STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 24, 2013

Kibadeni akana kumtimua Kaseja Msimbazi

Kocha King Abdallah Kibadeni
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnmGiUBH2n-4bYq2A7G-O5Mg7eMw2R8U3g_2gTLIHmOvOciOk4zkgnhEV0ZbsJdpep3-YAmE7L8q-zXX7P9cJDnYcQoRAUfq3BK2wnYkoqAoZu9sLMdhdazbFee-dXHAlY_7VkAk1INgo/s1600/JUMA_KASEJA%5B1%5D.JPG
Kipa Juma Kaseja
KOCHA wa Simba, Abdallah Kibaden 'King', ameibuka na kukanusha vikali uvumi kwamba ni yeye ndiye aliyemtimua kipa chaguo la kwanza wa timu hiyo na Taifa Stars, Juma Kaseja baada ya kumtema katika orodha ya nyota wanaotarajia kuwamo katika kikosi chake cha msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Badala yake, Kibaden ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani wa 'Wekundu wa Msimbazi' aliyewahi pia kuandika rekodi kwa kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho wakati akiifundisha mwaka 1993, amefichua kuwa Kaseja hakuwamo katika orodha ya wachezaji aliokabidhiwa na uongozi wa klabu yake hiyo.
Akizungumza na jana, Kibadeni, alisema wakati akikabidhiwa majina ya wachezaji wa timu hiyo ili aanze kuwanoa, jina la Kaseja halikuwamo na hivyo yeye hawezi kulirejesha kwa maamuzi yake binafsi.
"Sijamkata mimi, ila jina lake sikupewa. Hicho ndicho ninacheweza kukieleza... mambo mengine ni ya ndani ya klabu," alisema Kibaden, mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo aliyerejea kuwafundisha baada ya kuihama klabu aliyoiongoza msimu uliopita ya Kagera Sugar.
Alisema kwa sasa tayari ameshapata wachezaji 25 atakaokuwa nao katika msimu ujao wa ligi, huku akiwataja nyota wa kigeni kuwa ni wawili na wote wanatokea Uganda.
"Kikosi changu hakitazidi nyota 25, na wageni hadi leo (jana) ni kipa Abel Dhaira na beki Senkoomi (Samuel), mipango mingine ya ndani ni ya kiufundi. Mazoezi tunayoendelea nayo ni ya kawaida na wengi waliokuja kujaribiwa hawajanishawishi kuwachukua," aliongeza Kibaden.
Naye Kaseja ambaye aliwahi kusema kitambo kuwa hahofii kutemwa Simba, alisema kuwa hivi sasa anachofanya ni kuendelea kujiweka 'fiti' ili atumikie vizuri taifa kwa sababu yeye na wenzake wa kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) wana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanashinda katika mechi ijayo dhidi ya Uganda na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
"Jamani kuhusiana na Simba siwezi kusema lolote kwa sasa... ila maisha ni popote," alisema nahodha huyo wa Taifa Stars ambaye wiki iliyopita alishuhudiwa akiwa katika mazoezi ya timu ya vijana ya Simba B, akishauriana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Amri Said.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage hakutaka kueleza wazi suala la Kaseja na badala yake akasema kuwa hivi sasa, suala la nani asajiliwe na nani aachwe liko katika mamlaka ya kamati yao ya ufundi inayoshirikiana na benchi lao la ufundi.
Rage alisema vigezo vya kusajili mchezaji ni muhimu zaidi kutekelezwa na makocha na kisha kamati ya utendaji itakuwa ya  mwisho kwa lengo la kutoa baraka.
 
