STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 5, 2013

Hii ndiyo hutoba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Watanzania

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, TAREHE 4 OKTOBA, 2013
Ndugu Wananchi;
          Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza mwezi Septemba salama na kuwasiliana kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri.  Naomba radhi kuzungumza nanyi siku ya leo kwa sababu nilikuwa safari na nilirejea jioni ya tarehe 30 Septemba, 2013.   Awali nilifikiria nisiseme, nisubiri mwisho wa mwezi wa Oktoba.  Lakini, baada ya kupata taarifa ya yaliyojiri, nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia.  Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno.  Nitayatafutia mahali pengine pa kuyasemea.
Uhusiano na Rwanda
Ndugu Wananchi;
          Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Julai, nilizungumzia hali ya uhusiano wetu na Rwanda kutokuwa mzuri na tatizo la ujambazi na wahamiaji haramu katika Mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera.  Nafurahi kusema kuwa kwa yote mawili kuna maendeleo ya kutia moyo.
          Tarehe 5 Septemba, 2013, nilikutana na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Paul Kagame wa Rwanda mjini Kampala.  Tuliitumia fursa ya ushiriki wetu katika Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia uhusiano baina yetu na nchi zetu.  Mazungumzo yalikuwa mazuri na sote tulikubaliana kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo.  Kwa sababu hiyo tulielewana kuwa tutengeneze mazingira yatakayosaidia kutuliza hali na kurudisha nchi zetu katika uhusiano mwema kama ilivyokuwa siku zote.  Nawaomba ndugu zangu hususan wanasiasa, watumishi wa umma, wanahabari na wenye mitandao ya kijamii na blog na wananchi kwa ujumla tusaidie kuimarisha uhusiano mwema baina ya Rwanda na Tanzania na watu wake.
Majambazi na Wahamiaji Haramu
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba hiyo pia nilisema kuwa tutachukua hatua thabiti dhidi ya majambazi na wageni wanaoishi nchini bila ya kuzingatia taratibu zinazohusika.  Niliwataka majambazi wajisalimishe wao na silaha zao kwa hiari.  Wale wanaoishi nchini bila ya kuwa na kibali halali wahalalishe ukaazi wao au warejee makwao.  Nilitoa siku 14 kuanzia tarehe 29 Agosti, 2013 wafanye hivyo kwani baada ya hapo tungeanzisha operesheni maalum ya kushughulika na watu wa makundi yote mawili.
Ndugu Wananchi;
          Kumekuwepo na mafanikio ya kutia moyo.  Kwa upande wa wahamiaji wanaoishi nchini kinyume cha sheria watu wapatao 21,254 waliondoka kwa hiari.  Hali kadhalika zaidi ya ng’ombe 8,000 waliondolewa na silaha 102 zilisalimishwa.   Baada ya operesheni kuanza tarehe 6 Septemba, 2013 na kumalizika tarehe 20 Septemba, 2013, wahamiaji haramu 12,828 walirejeshwa makwao na watuhumiwa 279 wa unyang’anyi wa kutumia silaha walikamatwa.  Aidha, mabomu 10 ya kutupa kwa mkono (offensive hand grenades), silaha 80, risasi 780 na mitambo 2 ya kutengeneza magobole vilikamatwa.  Pia, ng’ombe 8,226 walikamatwa wakichungwa katika mapori ya hifadhi.  Kwa upande wa mazao ya misitu, mbao 2,105 zilikamatwa pamoja na nyara mbalimbali za Serikali.
Ndugu Wananchi;
          Agizo la kuwataka watu wanaoishi nchini isivyo halali wahalalishe ukaazi wao au waondoke kwa hiari au wataondolewa lilipotoshwa hasa na vyombo vya habari vya nje ya Tanzania.  Walikuwa wanadai eti Tanzania ilikuwa inafukuza wakimbizi.  Madai hayo si ya kweli hata kidogo.   Hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2013 wakimbizi 68,711 walikuwepo kwenye Kambi ya Nyarugusu, Mkoani Kigoma.  Hakuna mkimbizi ye yote aliyetakiwa kuondoka.  Ukweli ni kwamba hakuna mtu ye yote kati ya wale watu walioondoka kwa hiari au kusaidiwa kuondoka wakati wa operesheni ambaye ni mkimbizi.  Kama ingekuwa hivyo, wa kwanza kulalamika wangekuwa wenzetu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa.  Bahati nzuri jambo hilo halikutokea.
Ndugu Wananchi;
          Yalikuwepo pia madai kwamba tunawaonea na kuwatesa watu walioishi nchini miaka mingi.  Ati iweje sasa ndiyo waambiwe kuwa siyo raia.  Siku zote Serikali ilikuwa wapi? Uraia haupatikani kwa kuishi nchi ya kigeni kwa miaka mingi.  Unapatikana kwa kutimiza masharti ya kuomba na kupewa uraia.  Kama mtu hakufanya hivyo anabaki kuwa raia wa nchi aliyotoka au walikotoka wazazi wake.  Ipo mifano ya watu mashuhuri ambao walilazimika kuachia nyadhifa zao baada ya kugundulika kuwa siyo raia.  Hawakuwa wanaonewa, ndiyo matakwa ya Katiba na Sheria za nchi yetu.
Ndugu Wananchi;
          Katika kutekeleza operesheni hii niliagiza kuwa wale watu ambao wameishi hapa nchini miaka mingi ambao wana nyumba, mashamba au mali mbalimbali au wameoa au kuolewa na wana watoto au hata wajukuu waelekezwe kuhalalisha ukaazi wao.  Iwapo watakataa kufanya hivyo basi wasaidiwe kurejea kwao.  Pia niliagiza watu wasiporwe mali zao wala kudhulumiwa.  Sijapata taarifa ya kufanyika kinyume na maelekezo yangu.  Lakini kama wapo watu waliotendewa tofauti, taarifa itolewe kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa au hata Ofisi ya Rais ili hatua zipasazo zichukuliwe.  Hatutaki watu wadhulumiwe au kuonewa.
          Napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Waziri wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi kwa uongozi wao mzuri katika zoezi hili.  Pia, nawapongeza Makamanda na askari wa JWTZ na Polisi pamoja na maafisa wa Idara ya Uhamiaji, Idara ya Mifugo, Idara ya Wanyamapori, Idara ya Misitu na Idara nyinginezo za Serikali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya.  Najua awamu ya kwanza imeisha tarehe 20 Septemba, 2013 na kama nilivyosema kuwa safari hii operesheni itakuwa endelevu, muda si mrefu awamu ya pili itafuata.  Nawaomba waendelee kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu ya hali ya juu.
Ziara ya Canada na Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 17 na 28 Septemba, 2013 nilifanya ziara ya kikazi katika nchi za Canada na Marekani.  Nchini Canada nilitembelea Chuo Kikuu cha Guelph ambapo nilitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua jitihada zetu tuzifanyazo kujiletea maendeleo na mafanikio ya kutia moyo tunayoendelea kupata licha ya changamoto zinazotukabili.  Katika mazungumzo yangu na uongozi wa chuo hicho wamekubali kuwa na ushirikiano wa karibu na Wizara zinazohusika na Elimu, Kilimo na Mifugo pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine,  Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma.  Nimewataka Mawaziri wa Wizara hizo na viongozi wa vyuo hivyo kuchangamkia fursa hiyo bila kuchelewa. 
Ndugu Wananchi;
Nchini Marekani nilikutana na kuzungumza na maafisa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya nchi hiyo wakiwemo Rais Barack Obama na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Marekani.  Mazungumzo yetu yalilenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zetu na mambo yalienda vizuri.  Wote walituhakikishia kuwa mambo tuliyoyazungumza na kukubaliana na Rais Barack Obama wakati wa ziara yake nchini yanaendelea kufanyiwa kazi.  Miongoni mwa hayo maombi yetu ya kupatiwa vitabu milioni 2.4 vya sayansi na hisabati yamekubaliwa na utekelezaji umeanza.  Upatikanaji wa vitabu hivyo utamwezesha kila mwanafunzi wa sekondari kuwa na kitabu chake.
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na la faraja kwetu ni kuwa mapendekezo yetu ya miradi ya umeme na barabara za vijijini za kugharamiwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lao la Changamoto za Milenia yamepokelewa vizuri.  Kinachosubiriwa ni miradi ipi itakubaliwa na Bodi ya MCC na kiasi gani cha fedha kitatengwa na Bunge la Marekani kwa ajili hiyo.
Tuzo ya Uhifadhi
Jambo lingine muhimu katika safari yangu ya Marekani ni kutunukiwa tuzo na “International Congressional Conservation Foundation” kwa kutambua juhudi zetu katika kuhifadhi wanyama pori na mafanikio tuliyoyapata.  Licha ya changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, tuzo hii imetupa moyo wa kuongeza nguvu katika jitihada tunazozifanya sasa kupambana na ujangili na matatizo mengine ya uhifadhi wa wanyama na misitu. 
Ndugu Wananchi;
Kilichotupa moyo zaidi ni kauli za utayari wa kutusaidia katika mapambano hayo zilizotolewa wakati wa kupewa tuzo na katika mkutano wa mfuko wa Maendeleo wa Clinton na katika mkutano maalum wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo duniani.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ndugu Wananchi;
Shabaha kuu ya safari yangu ya Marekani ilikuwa kuhudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York mpaka Desemba, 2013.  Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni kuandaa agenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yaani: Post 2015 Development Agenda:  Setting the Stage. Kama mtakavyokumbuka Malengo ya Milenia yaliyoamuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, yanafikia ukomo wa utekelezaji wake mwaka 2015. 
Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu mjadala umehusu nini kifanyike baada ya mwaka 2015.  Hata hivyo, mjadala huo unaanza kwa kufanya tathmini ya utekelezaji wa yale Malengo Manane ya Milenia ya mwaka 2000 umefikia wapi mpaka sasa na utafikia wapi mwaka 2015 kwa kila nchi na kwa dunia kwa ujumla.  Tathmini ya jumla inaonesha kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa ya kutekeleza malengo haya katika kila nchi.  Yapo malengo ambayo utekelezaji wake umefikia shabaha hivi sasa na yapo ambayo upo uwezekano wa shabaha kufikiwa ifikapo mwaka 2015.  Vile vile yapo ambayo shabaha haitafikiwa. 
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wetu, Tanzania, tumefikia shabaha katika mambo yafuatayo: 
(1)                Lengo la Milenia namba 2 kuhusu uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule ya msingi;
(2)            Lengo la Milenia namba 3 hasa kuhusu usawa wa kijinsia katika Shule za Msingi na Sekondari.  Ukweli ni kwamba, wasichana wanaanza kuwa wengi kuliko wavulana.  Hatujafikia shabaha kwa upande wa usawa wa kijinsia katika elimu ya juu na ni vigumu kulifikia ifikapo 2015.  Pia hatujafikia lengo kwa upande wa usawa wa Wabunge wanawake na wanaume.  Hata hivyo, kwa kutumia mchakato wa Katiba unaoendelea sasa tunaweza kufikia lengo katika uchaguzi wa 2015 iwapo tutaamua iwe hivyo;
(3)            Lengo la Milenia namba 4 kuhusu kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano;
(4)            Tumefikia shabaha kwa Lengo la Milenia Namba 6 kuhusu  kupunguza maambukizi ya UKIMWI; na
