STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Juventus yaifyatua Napoli 3-1, yazidi kujikita kileleni

Paul Pogba akishangilia na wenzake
VINARA wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, Juventus imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuikung'uta Napoli wakiwa ugenini kwa mabao 3-1.
Bao la Paul Pogba katika dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Llorente liliwashtua wenyeji ambao walienda mapumziko wakiwa nyuma kabla ya kuzinduka kipindi cha pili baada ya iguel Britos kusawazisha dakika ya 64.
Dakika ya 69 wageni waliongeza bao la pili kupitia Martin Cacerea aliyemaliza pande la Andrea Pirlo na katika dakika za lala salama Arturo Vidal aliifungia Juventus bao la tatu na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 43 na kuzidi kuwakimbia wapinzani wa AS Roma waliomalizishwa sare ya 2-2 nyumbani na Lazio mapema jana.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Sampdoria ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Empoli.

No comments:

Post a Comment