STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Ali Baucha, Ney wa Mitego waja na Vululu

BAADA ya kutamba na 'Chimpododo' na 'Zumzum' aliomshirikisha K-One, dansa wa zamani na mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Ali Baucha anajiandaa kuachia wimbo wake mpya uitwao 'Vululu'.
Baucha aliiambia MICHARAZO kuwa wimbo huo mpya ambao umerekodiwa katika studio za Baucha Records, ameimba akishirikiana na Ney wa Mitego.
"Katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, nipo mbioni kuiachia kazi yangu mpya iitwayo 'Vululu' niliyoimba na msanii Ney wa Mitego, kila kitu kimekamilika kilichobakia ni siku ya kutoka hadharani," alisema Baucha.
Baucha alisema wimbo huo wa 'Vululu' ni miongoni mwa kazi mpya zilizotengenezwa na studio zake za Baucha Records.
Alisema kazi nyingine zitakazoachiwa ni pamoja na wimbo mpya wa K-One alioimba na Suma Lee na kazi mpya ya Fizzo aliyesumbua mwaka jana na '24 Hours' ambaye safari hii ataimba na Walter Chilambo

No comments:

Post a Comment