(5)            Kwa upande wa lengo namba 7 kuhusu mazingira, tumefikia shabaha kwa upande wa upatikanaji wa maji mijini.  Bado tuko nyuma kwa maji vijijini ingawaje tunaweza kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 kama tutaendeleza uwekezaji tulioamua kufanya katika bajeti ya mwaka huu.  Lakini, hatutaweza kufikia shabaha kwa upande wa usafi wa mazingira mijini na vijijini ifikapo mwaka 2015.  Safari bado ndefu sana.
Ndugu Wananchi;
Malengo ya Milenia namba 1 na namba 5 ambayo bado tuko nyuma sana ya shabaha hatutafikia lengo ifikapo 2015.  Tumeendelea kutekeleza lengo la Milenia namba 1 kuhusu kupunguza umaskini na njaa kwa zaidi ya nusu kutoka kiwango cha mwaka 2000.  Hatua tunazochukua kuleta mageuzi katika kilimo zina lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza mapato ya wakulima.  Mafanikio yanaanza kuonekana lakini si ya kiwango cha kutufikisha kwenye lengo ifikapo mwaka 2015.  Tunao, pia, mpango wa kupanua programu ya TASAF ya Conditional Cash Transfer ili tuwafikie watu wengi maskini.   Hata kama tutafanikiwa kuutekeleza mapema mpango huu utatusogeza sana mbele lakini bado tutakuwa chini ya lengo kwa upande wa kupunguza umaskini ifikapo 2015.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Lengo  la Milenia namba 5, kuhusu afya ya kina mama wajawazito bado tuko nyuma katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na kuongeza idadi ya wajawazito wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.  Hatutaweza kufikia shabaha ifikapo mwaka 2015.  Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (2007 – 2017) una nia ya kukabiliana na matatizo haya.  Tumeongeza ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali, tumeboresha upatikanaji wa dawa na tumepanua sana mafunzo ya madaktari, wauguzi na wakunga mambo ambayo yamesaidia kutufikisha hatua tuliyopiga mpaka sasa. Naamini juhudi zetu tukiziendeleza zitatusogeza mbele zaidi ingawaje bado tutakuwa chini ya lengo.  Miaka michache ijayo, tatizo hili nalo litakuwa historia.
Ndugu Wananchi;
Lengo la Milenia namba 8 linazihusu nchi tajiri kuongeza michango yao kusaidia nchi zinazoendelea kutekeleza Malengo ya Milenia.  Bahati mbaya sana mataifa tajiri hayajafikia viwango wanavyotarajiwa kutoa na hata vile wanavyoahidi wenyewe kutoa katika majukwaa mbalimbali.  Kama wangetimiza ahadi zao, sura ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia ingekuwa tofauti kabisa. 
Ndugu Wananchi;
Hiyo ndiyo hali ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia hapa nchini. Hakuna nchi ye yote duniani iliyofanikiwa kutekeleza shabaha za malengo yote kwa ukamilifu.  Ushauri wa viongozi wote waliozungumza ulitaka mataifa yaliyoendelea yatimize ahadi zao za kuchangia utekelezaji wa Malengo ya Milenia.  Ilionekana suala la upatikanaji wa fedha halina budi kuangaliwa kwa makini sasa na baada ya mwaka 2015.  Bila ya hivyo ufanisi utakuwa mdogo katika kuongeza kasi ya utekelezaji kwa pale paliposalia kufikia malengo ya 2015 na hata kwa Malengo ya baada ya mwaka 2015. 
Mashambulizi ya Kigaidi ya Westgate, Nairobi
Ndugu Wananchi;    
Wakati nikiwa safarini, tarehe 21 Septemba, 2013  kulitokea shambulilizi la kigaidi katika Jengo la Biashara la Westgate, huko Nairobi, Kenya.  Watu 67 walipoteza maisha na zaidi ya 200 walijeruhiwa.  Nilituma salamu za pole na rambirambi kwa Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wa Kenya na kuwahakikishia kuwa tupo pamoja nao katika wakati huu wa majonzi.
Nafahamu kuwa baada ya tukio hilo watu wengi hapa nchini wameingiwa na hofu kuhusu usalama wetu.  Ni hofu ya msingi kwani tarehe 8 Agosti, 1998 Ubalozi wa Marekani hapa nchini ulishambuliwa na magaidi na ndugu zetu 11 wasio na hatia walipoteza maisha. 
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwafahamisha kuwa tangu shambulio la mwaka 1998, Serikali imekuwa inajenga uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kupambana na ugaidi katika nyanja mbalimbali.  Tunaendelea kujiimarisha bila kusita siku hadi siku.  JWTZ, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa ajili hiyo.  Juhudi zetu hizo ndizo zinazotufanya tuwe salama hadi sasa.
Baada ya tukio la Kenya, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeimarisha mikakati yao maradufu.  Pamoja na kujizatiti kwetu huko hatuwezi kusema kuwa tukio la kigaidi halitaweza kutokea nchini.  Uhakika huo hatuna kwani hata mataifa makubwa na tajiri yameshambuliwa.  Kilicho muhimu ni kuendelea kuchukua tahadhari na wananchi kusaidia ili  vyombo vyetu vifanikiwe zaidi.    
Hali kadhalika, tumewataka watu wote wenye shughuli zinazokusanya watu wengi kama vile maduka, maofisi, mahoteli, migahawa n.k. waweke kamera za ulinzi nje na ndani ya maeneo yao.  Pia waangalie uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi (metal detectors and x-rays).  Najua watu wanaweza kulalamikia usumbufu au gharama, lakini gharama na hasara ya kushambuliwa ni kubwa zaidi kuliko ya usumbufu huo.
Ndugu Wananchi;
Nawaomba muendelee kufanya shughuli zenu bila ya hofu ingawaje msiache kuwa makini na kuchukua tahadhari.  Watu watoe taarifa kwa vyombo vya usalama wanapoona mtu au watu au kitu cha kutilia shaka.  Ni muhimu kwa usalama wake, wa kila mtu, jamii na taifa.  Maafisa husika wa vyombo vya ulinzi na usalama wataendelea kuelimisha umma kuhusu hatua mbalimbali za tahadhari za kuchukua.  Sisi Serikalini tumejipanga kuchukua hatua zaidi kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu na watu wake.  
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
          Kama mtakavyokumbuka, Bunge lilitunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Novemba, 2011.  Sheria hii imeweka mchakato mzima wa kupata Katiba hiyo na kuunda taasisi zake.  Mwezi Mei, 2012, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa na imekamilisha hatua tatu muhimu katika mchakato huo.  Hatua hizo ni kupokea maoni ya wananchi, kutayarisha rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya na kupokea maoni ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na ya taasisi.  Hivi sasa Tume inaandaa mapendekezo ya Rasimu ya Pili ya Katiba itakayopelekwa kwenye Bunge Maalum.  Baada ya tafakuri zake, Bunge Maalum litatoa rasimu ya mwisho ya Katiba ambayo itapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kupitia kura ya maoni.  Baada ya hatua hiyo, ndipo tutakapokuwa tumepata Katiba Mpya.
Ndugu Wananchi;
Baada ya Bunge la Novemba, 2011 kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kulikuwepo na madai ya kutaka sheria hiyo iboreshwe kutoka vyama vyote vya siasa vikiwemo vyama vya upinzani na Chama tawala.  Majadiliano yalifanyika baina ya Serikali na vyama hivyo pamoja na shirikisho la asasi za kiraia.  Makubaliano yalifikiwa kuwa marekebisho yafanyike kwa awamu.  Awamu ya kwanza ihusishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba kisha hapo yafanyike marekebisho yanayohusu Bunge Maalum na mwisho Kura ya Maoni.
Kama ilivyokuwa kwa mabadiliko yaliyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba, safari hii nayo vyama vya siasa vilitoa mapendekezo yao.  Yalifanyika mazungumzo kati yao na Serikali na maelewano kufikiwa kuhusu maeneo ya kufanyiwa marekebisho. Serikali ilitayarisha rasimu ya Muswada na kuuwasilisha kwa wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ndugu Wananchi;
 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa mapendekezo yake na ushauri kwenye maeneo mawili. Kwanza kwamba uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum ufanywe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kuafikiana na Rais wa Zanzibar.  Pili walishauri kwamba kama Bunge Maalum litashindwa kufikia maamuzi ndani ya siku 70 zilizopendekezwa, liweze kuongezwa muda hadi kufikia siku 90.  Maeneo mengine ya Muswada waliafikiana nayo.
Ndugu Wananchi;
          Kwa kuzingatia utaratibu wa kutunga Sheria, Serikali ilifikisha Muswada kwa Spika wa Bunge ambaye nae aliuwasilisha kwenye Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala.  Kama ilivyo ada, Kamati hiyo ilifanya vikao na wadau na kupokea maoni yao kuhusu Muswada.  Nimeambiwa kulikuwa na mjadala wa kina na mapendekezo mazuri yalitolewa na wadau.  Kisha hapo Wajumbe wa Kamati walikaa wenyewe kujadili Muswada walikuwepo pia Wabunge ambao si Wajumbe wa Kamati walioshiriki kwa vile Kanuni zinaruhusu.  Nimeambiwa pia kwamba mjadala ulikuwa mpana na wa kina zaidi.  Mapendekezo kadhaa yalitolewa na Wajumbe kuhusu vifungu mbalimbali vya Muswada.
Ndugu Wananchi; 
Nimefahamishwa kuwa Wabunge wa vyama vyote walichangia na kwamba baadhi ya nyakati mambo yalipokuwa ugumu mawazo mazuri ya baadhi ya Wabunge wa upinzani yalisaidia kupata ufumbuzi.  Nimeambiwa pia kwamba Wajumbe wa Kamati na upande wa Serikali walikubaliana kwa maeneo mengi isipokuwa machache ambayo walikubaliana kwa pamoja wayapeleke Bungeni ili Wabunge nao wayajadili na kuyapatia ufumbuzi. 
Ndugu Wananchi;
          Baada ya Kamati kumaliza kazi yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mathias Chikawe aliwasilisha Muswada Bungeni.  Akafuatiwa na Mheshimiwa Gosbert Blandes kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kutoa maoni ya Kamati. Baadaye Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Tundu Lissu  alitoa maoni yake. 
Ndugu Zangu;
Baada ya watu hao watatu kutoa maoni yao ilitarajiwa kuwa Wabunge wangeanza kujadili Muswada.  Naambiwa mambo hayakuwa hivyo.  Badala yake kukazuka malumbano baina ya Spika na baadhi ya Wabunge wa Upinzani wakitaka Muswada usijadiliwe.  Ilifikia wakati hoja hiyo ikabidi iamuliwe kwa kura ambapo ilishindwa.  Katika hali isiyotarajiwa, Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje ya Bunge isipokuwa wawili.  Kitendo hicho kimewanyima Wabunge wengi wa upinzani fursa ya kutetea hoja zao walizozitoa kupitia hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani.  Pia wamejinyima nafasi ya kusema mambo mengine wakati wa mjadala na Kamati ya Bunge zima.
Wabunge waliokuwepo waliendelea kuujadili Muswada na kutoa hoja na mapendekezo ya kuuboresha.  Walifanya hivyo wakati wa mjadala na wakati wa kupitia kifungu kwa kifungu.  Baadhi ya hoja na mapendekezo yalikubaliwa na mengine yalikataliwa.  Miongoni mwa yaliyokubaliwa na Wabunge, kwa mfano, ni kuhusu elimu ya mtu atakayekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum na lile la ukomo wa uhai wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
