STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 18, 2013

Nsajigwa amfagilia Samatta tuzo za Afrika

Shadrack Nsajigwa
Mbwana Samatta
NAHODHA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa, amewataka Watanzania kumuunga mkono Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta baada ya nyota huyo kuteuliwa miongoni mwa wachezaji 25 wanaocheza soka barani Afrika kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka.
Nsajigwa alisema watanzania wanapaswa kumuombea Mungu Samatta ili kuweza kufanya vyema katika tuzo hizo akidai kuwa mchezaji huyo ni mkubwa kwa sasa na alistahili kufika hapo alipofikia.
Katika ujumbe wake kupirtia mtandao wa Facebook, Nsajigwa alisema hakuna maana yoyote kwa watanzania kumbeza Samatta kama walivyokuwa wakifanya kupitia maoni yao katika mtandao huo kwa madai huko ni kukojikubali vyetu ilihali Samatta amewatoa kimasomaso Watanzania kiasi cha kutakiwa kumfurahia kwa mafanikio yake.
Janani Watanzania wenzangu wapenda mpira, hatuna budi kumpa sapoti na kumuombea mchezaji wetu kuliko kumbeza, tuache mambo ya kishabiki hayatufikishi kokote. Kwa sasa Samatta ni mchezaji mkubwa na anastahili kuwa pale. Ahsanteni," ujumbe wa Nsajigwa uliosomeka hivyo.
Samatta anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo, alitangazwa na Shirikisho la Sokla Afrika (CAF) kuwea miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya wachezaji wa klabu za ndani akiwa ni mmoja wa wachezaji wawili pekee wa kuanda wa Afrika Mashariki kuteuliwa katika tuzo za Afrika zitakazotolewa mwakani,. Mwingine ni Mkenya Victor Wanyama wa Kenya anayewania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika-2013.
Nyota huyo wa zamani wa African Lyon na Simba amekuwa mhimili mkubwa wa timu ya TP Mazembe akitajwa kama kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ya Kongo ambayo ipo katika Fainali za Kombe la Shirikisho, nyuma ya Tresor Mputu.
Orodha kamili ya wanaowania tuzo za Mwanasoka Bora wa klabu za ndani ya Afrika ambapo Samatta yumo ni kama ifuatavyo;
1. Adane Girma - Ethiopia - St George
2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly
3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon - Coton Sport
4. Ali Machani - Tunisia - CAB
5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon - Coton Sport
6. Daine Marcelle-Klate - South Africa - Orlando Pirates
7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia - CSS
8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest Wits
9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS Sfaxien
10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance
11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa - Orlando Pirates
12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP Mazembe
Mbwana Samatta
13. Moez Ben Cherifia - Tunisia - EST
14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly
15. Rainford Kalaba - Zambia - TP Mazembe
16. Senzo Meyiwa - South Africa - Orlando Pirates
17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade Malien
18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves
19. Tresor Mputu - DR Congo - TP Mazembe
20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly
21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST

Mwisho

Taifa Stars sasa kukipiga na Zimbambwe kesho ni baada ya Kenya kuchomoa

Stars ikijifua
TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Zimbabwe mchezo utakaofanyika kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars itaivaa Zimbabwe badala ya Kenya (Harambee Stars) ambayo ilipangwa hapo awali.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema tayari Zimbabwe wamethibitisha kuja kucheza na Taifa Stars na wanatarajiwa kuwasili jijini leo saa tatu asubuhi.
Wambura alisema kikosi cha Zimbabwe kitakuja na jumla ya watu 30 na kuongeza kwamba maandalizi ya mchezo huo unaofanyika kwa mujibu ya Kalenda ya Shirikisho la Soka duniani (Fifa) yako katika hatua za mwisho.
"Sasa Stars itacheza na Zimbabwe na wameshathibitisha kukubali mechi hiyo na watatua nchini Jumatatu (leo)," alisema Wambura.
Alisema mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda huku akimtaja Oden Mbaga wa Tanzania kuwa ndiye mwamuzi wa mezani na mwamuzi mstaafu wa Fifa, Mtanzania Leslie Liunda, atakuwa kamishna wa mchezo huo.
Kiingilio cha chini katika mechi hiyo ni Sh. 5,000 na cha juu ni Sh. 20,000 kwa viti vya VIP A.
Wambura alisema uongozi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) wamesikitika kuikosa mechi dhidi ya Stars ambayo kiufundi timu hizo mbili zilikuwa zimeshajipanga kukutana.
Aliongeza kuwa, baada ya mechi hiyo, kikosi hicho kitaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Chalenji yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12, mwaka huu jijini Nairobi, Kenya.
Katika mashindano hayo ya kila mwaka yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati, timu ya Tanzania Bara imepangwa Kundi B pamoja na Zambia, Burundi na Somalia huku Kundi A likiwa na wenyeji Kenya, Ethiopia, Zanzibar na Sudan Kusini.
Kundi C linaundwa na mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.
Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amelalamikia kitendo cha FKF kuizuia ghafla Harambee Stars kuja nchini kucheza mechi hiyo.
"Mwanzo tulipanga kambi ya Taifa Stars iwekwe Arusha ili wachezaji wazoe mazingira ya huko kwani kwa kiasi kikubwa yanawiana na mazingira ya Kenya ambako michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu itafanyika. Kenya wakakataa kucheza nasi Arusha kwa madai kwamba uwanja ni mbovu," alisema Poulsen.
"Siku tatu kabla ya mechi wanatuambia hawaji kucheza nasi wakati wametuharibia mipango. Inasikitisha sana."