NIPASHE

CHADEMA yafichua njama nzito dhidi yao

Mussa Tesha aliyemwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa Igunga
Viongozi Wakuu wa CHADEMA (kulia) Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuna mpango mchafu wa kuwabambikizia viongozi wakuu wa chama hicho kesi ya kumwagiwa Tindikali kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Musa Tesha.
Viongozi wanaoandaliwa mpango huo ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Mnyika alisema mpango huo unafanyika kwa lengo la kukidhoofisha chama chao kinachowapa wakati mgumu CCM.
Alisema hivi sasa baadhi ya makachero wa polisi wamekuwa wakiwakamata vijana na kuwalazimisha kukiri kwa kuandika au kuandikiwa maelezo kuwa viongozi hao waliwatuma kummwagia tindikali Tesha wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 2011.
Mnyika alisema wafuasi wao waliokamatwa na polisi kwa kuhusishwa na tukio hilo wameshinikizwa kusema Mbowe, Slaa, Lissu na yeye ndio waliowatuma kummwagia tindikali Tesha.
Alisema jambo hilo linaendeshwa kisiasa, ambapo wafuasi wanne wameshatiwa mbaroni na kuwalazimisha kuwataja viongozi wakuu wa CHADEMA kuhusika na uhalifu huo.
Mnyika aliwataja waliokamatwa ni pamoja na Evodius Justinian, aliyeshikiliwa kwa siku mbili mjini Bukoba, na baadaye akapelekwa Mwanza kabla ya kufikishwa Dar es Salaam.
Alisema zoezi hilo lilifanyika kwa kificho na mtuhumiwa huyo baadae alifikishwa Igunga.
Alibainisha kuwa taarifa za kada huyo kupelekwa Dar es Salaam  zilikuwa za kificho kwani wakili wake, Nyaronyo Kicheere aliyeongozana na ndugu wa mtuhumiwa huyo walipofika Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam walielezwa amepelekwa Makao Makuu.
Mnyika alisema mara baada ya Evodius kuonana na wakili wake, Kicheere, siku hiyo alieleza unyama aliofanyiwa na jeshi hilo wakati wote wa mahojiano mkoani Mwanza na Dar es Salaam.
Katika maelezo yake yaliyoshuhudiwa na Ofisa wa Polisi Makao Makuu, Advocate Nyombi, Evodius alisema kuwa baada ya kutolewa mjini Bukoba kwa siri bila ndugu zake kujua, alipelekwa jijini Mwanza na kuhojiwa bila kuruhusiwa kuonana na wakili wake.
Kada huyo akisimulia unyama aliofanyiwa alisema:  “Nimepigwa na polisi Mwanza, nikiwa chooni Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati naletwa huku, polisi wakaniambia mimi ni mtu hatari sana, niseme nilifanya nini Igunga na kama najua mkanda wa Lwakatare.
“Nikiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam niliomba kwenda chooni, waliingia pamoja na mimi wakanipiga sana, nimeshaandika maelezo kwa kulazimishwa, niliomba kuwa na wakili wakanikatalia.”
Aliongeza kuwa akiwa Dar es Salaam alihojiwa aseme ukweli kuhusu video ya Lwakatare. Akawajibu kuwa ilifanyiwa uhariri na Ludovick, lakini akapigwa makofi na askari wakaagiza nyaya za umeme za kutesea.
“Waliposimama kuleta nyaya za umeme, kwa kuhofia mateso ya umeme nikasema hii video ni yangu. Ninaumwa sana tumbo la kuhara damu, natumia dawa nilizonunuliwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Kagera tarehe 4 Aprili,” alisema.
Mnyika alisema mtuhumiwa wa pili aliyeteswa ili akubali kuandika kuwa Mbowe, Slaa, Lissu na Mnyika walimtuma akammwagie tindikali Tesha ni Seif Kabuta aliyekamatwa Mwanza.