Kwa maoni yangu madai ya Kambi ya Upinzani yanazungumzika na hata baadhi yangeweza kukubalika kama Wabunge wake wangekuwepo Bungeni na kushiriki mchakato wote wa kujadili na kupitisha Miswada Bungeni.  Bahati mbaya hawakuwepo, hivyo hapakuwepo na mtu wa kusema mawazo yao.  Baada ya kupoteza fursa yao halali, kutaka kupata ufumbuzi nje ya Bunge ni jambo lisilowezekana.  Haya ni masuala yanayohusu Bunge ambayo hujadiliwa na kuamuliwa Bungeni na si vinginevyo.  Kuandamana nchi nzima au kuchukua hatua za kutotii sheria kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Freeman Mbowe anavyotaka, hakutaleta mabadiliko wanayoyataka katika sheria hii. Naamini na wao wanautambua ukweli huo. 
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo wa wahenga kuwa “historia hujirudia”.  Naomba hekima ziwaongoze viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na zituongoze sote kutumia utaratibu tulioutumia mwaka 2012.  Kulipotokea mazingira kama haya pande zote zilikaa pamoja na kuzungumzia hoja moja baada ya nyingine na kukubaliana nini kifanyike na kifanyike vipi.  Baada ya kuridhiana hatua zipasazo za kisheria na kanuni zilichukuliwa na kumaliza mzozo.
Ndugu Wananchi;
Kufanya kinyume cha hayo hakutaleta ufumbuzi wa mzozo huu.  Tutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.  Tukikataa kufanya hayo Watanzania wanayo kila sababu ya kuhoji dhamira zetu na kutilia shaka nia zetu.  Watakuwa na haki ya kuuliza nia ni hii yetu sote ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia njia za kikatiba na kisheria au tuna dhamira nyingine iliyojifisha? 
Kama dhamira yetu ni kutaka kupata Katiba mpya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ushauri wangu na rai kwa ndugu zetu wa CHADEMA, CUF na NCCR-Maguezi ni kuwa waachane na mipango ya maandamano na kufanya ghasia.  Badala yake watumie njia halali zinazotambulika kikatiba na kisheria kujenga hoja za kufanya marekebisho wanayoyaona wao yanafaa kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.  Tukifanya hivyo tutakuwa tunajenga badala ya kubomoa.  Tutaliponya taifa.  Sisi katika Serikali tuko tayari.
Ndugu Wananchi;
Napenda pia kuzisemea baadhi ya hoja zilizotolewa na Kambi ya Upinzani.   Kwanza kabisa nasema kuwa nimesikitishwa sana na madai na tuhuma za uongo eti katika uteuzi wa Tume ya Katiba sikuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu.    
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu.  Nasema hivyo kwa sababu, sipendi kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amesema yale kwa kutokufahamu ukweli au kwa bahati mbaya.  Amesema yale kwa makusudi mazima ya kupotosha ukweli ili pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wale Wajumbe 166 wa Bunge Maalum.  
Napenda ieleweke kuwa siishabikii kazi hiyo, lakini kwa kutimiza wajibu na maslahi ya taifa nikiagizwa na Sheria za nchi nitafanya.  Nasema hivyo kwa sababu nafahamu ni kazi ngumu.  Kama kazi ya uteuzi wa Wajumbe 30 wa Tume haikuwa rahisi hata kidogo, hii ya uteuzi wa watu 166 itakuwa ngumu zaidi.  Ile ya Tume ilikuwa ngumu kwa namna mbili.  Kwanza, kwamba taasisi zilizoomba na waombaji walikuwa wengi mno kuliko nafasi za kujaza yaani 15 Zanzibar na 15 Bara.  Zanzibar ziliomba taasisi zaidi ya 60 na waombaji walikuwa zaidi ya 200 wakati Bara kulikuwa na taasisi zaidi ya 170 zikiwa na waombaji zaidi ya 500.  Kupata watu 30 kutoka orodha kubwa kiasi hicho si mtihani mdogo.  Pili kwamba tulitakiwa kuunda Tume inayoasili sura ya taifa, yaani watu wa nchi yetu kwa maeneo, vyama vya siasa, dini, wanawake, vijana, walemavu, wafanyakazi, wasomi, Wabunge, Wawakilishi, wanasheria, wafanyabiashara, wakulima, asasi za kiraia n.k.
Ndugu Wananchi;
Pamoja na changamoto hizo, lakini tulifanikiwa kuunda Tume iliyopokelewa vizuri na jamii na kufanya watu wengi hata wale ambao hawakuteuliwa wahisi kuwakilishwa.  Tulifanyaje? Kwanza kabisa tulihakikisha kuwa tunapata wawakilishi wa vyama vya siasa vyenye wawakilishi Bungeni na kwenye Baraza la Wawakilishi na tunapata wawakilishi wa mashirika ya dini zetu kubwa yaani, TEC, CCT na BAKWATA.    Ndiyo maana nikasema kuwa kwa Mheshimiwa Tundu Lisu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu.
Baada ya hapo ndipo tukaangalia waombaji wa makundi na taasisi nyingine.   Tulijitahidi sana kupata watu ambao wanawakilisha kundi zaidi ya moja.  Tulifikiria hivyo kwa sababu ni ukweli ulio wazi kuwa si kila taasisi iliyoomba itapata mwakilishi kwani hata tungependa iwe hivyo nafasi hazikuwepo.  Kwa kutumia utaratibu huu makundi mengi yamepata uwakilishi kutokana na watu waliopendekezwa na makundi mengi.  Tumefanya kazi kubwa sana ya kuwianisha mambo na makundi ya maslahi mbalimbali nchini. 
          Ndiyo maana naiona mantiki ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Rais wa Zanzibar wa kuwateua Wajumbe wa Bunge Maalum.  Dhana kuwa kila kikundi kiteue chenyewe watu ingefaa sana kama kungekuwepo na nafasi za kutosha kila kundi nchini.  Hilo haliwezekani, labda tuwe na Bunge Maalum lisilokuwa na ukomo wa wajumbe.
Ndugu Wananchi;
Mimi na Rais wa Zanzibar tumekuwa tunajiuliza baada ya kazi ngumu na nzuri tuliyoifanya na iliyopongezwa na wengi ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba nini kilichoharibika sasa hata tuonekane hatuaminiki kuteua hawa 166?  Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu, nimeshasema hazina ukweli wowote.  Ninapojiuliza kwa nini aseme uongo nashindwa kupata jibu linaloingia akilini.  Wakati mwingine nafikiria kuwa ni hiana.  Lakini nadhani ni hila za kisiasa zenye nia ya kutaka kupata watu wa kutetea maslahi ya chama chake.  Kama hiyo ndiyo shabaha basi amekosea sana. 
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Hatutengenezi Katiba ya Chama fulani bali Katiba ya nchi, Katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama ambao ndiyo wengi kuliko wote.  Lazima tuongozwe na ukweli huo na tuwe na msimamo huo wakati wote.  Lazima tukumbuke kuwa si watu wote wanaostahili au kuwa na sifa ambao wataomba na kupata nafasi ya kuwa Wajumbe, hivyo wale wachache watakao bahatika lazima wawasemee wote.  Wanatakiwa kusikiliza na kuwakilisha mawazo ya wote hata wale wasiokuwa wa Chama chao au kundi lao. 
Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri hii ndiyo sifa kubwa iliyooneshwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.  Wamewasimamia na kuwasemea watu wote bila ya kubagua.  Natambua kuwepo kwa baadhi ya watu ambao hawafurahii msimamo huo na matokeo ya kazi yao.  Watu hao kuwalaumu Wajumbe wa Tume kwa ajili hiyo ni kuwaonea na kutowatendea haki.  Tunataka watakaokuwa Wajumbe wa Bunge Maalum nao waige mfano huu mzuri.  Wajali maslahi mapana ya taifa letu na watu wake badala ya kujali yale ya taasisi zao au makundi yao.
Zanzibar Kutokushirikishwa
Ndugu Wanachi;
Nimeambiwa pia kuliwepo madai ya Zanzibar kutokushirikishwa ipasavyo.  Nimeeleza kwa kiasi gani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshirikishwa na kutoa maoni yake yaliyojumuishwa katika Muswada.  Hivyo basi napata tabu kuyaelewa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa msingi wake nini!  Labda kuna kitu sikuambiwa! 
Nimeulizia kuhusu hoja ya Kamati kutokufanya vikao Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau wa Zanzibar.  Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati haistahili kulaumiwa.  Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulauminiana isivyostahili.  Hivyo basi, kuligeuza jambo hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya maandamano sidhani kama ni sawa. 
Ndugu Wananchi;
Nimeambiwa pia kuwa kulikuwa na hoja ya kutaka idadi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar iwe sawa kama ilivyo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba.  Sababu ya idadi ya Wajumbe wa Tume kuwa sawa inatokana na utaratibu wao wa kufikia uamuzi.  Ni kwa maelewano ya wote (consensus) na siyo kwa kupiga kura.  Ndiyo maana idadi imewekwa sawa ili sauti za pande zote zisikike sawia.  Bunge Maalum lina sharti la kufanya uamuzi kwa theluthi mbili ya kura za kila upande kukubali.  Bila ya hivyo hakuna uamuzi.
 Hivyo basi, katika Bunge Maalum nguvu si uwingi wa kura ambazo upande fulani unaweza kupata bali ni ulinganifu sawa wa kura za kila upande peke yake.  Huu ndiyo msingi unaotumika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa kwa lengo la kulinda maslahi ya Zanzibar.  Zanzibar ina Majimbo 50 ya uchaguzi na Tanzania Bara ina Majimbo 189, hivyo ukiamua kwa wingi kila wakati Wazanzibari watashindwa.  Lakini, hapajakuwepo madai ya Zanzibar nao kutaka kuwa na idadi sawa ya majimbo kama Bara au kupunguza majimbo ya Bara yawe sawa na ya Zanzibar kwa sababu wingi si hoja. Msingi unaotumika ni kutoa nguvu sawa za uamuzi kwa kila upande wa Muungano wakati wa kuamua masuala ya Katiba.  Hakuna mdogo wala mkubwa, wote wako sawa.  Hakuna mdogo kumezwa na mkubwa.  Ndiyo msingi unaopendekezwa kutumika kwenye Bunge Maalum hivyo hakuna kitakachoharibika kwa idadi ya Wajumbe kutokukulingana.  Nadhani inafaa ibaki ilivyo.  Lakini kama Wabunge wataamua waongeze idadi itakuwa kwa sababu nyingine siyo hii ya mfano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
          Katika orodha ya madai ya ndugu zetu wa upinzani lipo suala la uhai wa Tume ya Katiba.  Wanataka usiishe wanapokabidhi rasimu ya pili kwa Bunge Maalum bali waendelee kuwepo mpaka mwisho wa mchakato.  Nimeulizia ilikuwaje?  Nimeelezwa kuwa jambo hili halitokani na mapendekezo ya Serikali wala ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.  Limetokana na pendekezo la Mbunge katika Bunge wakati wa kupitia vifungu na kuungwa mkono na Wabunge wengi.  Kwa hiyo kuilaumu Serikali si haki.  Serikali inaweza kuwa mshirika katika hoja hii.
          Nami naiona hoja ya Wajumbe wa Tume kuwa na wajibu wakati wa Bunge Maalum hasa wa kusaidia kufafanua mapendekezo ya Tume.  Je ushiriki huo uwe vipi? Je ni Wajumbe wote au baadhi yao ni jambo linaloweza kujadiliwa.
Ndugu Wananchi;
Naomba nimalizie kwa kuwasihi viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kuongozwa na hekima iliyotumika wakati tulipokuwa na tatizo linalofana na hili kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mimi naamini kama iliwezekana kufanikisha mambo wakati ule inaweza kufanya hivyo hata safari hii. Itatufikisha pale tunapopataka salama salimini bila maandamano, kushupaliana au uvunjifu wa amani.  Kupanga ni kuchagua, naomba sote, mmoja mmoja na kwa umoja wetu tuchague njia ya mazungumzo na maelewano kwani itaihakikishia nchi yetu amani, usalama na utulivu. Tukifanya hivyo historia itatuhukumu kwa wema.
Mungu Ibariki Tanzania.   Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.

