STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 30, 2013

Mrembo Miss Utalii Tanzania kupaa kesho kwenda Equatorial Guinea

Miss Utalii Tanzania 2013

MREMBO wa Miss Utalii Tanzania 2013, Khadija Mswaga anatarajiwa kuondoka nchini kesho kuelekea Equatorial Guinea kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kusaka mrembo wa Utalii Duniani 'Miss Tourism World 2013'.
Shindano hilo la urembo la dunia litafanyika katika nchi ya Equatorial Guinea ambapo warembo wa nchi 126 wanatarajiwa kuchuana kuwania taji hilo.
Rais wa Bodi ya Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps' aliiambia MICHARAZO kuwa mrembo huyo wa Tanzania ataondoka kesho Jumanne kwa ndege ya kampuni ya Ethiopia kuelekea nchini humo tayari kwa kinyang'anyiro kitakachofanyika Oktoba 12.
Chipungahelo alisema mwakilishi wao anaenda katika shindano hilo akiwa amebeba ujumbe wa kutangaza hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya dunia Afrika.
Mrembo huyo alisema ameamua kubeba ujumbe huo kwa sababu ni hifadhi ya kipekee duniani ambayo pia inaelezewa ndiyo chimbuko la binadamu wa kwanza na sehemu pekee binadamu anaishi na wanyama kwa ushirikiano bila kudhuriana.
Mrembo huyo alisema ana imani kubwa ya kufanya vizuri katika shindano hilo ili kuifuta machozi Tanzania ambayo imekuwa na bahati mbaya ya kufanya vibaya katika kila shindano la kimataifa inayoshiriki duniani.

Mabao 90 yatinga Ligi Kuu, Mrundi azidi kupepea Ashanti bado 'gonjwa'

Tambwe Amissi akishangilia moja ya mabao yake
JUMLA ya mabao 90 mpaka sasa yametinga wavuni wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa raundi ya sita, huku Mrundi Tambwe Amissi akiendelea kuongoza orodha ya wafungaji Bora akiwa  magoli saba.
Tambwe alionmgeza bao jingine jana wakati Simba walipoizamisha JKT Ruvu kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa na kuwaacha mbali wachezaji wenzake wanaomfukukizia katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.
Mfungaji Bora huyo wa Kagame Cup 2013, alifunga bao lake la saba katika mechi tatu mfululizo kwa mkwaju wa penati kabla ya Ramadhani Singano 'Messi' kuongeza la pili na kuifanya 'Mnyama' izidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 14 na mabao 15 ya kufunga na kufungwa manne.
Simba ikionekana kuwa na safu kali ya ushambuliaji, Ashanti imeendelea kuwa timu yenye ukuta mwepesi baada ya kuruhusu jumla ya mabao 14 huku yenyewe ikifunga mabao manne tu.
Matokeo ya mwishoni mwa wiki ya ligi hiyo imevuruga kabisa msimamo wa kwa baadhi ya timu kupanda nafasi za juu nyingine zikiporomoka, Kagera Sugar na Coastal Union zikichekelea huku, timu 'ndugu' za JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikiporomoka katika msimamo huo.
Kagera iliyopata ushindi ugenini dhidi ya Rhino Rangers imekwea hadi nafasi ya pili nyuma ya Simba ikiwa na pinti 11, huku Coastal na Azam zilizoambulia sare jijini Mbeya zikikalia nafasi ya tatu zikiwa na pointi 10 kila moja, kisha kufuatiwa na Yanga, JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikiwa nafasi ya nne na pointi zao 9.
Ashanti imeendelea kukalia mkiani ikiwa na pointi mbili tu baada ya jana kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo Jumapili ijayo itashuka dimba la Taifa kuikabili Yanga mabingwa watetezi wa taji hilo.
Msimamo kamili wa ligi hiyo baadfa ya mechi za jana ni kama ifuatavyo;