Alisema Kabuta baada ya kukataa kukiri kuwa viongozi wake wanahusika na matendo hayo, walimfungia katika chumba maalumu wakamleta mke wake, mama yake na mkwe wake na kumtesa mbele yao ili akiri kuwa Mbowe na wenzake walimtuma kummwagia Tesha tindikali.
Mnyika alisema mtuhumiwa wa tatu aliyekamatwa kuhusishwa na tindikali ni Oscar Kaijage wa Shinyanga mjini, ambaye awali alipokamatwa aliambiwa ni kwa sababu kuna pesa zimepotea kwa njia ya simu, na yeye alikuwa anajishughulisha na uwakala wa pesa kwa njia ya mitandao ya M-pesa na Z-pesa.
Alisema mtuhumiwa huyo alipokutanishwa na makachero wa polisi makao makuu, naye alilazimishwa aseme kuwa Mbowe, Slaa, Lissu na Mnyika walimtuma akammwagie Tesha tindikali.
Mnyika alisema mtuhumiwa wa nne ni Rajab Kihawa, aliyetumiwa wasichana kuitwa akiwa Dodoma, ambaye aliombwa akubali kupewa shilingi milioni 30, kama alivyolipwa Ludovick ili aseme kuwa Mbowe na wenzake waliwatuma kummwagia tindikali Tesha.
Mtuhumiwa wa mwisho ni Henry Kilewo, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Kinondoni, na Katibu wa Makatibu wa CHADEMA Kanda Maalumu ya Dar es Salaam anayeshikiliwa na polisi.
Polisi wanamtuhumu Kilewo kummwagia tindikali Tesha wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 2011.
Kilewo alishikiliwa na polisi kuanzia Ijumaa iliyopita na baada ya kuhojiwa alichukuliwa kwa kificho kupelekwa Mwanza kwa ndege ili aweze kuunganishwa katika kesi hiyo ya Igunga leo.
Mnyika alisema Kilewo amesafirishwa bila wakili wake kuwa na taarifa kuwa amepelekwa Mwanza, wala mke wake aliyeambiwa ampelekee  chakula, lakini alipofika polisi aliambiwa mume wake hayupo.
Mmoja wa mawakili wanaokwenda Igunga kuwatetea Kilewo na wenzake, Profesa Abdallah Safari alisema wameshitushwa kusikia wateja wao wamelazimishwa kutoa maelezo ili kuwahusisha viongozi wakuu wa CHADEMA.
Alibainisha kuwa kutokana na kesi hiyo kuonekana kujaa masuala ya kisiasa, atashirikiana na mawakili wenzake ambao ni Peter Kibatala na Gasper Mwalyela na kama itakapolazimika watawaongeza Mabere Marando, Kicheere, Method Kimomogoro na Lissu.
Aliongeza kuwa imefika hatua itabidi atumie kifungu cha sheria cha 102, ili kujenga dhana ya kutiliwa shaka kwani viongozi wote wa CHADEMA sasa wamefunguliwa kesi katika maeneo mbalimbali nchini, huku wale wa CCM wakiachwa.
Profesa Safari alitolea mfano Mbunge wa Tabora mjini, Ismail Aden Rage, ambaye alipatwa na hatia katika uchaguzi wa Igunga na alipaswa kufungwa miaka mitatu bila fidia, lakini DPP amekalia faili lake hadi sasa.
Aliongeza kuwa mambo hayo yanajitokeza kutokana na CHADEMA kumtaja ofisa wa usalama anayeitwa Shaali Ally kuwa ndiye aliwatafuta vijana wa chama hicho akiwemo Ahmed Sabula na wenzake.
Alibainisha kuwa Machi 29, mwaka huu vijana hao waliitwa na Shaali katika chumba cha hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam, akiwataka wakubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya CHADEMA, kuwasilisha kwake nyaraka za kamati kuu na kueleza mipango ya chama katika kesi ya Lwakatare.
Kwenye mpango huu, ofisa huyo wa usalama wa taifa ambaye Marando alisema anamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha sh milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa kama ujira kwa kukubali kutoa ushahidi dhidi ya Lwakatare.