Kenya yataja walishambulia Westgate

Washambuliaji ndani ya jumba la Westgate
Kenya imetoa majina ya wanaume wanne ambao inasema ndiyo walifanya shambulio la jengo la maduka la Westgate, mjini Nairobi majuma mawili yaliyopita ambapo watu zaidi ya 60 waliuwawa.
Wanaume hao walionekana kwenye picha za kamera za usalama zilizopatikana Westgate baada ya jumba hilo kuvamiwa kwa siku nne.
Msemaji wa jeshi aliwataja wanaume hao kuwa Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab al-Kene na Umayr.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Taarifa mjini Nairobi zinaonesha kuwa wawili kati yao wana uhusiano na al-Qaeda na mmoja ana uhusiano na kundi la al-Shabaab ambalo lilisema lilishiriki katika shambulio la Westgate.

BBC

Simba yabanwa na Ruvu, Tambwe atupia kama kawa

Betram Mwombeki akijaribu kumtoka beki wa Ruvu Shooting (Picha:Francis Dande)
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba jioni hii imeshindwa kuendeleza ubabe wake baada ya kubanwa mbavu na Ruvu Shooting na kutoka sare ya bao 1-1, huku Amisi Tambwe akiendelea kufunga.
Simba ililazimika kusubiri hadi kipindi cha pili kuchomoa bao kupitia mkwaju wa penati iliyofungwa na Mrundi Amisi Tambwe likiwa bao lake la nane.
Ruvu Shooting walitangulia kupata bao lao dakika ya nane tu tangu kuanza kwa pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao la maafande hao waliokuwa wenyeji wa pambano hilo liliwekwa kimiani na Said Dilunga na kudumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Hata hivyo kipindi cha pili kilipoanza iliwachukua dakika sita tu Simba kulirejesha bao hilo baada ya Betram Mwombeki kuangushwa langoni mwa Ruvu na mwamuzi kuamuru ipigwe penati iliyolalamikiwa na wachezaji wa maafande hao.
Hata hivyo kwa kuwa uamuzi wa refa ni wa mwisho wachezaji wa Ruvu kwa shingo upande walikubali mkwaju huo upigwe na Tambwe kusawazisha.

