifu wa haki, uonevu, ukosefu wa maadili na ukosefu wa ajira vitaendelea kuongezeka katika jamii.
"Suala la amani ni la kila mtu katika jamii hivyo kinachohitajika ni kila mmoja wetu kuwa sehemu ya kuhakikisha amani inakuwepo kwa nguvu zoake zote," alisema.
Kandoro aliwataka viongozi wa dini waache mahubiri ya kudai fedha zasadaka badala yake wafundishe waumini wao kufanya kazi kwa bidii ili mapato yao ndio watoe sadaka.
Alisema hivi sasa vijana wengi wapo vijiweni hawana kazi hivyo kinachohitajika ni juhudu kila mmoja wenu kwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha jamii iweze kukituma katika kujitafutia kipato cha halali badala ya watu kutoa sadaka za ufisadi, rushwa na madawa ya kulevya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo viongozi wa dini watasimamia haki taifa litastawi na kuwa mahali pa maendeleo na kuboresha uwajibikaji katika utumishi.
Akizungumza katika mkesha huo kwa niaba ya viongozi wa dini Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, alisema ni vyema viongozi wakazingatia maadili katika kutumikia Taifa na jamii ili kuondoa tabia ya ufisadi na rushwa iliozoeleka.
Mwamalanga alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa viongozi wa dini ambao wanawatetea watu ambao wamefaidika na fedha za Escrow waache kwani wanamkosea mungu.
Alisema mchakato wa kupiga vita ufisadi unahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo ni kosa kwa baadhi ya viongozi hasa wa dini kudiriki kutumia nafasi zao kutetea waovu.

No comments:

Post a Comment