Chanzo:TANZANIA DAIMA

Mwanamke Iringa ateketeza watoto wa jirani yake kwa wivu wa mapenzi

Picha hii haihusiani na habari hii, ila inaonyesha taswira ya nyumba iliyoteketea kwa moto
 MWANAMKE mmoja anayefahamika kwa jina la Taraji Muenzi, 31, mkazi wa kijiji cha Mwatasi, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa la kuichoma nyumba ya jirani yake na kuwateketeza watoto wawili waliokuwa ndani mwake pamoja na vitu vyote katika nyumba hiyo kwa kilichoelezwa wivu wa mapenzi.
Habari kutoka mkoani humo zinasema watoto walioteketezwa wakiwa ndani ya nyuma hiyo ni Faraji, 6 na Jacob, 3 ambao walikuwa watoto pekee wa Subira Kisitu aliyekuwa akituhumiwa na mtuhumiwa huyo kuwa anatembea na mumewe.
Inaelezwa kuwa Taraji kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu jirani yake kumuibia mume na kumchimba mkwara kwamba atamfanyizia, kiasi cha uongozi wa eneo lao kuitisha kikao na kumtwanga faini ya Sh 10,000 aliotakiwa kuilipa juzi, Juni 22 siku aliyofanya tukio hilo.Inaelezwa uongozi wa kitongoji hicho kiliamua kumtoza faini baada ya wiki iliyopita kumvamia jirani yake nyumbani kwake na kumwagia mboga na kusisitiza kuwa kuna kitu atakachomfanyia ambacho hatasahau maishani kama siyo kwa kumuua kwa sumu basi kwa kumchomea moto nyumba yake.
Hata hivyo inaelezwa kuwa jana juzi usiku akiamini kuwa jirani yake yupo ndani na wanawe aliamua kuichoma moto nyumba hiyo, ila kwa bahati mbaya jirani zake alikuwa klabuni akipata kinywaji na hivyo watoto pekee waliokuwa wamelala ndani ndiyo waliougua na kufa pamoja na mali zote.
Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza wanamshikilia mwanamke huyo ili kumfikisha mahakamani kwa kitendo alichokmifanya ambacho kimeacha gumzo kijiji cha Mwatasi, huku familia ya watoto ikiwa katika majonzi makubwa ya kupoteza watoto wao.

Sunday, June 23, 2013

Mbunge Sugu amuomba radhi Waziri Mkuu, kisa...!

Mhe Sugu
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda
BAADA ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."

Kiemba, Sure Boy ndiyo Wanasoka Bora Tanzania 2012

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akimpa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi, Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam

KIUNGO nyota wa timu ya Simba na Taifa Stars, Amri Kiemba amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Tanzania iliyotolewa na Chama cha Wanasoka Tanzania, SPUTANZA, katika hafla iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam.
Kiemba amenyakua tuzo hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Pepsi kwa ufanisi wake kwa msimu uliopita ambapo amekuwa katika kiwango cha juu akiisaidia kuifungia simba mabao 8 kwa msimu uliopita huku akiibeba Stars katika mechi zake za kimataifa.
Naye kiungo mwenye mapavu ya mbwa, Abubakar Salum 'Sure Boy' alinyakuwa tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi, tuzo ambayo alistahili kutokana na umahiri wa mchezaji huyo anayeichezea Azam na Taifa Stars.
Wengine walionyakua tuzo katika hafla hiyo ni kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif 'Casillas' aliyekuwa Kipa Bora wa Mwaka na kocha Mecky Mexime wa Mtibwa.
MICHARAZO inawapa pongezi wote waliotwaa tuzo hizo na kuwatakia mafanikio mema, kadhalika inawapa heko SPUTANZA na wadhamini wa tuzo hiyo ya kwanza kuandaliwa na chama hicho.

Orodha nyingine ya Form 6 wanaotrakiwa kwenda JKT



JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YA RUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT WWW.JKT.GO.TZ. 

ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO.

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAULU KWA DIVISION I, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.