Golden Bush Fc yapanda daraja

Golden Bush iliyopanda Daraja hadi la Tatu Kinondoni
TIMU ya soka ya Golden Bush Fc iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Nne Wilayani Kinondoni, imefanikuwa kupanda daraja hadi la Tatu.
Golden Bush klabu mpya katika na iliyokuwa ikishiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza imefuzu daraja la tatu kutokana na kufanya vyema katika mechi zake za mzunguko wa pili. 
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa klabu hiyo ni kwamba Chama cha Soka wilayani humo (KIFA) imeitangaza klabu hiyo kupanda daraja.
MICHARAZO inawapa pongezi vijana hao kwa mafanikio hayo na ikiwakumbusha hawapaswi kuvimba kichwa badala yake ijipange kukabiliana na michuano iliyopo mbele yao;
Taarifa hiyo ya uongozi wa Golden Bush unasomeka hapo chini kama ifuatavyo, l 

Wadau,
 
Nimekuwa kimya kwa muda mrefu hii inatokana na majukumu kuingiliana kidogo na kukosa muda wa kuwalisha taarifa mpyampya. Leo napenda niwataarifu kwamba ile timu yetu ya vijana imetangazwa rasmi na KIFA kwamba imepanda daraja la tatu. Hii imetokana na kumaliza mzunguko wa mwisho bila kutoteza mechi hata moja. mimi binafsi nilibahatika kuangalia mechi kama tatu hivi vijana wakifanya mamabo mazito, hakika mpira ni maandalizi na siyo kununua refa. Tumecheza games zote bila kumpa hata shilingi 500 refa nab ado tumefanilkiwa kumaliza ligi katika mzunguko wa pili ambao ni mgumu kabisa bila kufungwa.
 
Binafsi nawapongeza sana vijana kwa kazi kubwa sana lakini pongezi za pekee wanastahili bench la ufundi  chini ya Madaraka Selemani, Katina Shijja na Waziri Mahadhi kwa matokeo mazuri na kupandisha timu daraja ambayo kwa sasa hivi imekuwa gumzo hapa Dar es Salaam. Aidha ningependa kuwopongeza kwana namna ya pekee kabisa wachezaji wa timu yetu ya Veterans kwa msaada mkubwa wa kiushauri kwa mudawao wa kujitolea kutoa mawazo ya kila aina ambayo kwa hakika ndiyo yametufanya tufika hapoa tulipo leo. Nakumbuka hatua ya kwanza kabisa tulifungwa game ya kwanza 1-0, baada ya kupata matokeo yale wazee waliwaita vijana na kuwapa ushauri wa kisaikolojia, kiufundi na kuwaandaa kitalaam kabisa kwa game iliyofuata, nakumbuka tulishinda mecho zote zilizofuata na kuna timu ilikimbia baada ya kuona hadi half time tumewapiga 7-0. Nawashukuru sana watu wazima wakiongozwa na Macocha kwa kazi nzuri nzuri nzuri sana. Ni furaha kubwa nay a pekee unapokuwa na timu inayoandaliwa kucheza mpira siyo kwenda kuloga na kuhonga marefa. Tumefanya kazi yetu na wote kwa pamoja tunastahili sifa na kujipongeza.
 
Golden bush oyeeeeeeeeee!

Kiemba, Niyonzima hapatoshi tuzo za Mwanaspoti Bora 2013


Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda(kushoto)akisaini mkataba wa udhamini wa Tuzo ya Mwanaspoti bora wa soka wa Vodacom 2013,wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa (katikati) na Ofisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo Ibrahim Kaude.

Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa(katikati)akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kutangaza mdhamini mkuu wa Tuzo za Mwanaspoti bora wa soka wa Vodacom 2013,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda na kulia ni Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mkataba na kutangaza udhamini wa kampuni yake kwa Tuzo za Mwanaspoti bora wa soka wa Vodacom 2013.
 =======
KATIKA kuhakikisha zinathamini na kuleta ladha na ubora wa mchango wa wanasoka nchini wadau wa mchezo wa soka; Mdhamini mkuu wa  ligi ya Tanzania bara Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kampuni ya  Mwananchi Communications Limited (MCL)wameungana katika kuwezesha zoezi la utoaji wa Tuzo ya Mchezaji bora wa soka kwa mwaka 2013.

Tuzo hiyo itashuhudia wachezaji walioingia hatua ya Tano bora, AMRI KIEMBA, HARUNA NIYONZIMA, SHOMARI KAPOMBE, THEMI FELIX, na KELVIN YONDANI wakichuana kuwania umwamba wa soka nchini Tanzania, Baada ya kupigiwa kura na mashabiki na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake Zamoyoni Mogela kuchambua majina hayo kulingana na kura walizopata.

Akizungumza katika Mkutano wa kutambulisha tuzo hizo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda, amesema daima Vodacom imekuwa msitari wa mbele katika kuunga mkono michezo nchini, hususani mchezo wa soka na kuhakikisha unakuwa moja ya ajira muhimu kwa watanzania.

"Vodacom tumeendelea kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya soka la Tanzania, sasa soka limekuwa zaidi ya burudani kwa watanzania kutokana na chachu ambayo tumeiweka tangu tuanze kudhamini ligi kuu, ambayo sasa imekuwa na ushindani mkuba na thamani yake inazididi kupanda siku hadi siku" alisema Kamuhanda na kuongeza,

"Mafanikio haya yanayopatikana katika soka letu, yanatokana na nguvu na kujitoa kwa hali na mali, lakini watu wa kwanza ambao wanaleta mafanikio haya ni wachezaji ambao wamekuwa wanapambana kufa na kupona kutoa burudani kwa Watanzania, Ni lazima tuwaenzi wachezaji hawa, Tunapouzungumzia mchezo wa soka tunazungumzia maisha ya watu sasa, Mpira ni maisha ya watu kwani umetoa ajira kubwa kwa jamii ya Watanzania" alisema.

Kamuhanda aliongeza kuwa wameamua kudhamini tuzo hizo ili kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya soka Tanzania na kuleta mapinduzi katika soka la Tanzania kwa kutambua michango wa wachezaji mbalimbali ambao mpira kwao ndo ajira kuu.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa amesema kuwa, waliamua kuanzisha tuzo hizo ili kuendelea kuunga mkono jitihada za wachezaji wa Tanzania na kuleta ushindani na kujenga moyo miongoni mwa wachezaji wa soka nchini.

"Tuzo hizi zinatambulika rasmi kwa jina la zitaitwa MWANASPOTI BORA WA SOKA WA VODACOM 2013. Ni za kipekee na za kwanza kabisa nchini kwa wigo wa wachezaji wanaohusishwa, ushirikishwaji wa uteuzi wa mshindi, na vigezo husika." ALISEMA Mukasa na kuongeza.

"Kwa mwaka huu, licha ya kumpata Mwanaspoti Bora wa soka wa mwaka wa jumla, tuzo hizi zitakuwa na "categories" zaidi ya 10 ikiwemo kocha bora, mwamuzi bora, mchezaji bora wa kike, mchezaji bora chipukizi, "1st eleven", goli bora, mchezaji bora wa kigeni, Mchezi bora wa kulipwa anayecheza nje, na Kipengele kingine kitajulikana siku ya kilele (surprise)." Alisema Mukasa.

Mukasa alihitimisha kwa kusema kuwa ili kuweka usawa miongoni mwa wapenzi wa soka wachezaji hao walioingia katika Tano bora wanaweza kupigiwa kura na Mashabiki kwa  kuandika ujumbe mfupi unaoanza na neno KURA kisha jina la mchezaji anayemchagua kati ya hao waliotajwa na kisha kutuma kwenda namba 15678. Mshindi wa Tuzo hiyo atatangazwa siku ya kilele cha sherehe hizo.
Mwisho 

Botswana yajitosa kusapoti IBF

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAACEaUk%2BaDQAAACq2uhA&midoffset=2_0_0_1_1792922&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
GABORONE,
BOTSWANA's Botswana’s Minister for Environment and Tourism Hon. Tshekedi Khama (seeing photo with the IBF/Africa President Onesmo Ngowi) pledged his government’s support to the success of "IBF Sports Tourism Program" for African countries.


Hon. Tshekedi Khama assured the IBF/Africa President, Onesmo Ngowi of his government's support towards the development of "Sports Tourism" to Africa as one of sustainable by-products of tourism sector.

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAACEaUk%2BaDQAAACq2uhA&midoffset=2_0_0_1_1792922&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
Ngowi and Khana

The IBF/Africa President paid a courtesy visit to the Minister for Environment and Tourism Hon. Tsekedi Khama in the minister’s office as part of his marketing drive for the “IBF International Jr. Featherweight Title” which Botswana’s pro-boxer Lesley Sekotswe will meet a boxer from Britain to be announced soon.


This epic event will be televised live by Super Sports 9 and streamlined by VoxAfrica by to over 100 million homes in Europe, Asia, Africa and the USA.


The event will present great opportunity to Botswana to showcase its tourism attractions to millions of inbound tourists. Such a befitting event will also attract direct investments which Botswana needs for its economic diversification from its mineral based economy.


Over the decades, tourism has experienced continued growth and deepening diversification to become one of the fastest growing economic sectors in the world. Today, the business volume of tourism equals or even surpasses that of oil exports, food products or automobiles.


Tourism has become one of the major players in international commerce, and represents at the same time one of the main income sources for many developing countries. This growth goes hand in hand with an increasing diversification and competition among destinations.


"Sports Tourism" globally provides a forum where stakeholders leans how to properly utilize it to effect profound positive change for destination positioning.


Through the much needed awareness and interactions provided over by the "Sports Tourism", stakeholders  are able to learn new trends in the industry, provide much needed information on their respective destinations and also the various tourism by-products in place which are effective promotional tools within the various destinations.


According to the UNWTO, tourism sector generates over US$ 4.5 trillion per annual and out of this figure "Sports Tourism" generated over US$ 100 billion.


BOTSWANA has made gigantic strides to pro-boxing as a result of the President of IBF/AFRICA Onesmo Ngowi's historic visit, in April 1-6 2013 this year. The visit excited a lot of boxing stakeholders in this country. Also, the visit has also helped to encourage the number of experienced amateur boxers to join professional boxing ranks hence the October 5, tournament.


