STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Messi, Suarez, Neymar wafunga Barca wakiua Atletico Madrid

Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Nyota wa Barcelona wakishangilia ushindi wao
Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Furaha tupu kwa wakali wa Nou Camp
WASHAMBULIAJI nyota wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wote walifunga wakati timu yao ikiiadhibu mabingwa watetezi wa La Liga, Atletico Madrid kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi hiyo ya Hispania.
Neymad alianza kufungua karamu ya mabao kwa wenyeji waliokuwa uwanja wa Nou Camp katika dakika ya 12 baada ya kumalizia kazi nzuri ya  Suarez kabla ya Suarez kufunga b ao la pili dakika ya 35 kwa kazi nzuri ya Messi.
Wenyeji walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Mario Mandzukic katika dakika ya 57 kwa mkwaju wa penati baada ya Messi kucheza madhambi langoni mwake dhidi ya Jesus Gamez.
Hata hivyo mshambuliaji huyo anayenyemelewa na Chelsea, alisahihisha makosa kwa kutumbukiza wavuni bao la tatu dakika tatu kabla ya pambano hilo kumalizika na kuifanya Barcelona kuwapumulia Real Madrid kwa tofauti na pointi moja, wenyewe wakiwa na 41 wakati Real wakiwa na 42.
Atletico Madrid wameendelea kusalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi  18 kama Barcelona, huku Real Madrid akiwa na mecho moja mkononi kwani imecheza mechi 17 tu.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Athletic Bilbao ilikubali kipigo cha 2-1 nyumbani dhidi ua Elche, Granada ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Real Sociedad inayonolewa na kocha David Moyes na leo usiku Rayo vallecano itakuwa wenyeji wa Cordoba katika mfululizo wa ligi hiyo inayozidi kushika kasi.

No comments:

Post a Comment