Kwa taarifa zaidi (imenukuliwa kutoka): JKT.go.tz

bulombora.pdf
File Size: 826 kb
File Type: pdf
Download File


kanembwa.pdf
File Size: 674 kb
File Type: pdf
Download File


maramba.pdf
File Size: 342 kb
File Type: pdf
Download File


mgambo.pdf
File Size: 810 kb
File Type: pdf
Download File


mlale.pdf
File Size: 729 kb
File Type: pdf
Download File


msange.pdf
File Size: 1262 kb
File Type: pdf
Download File


ruvu.pdf
File Size: 903 kb
File Type: pdf
Download File


rwamkoma.pdf
File Size: 569 kb
File Type: pdf
Download File

Zola D aachia za zamani

Zola D katika pozi
MKALI wa miondoko ya Hip Hop nchini, David Michael 'Zola D', ameachia 'audio' za nyimbo zake za zamani baada ya kuombwa na mashabiki wake.
Zola D alisema nyimbo hizo zilizoachiwa video zake na kufanya mashabiki kutaka kusikia 'audio' ni zile zilizorekodiwa kati ya mwaka 2007 mpaka mwaka juzi na tayari baadhi zipo kwenye mitandao ya kijamii.
"Nimeachia 'audio' za nyimbo kama tano hivi za zamani ukiwemo nilioimba na Baby Madaha baada ya kuombwa na mashabiki waliotaka kuusikia baada ya kuiona video yake, " alisema.
Zola D alisema kwa sasa baada ya kutoka kwenye misiba ya wasanii wenzake, Albert Mangweha aliyewahi kuimba naye wimbo na Langa Kileo anajipanga kutoa kazi mpya kwa mashabiki na kufuatiwa na albamu kamili itakayokuwa na jumla ya nyimbo 21.

MAAJABU: HII NDIYO KAZI YA UUMBAJI YA MUNGU


Maajabu  ya  uumbaji  yamemfanya  mama  mzazi  wa  Xiao Wei  ambaye  ni  mchina amwage  machozi  akiomba  msaada  wa  kunusuru  maisha  ya  mwanae   mwenye  umri  wa  miezi  7 aliyezaliwa  na  makalio  matatu...
Kalio  la  tatu  lipo  kama  mkia  mfupi, wenye  urefu  wa   sentimita  8  ( 8 cm ), katikati  ya  makalio  mengine  mawili.
Akiongea   kwa  uchungu, mama  mzazi  wa  mtoto  huyo  amedai  kuwa  kwa  muda  mrefu  amekuwa  akiwaomba  madaktari  wafanye  upasuaji  wa  tako  hilo  lakini  wao  wamekuwa  wakimjibu   kuwa  hiyo  si  kazi  nyepesi  kama  anavyodhani....
"Tukilikata  litaota  tena, hivyo  hatutakiwi  kukurupuka  na  badala  yake  tutakiwa  kupata  muda  wa  kupitia  vitu  vingi  ukiwemo  mrija  wa  uti  wa  mgongo  ambapo  kalio  hilo  limejiegesha"...Alisema  daktari  mmoja  akimjibu  mama  huyo.
 

Una tatizo la nguvu za kiume au za kike? Soma hapa!

KITABU AMBACHO KINATOA TIBA ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI IKIWEMO MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZA MAJANI SASA KIPO MITAANI KINAPATIKANA MITAA YA UHURU NA MSIMBAZI KWA MAHITAJI YA KITABU HIKI NA DAWA MBALIMBALI ZA KUTIBU MARADHI PAMOJA NA MATATIZO PIGA SIMU  0787406938

