STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Waziri Mahanga azindua kitabu cha Marehemu Steven Kanumba

NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga,  jana amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven Charles Kanumba, Kinachoitwa ''Steven Charles Kanumba: The Great Fallen Tree''  kilichoandikwa na Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.
Wasanii mbalimbali wa filamu walihudhuria uzinduzi huo huku bendi ya Malaika chini ya Christian Bella ilitumbuiza kusindikiza uzinduzi huo.
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).

No comments:

Post a Comment