Cameroon yaungana na Nigeria, Ivory Coast kutangulia Brazili WC 2014

Nahodha Et'oo akiwajibika uwanjani katika mechi ya jana ambapo Cameroon ilishinda mabao 4-1

 
Huku wawakilishi watatu wa Afrika kwenye fainali za FIFA za kombe la dunia wakiwa tayari wamefahamika,timu hizo ni NIgeria, Côte d'Ivoire na Cameroon , kuna dalili zote wawakilishi wa Bara hilo wakatoka ukanda wa Magharibi.
Ghana iliyoifumua Misri mabao 6-1 kesho itaavana na wapinzani wao hao wakiwa na dalili zote za kufuzu sawa na ilivyo kwa Burkina Faso watakaocheza na Algeria 3-2.
Sare zozote za ugenini kwa timu hizo za Afrika Magharibi dhidi ya Waarabu zitafanya wawakilishi wa Afrika kwa mwakani nchini Brazili kuwa za ukanda huo kama ilivyokuwa mwaka 2010 katika fainali za WOZA.
Nigeria ilianza kukata tiketi hiyo juzi kwa kuinyuka Ethiopia kwa mabao 2-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi ya kwanza kushinda 2-1.
Mabao ya Victor Moses kwa penati na Victor Obinna yalitodha kuivusha Nigeria katiia fainali hizo, huku kocha wake, Stephen Keshi akiweka rekodi kuwa kocha wa kwanza Muafrika kuzipeleka timu mbili tofauti katika fainali hizo.
Keshi aliipeleka Togo katika fainali za mwaka 2006 nchini Ujerumani na safari hii akiwa na Nigeria, pia mwenyewe akishacheza fainali hizo wakati wa uchezaji wake.
Katika mechi nyingine ya mtoano wa bara la Afrika, Ivory Coast ililazimishwa sare y 1-1 na Segenal, lakini Tembo hao Afrika walifuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mechi ya kwanza wakiwa nyumbani kushinda mabao 3-1.
Segenal walitangulia kupata bao kupitia kwa Moussa Sow kabla ya Ivory kuepuka kipigo cha mara ya kwanza tangu kwa karibu mwaka na nusu sasa kwa kusawazisha kupitia kwa Salomon Kalou.
Jana Simba Wasiofugika, waliungana na Nigeria na Ivory Coast kutinga fainali hizo za Brazil baada ya kuizamisha Tunisia kwa mabao 4-1.
Mabao ya Cameroon yalifungwa na Pierre Webo, Benjamin Moudandjo na kiungo mkongwe Jean Makoun aliyefunga mabao mawili.

Katika pambano la kwanza timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu ya kutofungana.

Golden Bush Veterani yawanyoa wazee wenzao

Kikosi cha Golden Bush Veterani
Benchi la ufundi la timu hiyo
WAKALI wa kandanda kwa timu za maveterani jijini Dar er Salaam, Golden Bush juzi iliwanyoa wazee wenzao wa Kivukon Veterani kwa mabao 3-0 kablka ya jana kupata ushindi mwingine dhidi ya Kijitonyama.
Ushindi wa juzi dhidi ya Kivukoni ulikuwa ni wa kulipa kiasi kwa wakali hao ambao wiki chache za nyuma walifumuliwa na wapinzani wao hao.
Golden Bush ilipata ushindi huo katika uwanja wa Kinesi Ubungo kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Abuu Ntiro, Said Sued 'Panucci' na Mgaza Aguero.
Mlezi wa klabu hiyo yenye maskani yake Sinza, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema ushindi huo mfululizo kwa timu yake umewapa faraja.
Ticotico alisema kwa sasa kikosi chao kinajiandaa kwa ajili ya ziara ya kwenda visiwani Zanzibar kuvaana na wazee wa huko katika mehci ya kuadhimisha siku ya Uhuru, Desemba 9.