Upon arrival in Botswana in October 02, the IBF/Africa President met several high ranking government officials as well as corporate leaders to encourage them to support the "IBF Sports Tourism" initiative to Africa of which Botswana is one of the six pilot countries. Other countries are Namibia, Tanzania, Ghana, UAE, South Africa and Tunisia respectively.

 
Botswana is endowed with great wealth in terms of mineral resources (diamond, gold and uranium) and exports of meat to Europe, Asia and USA. It has great amateur boxing foundation as most of her boxers perform well in various international meets hence the great potential fueling pro-boxing.
  

Under its pet project of "IBF Sports Tourism", the IBF/AFRICA has projected Botswana as the strong foundation for future boxing tournaments given its strong amateur boxing foundation, vibrant economy and good governance.


"These are the three pillars and ingredients of boxing development so we can see positive signs ahead” echoed the IBF/AFRICA President, Onesmo Ngowi who was a professional boxer on how he sees Botswana's direction in pro-boxing.


Ngowi illustrated that Botswana’s "economy and good governance" are key towards sustainable boxing development. "You need to build up a strong foundation for "Sports Tourism" and many developing countries fail to succeed due to their poor economies and governance. When you have GDP Per Capita Income in the region of  US$ 3000 then you can afford to pay $ 200 - $ 500 to see boxing events". he emphasized.


Also, the IBF/AFRICA's President alluded that lack of "TV and Corporate Sponsorship" may be another contributing factor for poor showing of Africa in the boxing industry. "Our TV Networks want promoters to pay them when showing their boxing tournaments instead of them TV paying for the boxing broadcasting" continued Ngowi.


The Botswana's October 5, 2013 tournament is coming at a time when the world’s diamond merchants De Beers are moving its international auction headquarter from London to Gaborone Botswana. The move herald Botswana’s robust economic development and the country’s keen interests to diversify its economy hence  development of tourism sector.

Given these rather positive trends, Sports Tourism as one of by-products of tourism is coming at the right moment.

Ajali tena! Basi la Machinga uso kwa uso na Lori, dereva afa papohapo

Baadhi ya mashuhuda wakilishangaa basi la Machinga lililopata ajali

AJALI za barabarani zimeendelea kupoteza uhai wa watumiaji wake baada ya basi la Machinga kupata ajali mbaya ya kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha kifo cha dereva wake.
Taarifa zinasema kuwa dereva aliyepoteza maisha yake anafahamika kwa jina la Noor, na ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kilimahewa mbele kidogo ya Kimanzichana.
Basi hilo lilikuwa likitokea Dar kuelekea Mtwara na ndipo likagongana uso kwa uso na lori la mizigo na kusababisha kifo hicho na abiria wengine kadhaa kujeruhiwa.
Taarifa zaidi juu ya ajali hiyo itawajia kadri tukibahatika kuzipata kupitia hapa hapa www.micharazomitupu.blogspot.com

Friday, October 4, 2013

Masheikh wauwawa Mombasa, kanisa lachomwa moto katika ulipizaji kisasi

Sheikh Abuu Rogo enzi za uhai wake, huyu aliuwawa mwaka jana

POLISI Kenya imetangaza kuwa, watu wanne akiwemo Sheikh Ibrahim Ismail Rogo wameuawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana ndani ya gari dogo jana usiku huko mjini Mombasa.

Taarifa ya Polisi Kenya imeeleza,  Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa mrithi wa Sheikh Aboud Rogo ambaye  naye aliuawa na familia yake kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwezi Agosti 2012.

Mauaji ya Sheikh Ibrahim Rogo ambayo yameutikisa mji wa Mombasa, yametokea  baada ya kupita takriban wiki mbili tokea kundi la al Shabab lilipovamia  na kuua  watu wasiopungua 63 na kujeruhi mamia ya wengine kwenye jengo la maduka ya biashara la Westgate jijini Nairobi.

Baadhi ya wananchi wa Mombasa wanakituhumu kikosi  maalumu cha kupambana na ugaidi kuwa ndicho kilichotekeleza  mauaji hayo.

Sheikh Ibrahim Rogo ambaye alikuwa akitoa mihadhara kwenye Msikiti wa Musa mjini Mombasa alituhumiwa na jeshi la polisi kuwa anawachochea vijana wa Kiislamu kujitumbukiza kwenye makundi  ya kigaidi.

Polisi Kenya imesema kuwa, Gaddafi Mohammad, Issa Abdallah  na Omar Abu Rumeisa ni miongoni mwa waliouawa, naye Salim Aboud alinusurika kwenye shambulio hilo.

=========

Protestors on Friday engaged armed police in running battles in Mombasa following killing of a Muslim cleric, and three others.

The rioting youths in Majengo area set a church on fire.

Earlier in the morning, hundreds of armed police were deployed across islamist strongholds in Majengo and Kisauni  as authorities anticipated riots from slain Sheikh Ibrahim Rogo’s militant supporters.

Tension which has been building up since Thursday’s blood end of Sheikh Rogo and his three friends was expected to reach boiling point at the afternoon Friday prayers in areas like Majengo especially at Musa Mosque where the slain preacher delivered controversial ceremonies.

Reports show that Sheikh Ibrahim delivered a lecture at the mosque at about 8.00pm on Thursday before  embarking on his last journey to meet his end in a drive by shooting near the Butterfly Pavillion afew minutes before 10.00pm long the Mombasa-Malindi road.

Unconfirmed reports indicate  the four were buried in the early hours of Friday at the same cemetery where slain radical islamist Sheikh Aboud Rogo Mohamed was buried on August 27 last year.

It is not clear whether the two Rogos are related.

Reports indicate the four victims were buried in a single grave at the Tudor Muslim Cemetery and accorded the rites of martyrs.

Supporters have identified the other victims as Abu Rumaysa Omar and others identified only as Issa and Shebe Gaddafi.

Salim Aboud who was with them escaped unscathed but with brief facial injuries after playing dead among the slumped corpses inside a bullet ridden car.

Militant islamist Sheikh Abubakar Shariff alias Makaburi who was among the first people to reach the scene of crime declared Thursady’s events as “an assassination” claiming state agents slew the four muslims “in retaliation” for the terrorist carnage at the Westgate Mall in Nairobi last month.

Makaburi who is facing terrorist charges and was  an ally of slain islamist Sheikh Aboud Rogo Mohamed claimed Sheikh Ibrahim Rogo was the target of Thursday’s shooting because of his past links to the former Rogo who was killed on August 27 last year.

And Makaburi denounced the Kenya government and  muslims collaborating with it following the Westgate massacre and in light of Thursday’s events.

He further warned that muslims are now justified to disobey Kenyan laws “because we cannot sit back and be slaughtered or see our sheikhs killed everyday.”

As they descended on the scene where the four were killed militant supporters of the slain preacher swore to avenge the killing.

According to Kisauni OCPD Julius Wanjohi who covers Bamburi where the killings took place, the four were killed when a “vehicle with unknown occupants sped past the car which was carrying Sheikh Ibrahim and four others and slowed a few metres from the vehicle.”

The OCPD says the occupants of the unknown car opened fire on the right side of the approaching car carrying Sheikh Ibrahim.

Wanjohi further says Sheikh Ibrahim and three others were killed “on the spot and the vehicle sped away” apparently towards Bamburi.

According to the OCPD Sheikh Ibrahim̢۪s car was heading towards Mtwapa where he is believed to live.
Source: Standard

Kaburi ya anayedaiwa kufufua lafukuliwa kuchunguza viungo vilivyokuwepo ndani yake

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kaburi ambalo alizikwa mtoto Shabani Maulidi (15), ambaye anadaiwa kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai hivi karibuni, jana lilifukuliwa na viungo vya mwili wake kukutwa ndani.
Kazi hiyo iliyofanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Lucas Ndungulu, ilizua taharuki kwa umati wa watu waliokuwa eneo hilo, baada ya nyumba ya jirani lilipo kaburi hilo, Masanja Marwa, kubomoka ghafla wakati ufukuaji huo ukiendelea, huku mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja naye akianguka na kuzirai.
Kwa sasa mtoto huyo ambaye alionekana hai, amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uangalizi wa kitaalamu.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Ndungulu alisema kuwa wameamua kufukua kaburi hilo ili kupata sehemu ya viungo vya mwili kwa ajili ya vipimo.
“Lengo la kufukua kaburi hili ni kutaka tupate kiungo chochote cha mwili wa marehemu ili tufanye utafiti wa kitaalamu ili tujue kama ni kweli huyu anayedaiwa kuwa ni mtoto wao ndiye,” alisema.
Alisema kuwa ufukuaji huo umemalizika na kwamba wamepata baadhi ya viungo vya mwili wa marehemu na kuchukua baadhi ya mifupa ya mapaja yote mawili ambayo itapelekwa katika hospitali ya rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa Ndugulu, majibu ya vipimo hivyo yatatolewa baada ya wiki mbili kama hakutakuwa na tatizo lolote la kukatika kwa umeme.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Adamu Sijaona, alisema kuwa pamoja na kuchukua viungo hivyo, pia watachukua damu ya wazazi na mtoto mwenyewe.
“Tumechukua pia damu ya mama na baba wa Maulidi mwenyewe ili tukapime vinasaba (DNA) na kama alivyosema mtafiti, majibu yatatoka baada ya wiki mbili,” alisema.
Akizungumza baada ya kazi ya ufukuaji kumalizika, baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi Shabani, alisema kuwa endapo majibu yatakuja tofauti au vile wanavyokusudia, wapo tayari kuyapokea na kwamba ikigundulika huyo aliyeonekana ni Maulidi, pia watampokea na kuendelea kumtunza.
“Lakini nina imani kuwa huyu aliyeonekana ni mwanangu Maulidi kabisa, kwa sababu anazo alama zote,” alisema mzazi huyo.
Mtoto Maulidi aliyefariki dunia miaka mitatu iliyopita na kufanyiwa matanga, alionekana akiwa hai baada ya kukutana na mama yake ana kwa ana mapema wiki hii asubuhi wakati akienda kwenye shughuli zake za biashara.
Ilidaiwa na wazazi wake kuwa Maulidi alitoweka ghafla na kushindwa kurudi nyumbani kwao Januari mosi 2011, wakati alipokuwa amewapeleka mbuzi malishoni na mwili wake kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa mujibu wa baba yake, Maulidi hakurudi nyumbani siku hiyo, ambapo waliendelea kumtafuta bila mafanikio na ndipo baada ya siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji kilicho maeneo ya Kijiji cha Nyankumbu, Kitongoji cha Mwembeni.
Tukio hili ni la tatu kutokea mkoani hapa ambapo wilayani Kasamwa, mwanamke aliyefariki dunia miaka mitano iliyopita alionekana hai na kutambuliwa na ndugu yake. Tukio la pili lilitokea Wilaya ya Chato, wakati kijana aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita alionekana akiwa hai.
Tanzania Daima