                                  P  W  D  L    F  A  GD  PTS
1.  Simba                    6   4   2   0  15  4  11   14
2. Kagera Sugar         6   3   2   1   7   3    4   11
3. Azam                     6    2   4   0   9   6   3   10
4. Coastal Union        6    2   4   0   6   3   3   10
5. Yanga                    6    2   3   1  11  7   4   9
6. JKT Ruvu              6    3   0   3   6   4   2    9
7.  Ruvu Shooting      6    3   0   3   6   4   3    9
8.  Mbeya City          6   1   5   0   6   5   1    8
9.  Rhino Rangers      7   1   4   2   7   8   -1   7
10.Mtibwa Sugar       6   1  4   1   5   6    -1   7
11.Oljoro                   6   1   2   3   3   6   -3   5
12.Mgambo               6   1   2   3   2  10  -8   5
13.Prisons                  6   0   4   2   3    9   -6   4
14.Ashanti                  7   0   2   5   4  15 -11  2
 
Wafungaji Bora:

7- Tambwe Amisi (Simba)
3- Jerry Tegete , Didier Kavumbagu (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Kipre Tchetche (Azam), Peter Michael (Prisons)
2- Jonas Mkude (Simba), Jerry Santo, Haruna Moshi (Coastal Union), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Paul Nonga, Mwagani Yeya (Mbeya City), Hamis Kiiza (Yanga), Themi Felix (Kagera Sugar), Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla,(Coastal Union), Henry Joseph, Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris,  John Bocco, Joseph Kimwaga (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Juma Luzio, Masoud Ally, Shaaban Nditti, (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Tumba Swedi, Paul Maono (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Salum Machaku, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Godfrey Wambura, Clement Douglas (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary, Paul Malipesa (Oljoro JKT)

Matokeo ya mechi zilizopita

Agosti 24, 2013Yanga vs Ashanti United (5-1)
Mtibwa Sugar vs Azam (1-1)
Oljoro JKT vs Coastal Union (0-2)
Mgambo JKT vs JKT Ruvu (0-2)
Rhino Rangers vs Simba (2-2)
Mbeya City vs Kagera Sugar (0-0)
Ruvu Shooting vs Prisons (3-0)

Agosti 28, 2013Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar (1-0)
Rhino Rangers vs Azam (0-2)
JKT Ruvu  vs Prisons (3-0)
Mbeya City vs Ruvu Shooting (2-1)
Mgambo  vs Ashanti United (1-0)
Oljoro JKT vs Simba (0-1)
Yanga  vs Coastal Union (1-1)

Sept 14, 2013Simba  vs Mtibwa (2-0)
Coastal Union  vs Prisons (0-0)
Ruvu Shooting va Mgambo JKT (1-0)
Oljoro JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Mbeya City  vs Yanga (1-1)
Kagera Sugar vs Azam (1-1)
Ashanti United  vs JKT Ruvu (0-1)

Sept 18, 2013Prisons vs Yanga (1-1)
Simba vs Mgambo JKT (6-0)
Kagera Sugar vs JKT Oljoro (2-1)
Azam  vs Ashanti United (1-1)
Coastal Union  vs Rhino Rangers (1-1)
Mtibwa Sugar  vs Mbeya City (0-0)
Ruvu Shooting vs  JKT Ruvu (1-0)

Sept 21, 2013Mgambo JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Prisons vs Mtibwa Sugar (1-1)
Simba vs Mbeya City (2-2)
Kagera Sugar vs Ashanti United (3-0)

Sept 22, 2013JKT Ruvu vs Oljoro JKT (0-1)
Azam  vs Yanga (3-2)
Coastal Union v Ruvu Shooting (1-0)

Sept 25, 2013
Rhino Rangers vs Ashanti Utd (2-0)

Sept 28, 2013Yanga vs Ruvu Shooting (1-0)
Rhino Rangers v Kagera Sugar (0-1)
Mbeya City vs Coastal Union (1-1)
Mgambo JKT vs Oljoro JKT (0-0)

Sept 29,2013
Ashanti Utd vs Mtibwa Sugar (2-2)
JKT Ruvu vs Simba (0-2)
Prisons vs Azam (1-1)

Mechi zijazo katika ligi hiyo
Okt 05, 2013Ruvu Shooting vs Simba
JKT Ruvu vs Kagera Sugar
Coastal Union vs Azam
Oljoro JKT vs Mbeya City