Vumbi awataka Choki, Asha Baraka kumaliza tofauti zao

Ally Choki

Asha Baraka

Alain Dekula Kahanga 'Vumbi'
MWANAMUZIKI wa zamani wa bendi ya Marquiz Original, Alain Dekula 'Vumbi' anayefanya shughuli zake za muziki nchini Sweden, amewasihi wakurugenzi wa bendi za Extra Bongo, Ally Choki na mwenzake wa African Stars 'Twanga Pepeta' Asha Baraka kumaliza tofauti zao.
Vumbi alisema amekuwa akifuatiliwa malumbano baina ya wakurugenzi hao kupitia mitandao ya kijamii na kushangazwa kusikia wawili hao wakiapiana kutozikana wala kuhudhuria mazishi ya mwenzake akidai hadhani ni jambo zuri au lenye tija kwa muziki wa Tanzania.
Mcharaza gitaa la solo huyo, alisema ni vyema wawili hao wakaa chini na kumaliza tofauti zao kwa masilahi ya muziki wa Tanzania ambao alidai bado una kazi pevu kuweza kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania kama alivyoutangaza marehemu Dk Remmy na kundi la Tatu Nane.
"Sifurahishwi na uhasama unaoendelea baina ya Asha Baraka na Ally Choki, ningependa wakae chini na kuzika tofauti zao kwa masilahi ya muziki wa Tanzania, malumbano kati ya makundi siyo jambo jipya, lakini haikuwahi kufikia watu kukataliana kuzikana," alisema Vumbi.
Vumbi alisema anafahamu 'bifu' za kisanii hufanywa kokote duniani kwa lengo la kuongeza soko na kuvuna mashabiki, lakini siyo kama uhasama uliopo baina ya watu hao wawili ambao ni moja ya mihimili mikubwa ya muziki wa dansi Tanzania kwa kusaidia ajira ya watu wengi.
"Naomba unifikishie salamu zangu wakae chini na kusameheana kama kuna tatizo baina yao, ili kusaidia dansi lizidi kusonga mbele, malumbano na 'bifu' zitumike kuinua soko la muziki na sio  kuwekeana kinyongo kama ninachosikia na kukisoma mitandaoni," alisema.
Kauli ya Vumbi imekuja baada ya wakurugenzi hao kunukuliwa wakiapiana kwamba 'hawapendani' na katu mmoja wao asihudhurie wala kumzika mwenzake akitangulia kufa kutokana na kutofautiana mara baada ya kuachana kufanya kazi sehemu moja.
Choki alikuwa mmoja wa wanamuziki wa Twanga Pepeta akiingia na kutoka kabla ya kuanzisha Extra Bongo ambayo imekuwa ikiwanyakua wanamuziki toka kwa wapinzani wao hao, huku yeye akifikishwa mahakamani akidai gari analodai alipewa kwa makubaliano.

MASHALI, MIYEYUSHO WAJIFUA KUWAVAA WAKENYA


Francis Miyeyusho (kulia) akimtupia konde Thomas Mashali wakati wa mazoezi jana

  Miyeyusho akijifua kumkabili bondia Shadrack Machanje kutoka Kenya.
  Mashali akipasha tayari kuzipiga na bondia Patrick Amote wa Kenya.
Mabondia hao katika pozi la kuzipiga wakati wa mazoezi ya jana Francis Miyeyusho (kulia) akimtupia konde Thomas Mashali wakati wa mazoezi jana
 Mashali (kushoto) akikwepa konde la Miyeyusho. ---
 Mabondia wa hapa nchini Thomas Mashali na Francis Miyeyusho Jana wamefanya mazoezi ya pamoja katika gym iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Mabondia hao wanajiandaa kuwakabili wenzao kutoka Kenya ambao ni Patrick Amote na Shadrack Muchenje kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.PICHA NA MUSA MATEJA / GPL

Ommy Lax, PNC kupotezea videoni

Ommy Lax
MSANII anayekuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya Iman Omar 'Ommy Lax' anajiandaa kurekodi video ya wimbo wake mpya uitwao 'Wapotezee' alioimba na mkali wa Watanashati, PNC.
Akizungumza na MICHARAZO, Ommy Lax alisema kuwa maandalizi ya kuanza kurekodi video hiyo imekamilika na kwamba zoezi hilo litafanyika wiki hii katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam.
Ommy Lax alisema kuwa 'audio' wa kibao hicho tayari imeanza kurushwa hewani na ameona ni vyema kukata kiu ya mashabiki wake kwa kuwatengenezea video ili waone kwa ukamilifu ujumbe wa wimbo huo.
"Baada ya kuachia 'audio' kwa sasa nafanya maandalizi ya kurekodi video ya wimbo wangu uitwao 'Wapotezee' ambao nimeimba kwa kumshirikisha PNC, nimepanga kurekodi wiki ijayo ili niisambaze mapema," alisema Ommy Lax.
Hicho ni kibao kingine toka kwa msanii huyo ambaye anatamba na wimbo wa Kioo Changu alioimba na Matonya 'Tonya Business'.

Miaka 13 ya Kikosi ilikuwa noumaa, Kalapina afunika, Chid ndani ya nyumba


 Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam. (Picha zote na Habari Mseto Blog).
 Chid Benz
 Fukuda akichana mistari
 Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi  akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.
Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi. 
 Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.
   
 Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza
 
 Afande Sele akipagawisha  mashabiki.