Kuziona Simba na Ruvu Buku 5 tu, Mohammed Theofil kuzihukumu Taifa

Ruvu Shooting wakataokuwa wenyeji wa Simba
Vinara wa Ligi Kuu, Simba watakaovaana na Ruvu Shooting kesho jijini Dar
Na Boniface Wambura
KITIMTIM cha michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kinatarajiwa kuingia raundi ya saba kesho (Oktoba 5 mwaka huu)  kwa mechi nne ambapo Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa vinara Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mohamed Theofil kutoka Morogoro kuanzia saa 10 kamili jioni vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.

Mechi nyingine za kesho ni JKT Ruvu itakayoumana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam huku Coastal Union ikiwa mwenyeji wa Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha ndiyo utakaotoa fursa kwa timu za Oljoro JKT na Mbeya City kuoneshana ujuzi katika kusaka pointi tatu.

Ligi hiyo itaendelea Jumapili (Oktoba 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Mgambo Shooting itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Maamuzi ya Kamati y Maadili TFF kufanyiwa mapitio upya, kisa...!

MCHAKATO wa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaelekeo ukingoni ambapo Maamuzi ya Kamati ya Maadili yanatarajiwa kupitiwa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Okt 26/27 jijini Dar es Salaam.

Hivi sasa, wagombea wanasubiri vyombo vya juu vya uamuzi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa mwisho kabla ya kuanza kampeni na hatimaye uchaguzi.

Hata hivyo, baada ya Kamati ya Maadili kufanya uamuzi dhidi ya kesi nane zilizowasilishwa mbele yake, Sekretarieti imeona kuwepo kwa ukakasi katika utekelezaji wa uamuzi huo kutokana na ukweli kuwa kuna baadhi ya mambo yanaonekana kuwa na ugumu katika kuyatekeleza.

Sekretarieti si chombo chenya mamlaka ya kutafsiri uamuzi wa vyombo huru vya Shirikisho, kazi yake kubwa ni kupokea uamuzi na kuutekeleza, hivyo kwa kuwa kuna ukakasi huo imeamua kuwasilisha uamuzi huo kwenye Kamati ya Rufani ya Maadili kwa ajili ya kuufanyia mapitio (revision) na pia kutoa mwongozo kabla ya kurejesha uamuzi huo kwenye Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya kuendelea na mchakato.

Sekretarieti imefanya hivyo kwa lengo la kusaidia wagombea ambao wengi wanaonekana kuwa njia panda baada ya kupokea uamuzi wa Kamati ya Maadili na kuiuliza Sekretarieti kuwa inakuwaje Kamati ya Maadili iwaone hawana hatia, lakini hapo hapo ikubaliane na uamuzi wa kuwaengua, jambo ambalo kwa kweli limetufanya tukose majibu sahihi na hivyo kuamua kuomba revision na mwongozo.

Pia mwongozo utakaotolewa na Kamati ya Rufani ya Maadili utasaidia kuweka mwelekeo mzuri wa masuala ya Maadili katika siku zijazo.

Miongoni mwa mambo yanayoonekana kuwa na ukakasi ni kuwaona watu wote ambao kesi zao ziliwasilishwa kwenye Kamati ya Maadili hawana hatia, lakini hapo hapo kukubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi wa kuwaengua baadhi yao kwa sababu za kinidhamu ikisema haiwezi kuwahukumu mara mbili kwa kuwa wameshaadhibiwa kwa kuenguliwa kwenye uchaguzi.

Ili haki itendeke na ionekane inatendeka, Sekretarieti imeona ni vizuri masuala hayo yakafanyiwa revision (mapitio) na kutolewa mwongozo ili kuondoa ukakasi uliojitokeza miongoni mwa wagombea, Shirikisho na wadau na hivyo kujenga hisia kuwa kuna mbinu zimefanyika dhidi ya baadhi ya wagombea.

Uamuzi huu haumaaniishi kuwa Sekretarieti inapingana na uamuzi wa Kamati ya Maadili, bali ni utaratibu wa Sekretarieti kuomba ufafanuzi au mwongozo kutoka vyombo husika pindi inapotokea ukakasi katika utekelezaji wa uamuzi wa vyombo vya uamuzi vya Shirikisho.

Sekretarieti imeshamwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Maadili ili aitishe kikao kwa manajiri ya kufanya mapitio na kutoa mwongozo ambao utasaidia Shirikisho kuendelea na uchaguzi bila ya ukakasi.

TFF yaipigia goti serikali, taasisi kuisaidia U20 WanawakeSerikali, T

Lina Kessy
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiomba Serikali, taasisi na kampuni mbalimbali kuisaidia timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inayojiwinda kwa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Msumbiji.

Timu hiyo hivi sasa iko kambini Mlandizi mkoani Pwani chini ya Kocha Rogasian Kaijage kujiandaa kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itakayochezwa Oktoba 26 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya TFF, Lina Kessy amesema hiki ndio kipindi muafaka cha kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Ameitaka jamii kujitokeza kuisaidia timu hiyo ambayo haina mdhamini wala mfadhili, kwani timu za Taifa ni za Watanzania badala ya kusubiri ifanye vibaya na kusema ni kichwa cha mwendawazimu.

Kessy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA), ameishukuru kambi ya JKT Ruvu kwa kutoa fursa ya kambi kwani timu hiyo hailipii malazi badala yake inalipia huduma nyingine inazopata hapo.

Vilevile amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakijitolea kutokana na ukweli kuwa tangu kuanza mashindano ya mpira wa miguu wa wanawake kumekuwepo uungwaji mkono mkubwa.

“Shukrani za kipekee kwa wazazi kukubali watoto wao wachezee timu ya Taifa, kwani wengi bado wanasoma na wapo chini ya uangalizi wa wazazi. Pia tunawaomba wazazi wajitokeze mazoezini ili kuwajenga kisaikolojia wachezaji wetu,” amesema.

Fainali za Dunia za U 20 kwa wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada. Iwapo Tanzania itaitoa Msumbiji katika raundi hiyo, raundi inayofuata itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe.

TFF, Polisi wapiga mkwara 'wakora' viwanjani

http://reluctantgourmet.com/media/k2/items/cache/2e2c1711fe12b24ae23d95c35bfd21c2_XL.jpg
Kisu, moja silaha hatari inayowezwa kutumiwa vibaya na mashabiki uwanjani kuleta maafa
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Jeshi la Polisi kuanzia sasa halitashikilia silaha za washabiki, na badala yake litawazuia kabisa kuingia viwanjani wakati wa mechi.

Jeshi la Polisi limekuwa likihifadhi silaha za washabiki wanaokwenda viwanjani, na baadaye kuwarejeshea baada ya mechi kumalizika kwa vile Kanuni za Usalama Viwanjani za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zinakataza silaha viwanjani.

Wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jeshi la Polisi lilikamata bastola 17 katika upekuzi wa washabiki waliokwenda kushuhudia mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting na ile kati ya JKT Ruvu na Simba. Wote waliokutwa na silaha hizo walikuwa na leseni za kuzimiliki.

Hivyo, kwa washabiki wanaomiliki silaha hatawaruhusiwa kabisa kuingia viwanjani, na badala yake tunawashauri kuzihifadhi huko wanakotoka kabla ya kufika viwanjani.

Pia tunatoa mwito kwa shabiki ambaye atamuona mwenzake akiwa na silaha uwanja kutoa taarifa kwa mamlaka husika likiwemo Jeshi la Polisi ili aweze kuchukuliwa hatua.

Viwanja 10 kutimka vumbi FDL wikiendi hii

Polisi  Moro, moja ya timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza
Na Boniface Wambura
KIVUMBI cha Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2014/2015) inaendelea wikiendi hii (Jumamosi na Jumapili) kwa kuzikutanisha timu 20 zitakazopambana katika viwanja kumi tofauti.

Jumamosi kutakuwa na mechi kati ya Green Warriors na Friends Rangers (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi), Kimondo na Burkina Faso (Uwanja wa CCM Vwawa, Mbozi), Mlale JKT na Mkamba Rangers (Uwanja wa Majimaji, Songea) na Kurugenzi dhidi ya Polisi Morogoro (Uwanja wa Wambi, Mafinga).