Okt 06, 2013

Mgambo JKT vs Prisons
Yanga vs Mtibwa Sugar

Rich Richie ana mbili kwa mpigo

Rich Richie
MUIGIZAJI nyota ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu, Single Mtambalike 'Richie' yupo njia panda asijue ni filamu ipi kati ya mbili mpya alizozikamilisha kwa mkupuo aanze kuiingiza sokoni.
Filamu hiyo alizofyatua mkali huyo aliyeewahi kutamba na michezo ya runinga kupitia vituo vya televisheni vya ITV na CTN, ni 'Kitendawili' na 'Likizo Hii'.
Richie alisema hajui hadi sasa filamu ipi kati ya hizo aanze kuingiza sokoni kutokana na zote kuwa bomba kwa ujumbe wake na namna washiriki wake walivyozitendea haki.
"Kwa kweli nipo njia panda mpaka sasa sijui nianze na 'Kitendawili' au 'Likizo Hii' ambazo nimezikamilisha hivi karibuni na zote zimechezwa na wasanii nyota nchini," alisema Richie.
Aliwataja baadhi ya wasanii waliozishiriki filamu hizo ni pamoja na Mzee Majuto, Chuchu Hans, Maringo Saba, Baba Haji na wengine.

Francis Miyeyusho 'amyeyusha' Momba kwa pointi

Bondia Sadiki Momba (kushoto) akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika jana Jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es Salaam. Miyeyusho alishinda kwa pointi 
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi 
Mwamuzi Sako Mtilya akimnyanyua mkono juu bondia  Francis Miyeyusho baada ya kumshinda kwa pointi mpinzani wake  Sadiki Momba wakati wa mpambano wao
Bondia Mussa Sunga kushoto akipambana na Fadhili  Awadh wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili. Awadh alishinda kwa Point 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis, Manny Pacquaio,Muhammed Ali, Floyd Mayweather, na wengine kibao
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis, Manny Pacquaio,Muhammed Ali, Floyd Mayweather, na wengine kibao
Baadhi ya raia wa kigeni kutoka china waliokuja kumsapoti bondia Mussa Sunga wakiwa katika picha ya pamoja na bondia huyo
DVD KALI ZA MCHEZO WA NGUMI ZINAZOSAMBAZWA NA KOCHA SUPER D
Mashabiki wa mchezo wa masumbwi



BINGWA wa Kimataifa wa Ngumi za Kulipwa anayetambuliwa na IBO, Francis Miyeyusho ameendeleza rekodi yake ya kuwachakaza wapinzani wake baada ya mwishoni mwa wiki kumshinda kwa pointi Sadick Momba.
Miyeyusho alipata ushindi huo siku ya Jumapili katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa kwenye ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho aliyemchakaza hivi karibuni Mzambia Fidelis Lupupa, alionyesha tangu mwanzoni mwa mchezo huo dhamira yake ya kuibuka ushindi, licha ya Momba kuonyesha upinzani mkubwa.
Wakiviziana na kudonoana kwa zamu, mabondia hao walijikuta wakimaliza pambano hilo la uzito wa bantam bila mashabiki kutabiri mapema nani mshindi kutokana na waliovyoonyesha upinzani katika mchezo huo.
Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo na majaji kutoa matokeo yao, mwamuzi Sako Mtilya alimtangaza Miyeyusho kuwa ndiye mshindi na kufanya mashabiki waliofurika kwenye ukumbi huo kumshangilia bondia huyo.
Huo ni ushindi wa 12 mfululizo kwa Miyeyusho ndani ya ardhi ya Tanzania tangu Aprili 2009 akiwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo katika kipindi hicho, bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 47 na kushinda 36 akipoteza 10 na kuambulia sare mbili alishatoka nje ya nchi mara tatu na mara zote kudundwa na wapinzani wake kwa KO.
Katika pambano jingine la utangulizi Fadhili Awadh alimshinda kwa pointi Mussa Sunga katiika pambano lililokuwa limekaa ufundi.