Polisi Dodoma na Stand United (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Toto Africans na JKT Kanembwa (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mwadui na Polisi Mara (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Polisi Tabora na Pamba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Keshokutwa (Jumapili) kutakuwa na mechi kati ya African Lyon na Transit Camp (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi) na Villa Squad dhidi ya Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam).

Uhuru Seleman awataka 'Wagosi wa Kaya' kuwaiga wenzao wa Mbeya

Uhuru Seleman akiwa na taji la ubingwa la Ligi Kuu alipokuwa Simba
KIUNGO wa Coastal Union, Uhuru Seleman amesema amekunwa na mashabiki wa soka wa mkoa wa Mbeya kwa namna wanavyoisapoti timu yao ya Mbeya City kiasi cha kuzisahau Simba na Yanga na kuwataka mashabiki wa Coastal Union na Tanga kwa ujumla kuiga mfano huo.
Uhuru ambaye ni mwenyeji wa Mbeya, alisema wiki iliyopita Coastal ilipoenda kuumana na Mbeya City alishangazwa na namna wakazi wa mkoa huo walivyoungana pamoja na kuishangilia timu yao mwanzo mwisho kitu alichodai hajawahi kukiona Tanga na kuwataka 'Wagosi wa Kaya' kuzinduka.
Kiungo aliyewahi kuzichezea Mtibwa Sugar, Simba na Azam, alisema kwa namna mashabiki wa mkoa Mbeya wanavyoungana na kuzisahau kabisa Simba na Yanga inawatia moyo na kuwapa nguvu wachezaji wa timu hiyo kujituma uwanjani.
"Huwezi amini ukiwa Mbeya husikii habari za Simba na Yanga wao na Mbeya City na Prisons, kitu ambacho nilikuwa napenda kuwaomba mashabiki wa soka wa mkoa wa Tanga kuiga jambo hilo na kuwa na uzalendo kwa timu zao na hasa Coastal Union iliyopo Ligi Kuu," alisema.
Alisema sapoti wanayopewa wachezaji wa Mbeya City inawatia moyo na kupata nguvu ya kuipigania timu yao kuweza kuwa na matokeo mazuri licha ya ugeni wake katika ligi hiyo inayozidi kushika kasi.
"Uzalendo wa namna hiyo wa kuziunga mkono timu za nyumbani husaidia kuwatia nguvu wachezaji badala ya utamaduni wa mashabiki kugawanyika kwa unazi wa Simba na Yanga na kuzisahau timu zao ambazo zinawapelekea mechi kubwa na kuziona timu wanazoziota," alisema Uhuru.
Kiungo huyo na wachezaji wenzake watakuwa uwanja wa Mkwakwani Tanga kesho kwa ajili ya kuwakabili Azam katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu hizo zote zinatokea Mbeya walipoumana na wenyeji wao Mbeya City na Prisons na kuambulia sare ya bao 1-1 kila moja.

Julio aitisha Ruvu Shooting, wawili kulikosa pambano kesho Taifa

Julio akitetea na Mombeki na Henry Jospeh akiwa kando yake
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanatarajiwa kushuka kesho dimbani kuvaana na Ruvu Shooting bila ya wachezaji wake, Miraj Adam na Abdallah Seseme ambao ni majeruhi huku wakiwa hana hakika ya kumtumia Issa Rashid 'Baba Ubaya' ambaye hali yake bado haijatengemaa vyema.
Hata hivyo kitu cha kufurahisha ni kwamba nahodha wake msaidizi, Nassoro Masoud 'Chollo' na mkongwe Henry Joseph wenyewe wapo fiti tayari kuwakabili maafande hao wanaonolewa na kocha Charles Boniface Mkwasa.
Akizungumza na MICHARAZO  kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema Simba ipo kamili kuivaa Ruvu licvha ya kuwakosa Abdallah Seseme na Miraji Adam ambao wote wamefungwa plasta gumu (POP) miguuni.
Julio alisema ukiondoa wachezaji hao wengine wanaendelea vyema japo hali ya Baba Ubaya aliyeanza mazoezi na wenzake bado haijatengemaa vizuri na hivyo kutokuwa na hakika ya kumtumia katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa na kudai itakuwa ngumu na yenye ushindani mkubwa.
"Kikosi kipo tayari kwa vita dhidi ya Ruvu Shooting, japo tunasikitika kusema kuwa hatutakuwa na Seseme na Miraj ambao wote wamefungwa POP huku Baba Ubaya akitupa mashaka, japo Henry Joseph na Chollo wamerejea dimbani kuungana na wenzao ambao wana ari ya ushindi," alisema.
Kuhusu mfungaji wao bora, Amisi Tambwe ambaye majuzi alishindwa kuendelea na mazoezi na wenzake kutokana na kusumbuliwa na tumbo, Julio alisema anaendelea vyema na Jumamosi ataendelea kuongoza 'mauaji' kwa Ruvu.
"Aaah alichafukwa na tumbo tu na wala halikuwa tatizo kubwa na panapo majaliwa ataendelea kuongoza mauaji dhidi ya wapinzani wetu katika Ligi Kuu," alisema Julio beki wa zamani wa Plisner, Simba na Taifa Stars.
Mbali na mechi ya Simba na Ruvu, kesho kutakuwa na mechi nyingine nne zitakazozikutanisha timu za JKT Ruvu dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Chamanzi, Coastal Union kuialika Azam jijini Tanga na Oljoro JKT kuikaribisha Mbeya City kabla ya Jumapili Yanga kupepetana na Mtibwa Sugar na Mgambo JKT kuumana na Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga

Gari laacha njia na kuua wawili Mbeya, wengine wanaswa na bangi gramu 900

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbSKddVeeyHTyKf5ybVJhtXhjjGjgBrBwlffjXY7411udEf3xhx7lKaamyX8nf6GDoTTpcl46_dmR43D3Qz68E3q_lkYa3MX0qj0z7BBK8jJTKBwPpBBG6g038Al0GJJShhP09FkJnDXU/s640/Kamanda+wa+Polisi+Mbeya+.JPG

WATEMBEA kwa miguu wawili wamepotea maisha yao baada ya kugongwa na gari lililoacha njia mjini Mbeya huku watu wengine wawili wakinaswa na dawa za kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa gramu 900.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Polisi mjini humo inayosemeka hapo chini ni kwamba watu hao walipatwa na ajali hiyo jana saa 1 usiku. Isome mwenyewe taarifa hiyo.

MNAMO TAREHE 03.10.2013 MAJIRA YA SAA 19:46HRS HUKO KATIKA ENEO LA SIMIKE JKT – ITENDE BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA.  GARI T.170 AUM AINA YA  TOYOTA CRESTA LIKIENDESHWA NA DEREVA MAHUNDI S/O KAPITI, MIAKA 27, KYUSA, MKAZI WA ITIJI LILIACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI  KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI AMBAO NI 1. DEREVA MWENYEWE 2. NEEMA D/O MWINUKA, MIAKA 32, MNDALI, MWALIMU AMBAYE ALIKUWA MTEMBEA KWA MIGUU MKAZI WA NZOVWE PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI AMBAO NI 1.TWINZA S/O MWAKIYOMA, MIAKA 36, KYUSA, MKAZI WA MAJENGO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA 2. STIVIN S/O MWAKALINGA, MIAKA 36, KYUSA, MKAZI WA NZOVWE AMBAYE ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.  MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 


WILAYA YA  MOMBA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 03.10.2013 MAJIRA YA  SAA 11:00HRS  HUKO KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO TUNDUMA  WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. IZDORI S/O PELLA, MIAKA 24, MKINGA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MAPOROMOKO NA 2. AMOS S/O ALISON MELLA, MIAKA 28, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA MIGOMBANI WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 900. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA IZDORI S/O PELLA. WATUHUMIWA NI WAVUTAJI NA WAUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA   KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE.
Signed by:
                           [DIWANI ATHUMANI - ACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Kwa Mombeki Soka kwanza blabla baadaye


MSHAMBULIAJI mrefu wa Simba, Betram Mombeki amesema yeye kazi yake kubwa katika klabu hiyo ni kucheza mpira na siyo kuzungumza na vyombo vya habari.
Alisema iwapo kutakuwa na watu wanaotaka kumpamba au kumponda basi wapime uwezo wake uwanjani wakati anaitumikia Simba.
Akizungumza na gazeti hili katika mazoezi ya Simba, Mombeki aliyesajiliwa akitokea Pamba ya Mwanza, alisema huwa hapendi kuzungumza na vyombo vya habari kwa sababu siyo kazi yake.
"Unajua kazi yangu ni kucheza soka, ndiyo kazi yangu pekee ninayoijua yaani kujipanga vyema kuisaidia timu yangu iwe ni kwa kufunga au kutoa pasi ya mwisho, lakini siyo kuzungumza na wanahabari kila mara," alisema.
Mombeki alisema kama kuna mtu anataka kujua sifa na ubaya wake wampime kwa majukumu yake uwanjani badala ya kuzungumza au kutaka kujisifia yeye mwenyewe.
Mkali huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Simba tangu atue katika klabu hiyo akionyesha makali yake kwenye mechi za kirafiki na hata kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kutoa pasi za mwisho kwa Amisi Tambwe.
Mombeki, alisema kama mchezaji anajua majukumu yake ni kucheza kwa bidii ili mwishowe Simba imalize vyema ligi hiyo.
Mchezaji huyo mpaka sasa ametupia bao moja tu kimiani, huku mchezaji ambaye amekuwa akimpa pasi za mwishjo, Tambwe akiwa na mabao saba akiwa ndiye kinara wa mabao mpaka sasa.