STRIKA
USILIKOSE
Monday, November 25, 2013
Shule ya Mwandege Boys yatoa msaada wa vitabu vya Sh Mil 3 Mwandege SM
UONGOZI wa Shule ya Sekondari ya Mwandege Wavulana iliyopo Mkurunga, Pwani imetoa msaada wa vitabu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni Tatu kwa Shule ya Msingi ya Mwandege ili kusaidia na kukuza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Vitabu hivyo vinavyohusisha kamusi na vile vya masomo mbalimbali kwa Shule ya Msingi vilikabidhiwa juzi kwa shule hiyo katika sherehe za mahafali ya tano ya kidato cha nne ya Shule ya Mwandede Wavulana yaliyofanyika jana katika shule yao wilayani humo.
Mkuu wa Shule wa Mwandede Wavulana, Enock Walter, alisema uongozi wa Shule yao chini ya Bodi ya Wakurugenzi wametoa vitabu hivyo kwa lengo la kusaidia kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa shule ya Mwandege ambayo ipo jirani nayo.
Mwl Walter, alisema kwa kuwa wao ni wadau wakubwa wa elimu na wanatambua kufanya vyema kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ni kuzisaidia Shule za Sekondari kupata wanafunzi bora ndiyo maana wamejitolea kutoa zawadi hiyo aliyoamini itasaidia japo ni ndogo.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Mercy Sillah, aliyevikabidhi vitabu hivyo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwandege, Joseph Awino, alisema kilichofanya na uongozi wa Shule ya Mwandege Wavulana ni mfano wa kuigwa na wadau wengine wa elimu nchini.
DC huyo, alisema lau wadau wengine wa elimu wangekuwa wakifanya kama ilivyofanya Shule ya Mwandege Wavulana ni wazi kiwango cha elimu ya Tanzania kingepaa, huku akifichua miongoni mwa shule za msingi wilayani humo zinazofanya vyema ni Mwandege.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwandege, Joseph Awino aliishukuru shule ya Mwandege Wavulana kwa msaada huo na kuahidi kuvitumia kwa lengo la kuongeza kiwango cha elimu na ufaulu kwa wanafunzi wake zaidi na ilivyo sasa.
"Tunashukuru kwa msaada huu na Mungu awazidishie Mwandege Boy's na tunaahidi kutumia vitabu hivyo kama vilivyokusudiwa kwa lengo la kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wetu ambao baadhi wanaweza kusoma hapa, ahsanteni sana," alisema Mwl Awino.
Kili Stars yaagwa, wachezaji waahidi makubwa Chalenji 2013
![]() |
| Wachezaji wa Kilimanjaro stars |
![]() |
| Nahodha mpya wa Kili Stars, Kelvin Yondani 'Vidic' akizungumza huku kocha wake, Kim Poulsen akisikiliza kwa makini |
![]() |
| Hiki ndicho kikosi cha Kili Stars |
Kikosi
cha Kilimanjaro Stars imeagwa leo tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya
kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba
27 mwaka huu.
Hafla
ya kuiaga timu hiyo imefanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli
ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager unaongozwa na Ahmed Idd
Mgoyi. Timu itaondoka saa 10 alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni
makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na
Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu
Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman
Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar
(Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias
Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma
Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa
(Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na
Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu
wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza
fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo
linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha
Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa
Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu
wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro
Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya
kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Sunday, November 24, 2013
Real Madrid yaijibu Barca, Atletico Madrid ikifanya kufuru La Liga
![]() |
| Fabregas akifunga mkwaju wake wa penati jana |
![]() |
| Ronaldo akielekea kufunga bao la kwanza la Real Madrid kabla ya kutolewa kwa maumivu |
![]() |
| Barca wakipongezana |
![]() |
| Villa na Garcia wa Atletico Madrid wakishangilia mabao yao ya jana. Kila mmoja kati ya wawili hao alifunga mabao mawili |
WAKATI Real Madrid ikijibu mapigo kwa mahasimu wao Barcelona waliotangulia kushinda mabao 4-0 kwa kuichakaza Almeria kwa magoli 5-0, Atletico Madrid ilifanya kufuru zaidi kwa kutoa kisago cha mabao 7-0 katika Ligi ya Hispania.
Madrid ilipata ushindi huo ugenini kupitia kwa mabao ya Cristiano Ronaldo aliyefunga bao la mapema la dakika ya tatu tu ya mchezo kabla ya kutolewa uwanjani kwa kuumia.
Mabao mengine yalifungwa na Karim
Benzema dakika ya 61 pasi ya Jese Rodriguez
kabla ya Gareth Bale kufunga bao la tatu dakika ya 71, Isco akaongeza la nne na Alvaro Morata akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 81.
Mapema Barcelona waliifumua timu ya Grenada kwa mabao 4-0 bila ya kuwa na nyota wake, Lionel Messi aliye majeruhi.
Magoli ya penati ya Andres Iniesta na nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc
Fabregas yaliipa uongozi Barcelona kabla ya kuongeza mengine mawili kupitia kwa Alex Sanchez na Pedro kuifanya Barca iendeleze rekodi ya kushinda mechi mfululizo.
Hata hivyo ni Atletico Madrid walifanya kufuru usiku wa manane wa leo baada ya kuifumua Getafe kwa mabao 7-0 na kuzidi kung'ang'ania katika nafasi ya pili ya msimamo wa La Liga ikifikisha pointi 37,
Raul Garcia na David Villa walifunga mara mbili, huku Diego Costa, Adrian na lile la kujifunga la Lopo lilitosha kuifanya Atletico kuifukizia Barca inayoongoza kwa pointi 40, tatu pungufu na ilizonazo klabu hiyo.
Saturday, November 23, 2013
TFF yaunda kamati zake ndogondogo, Zitto Kabwe, Wilfred Kidao waula
RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile
za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais
Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia
Kamati ya Utendaji.
Pia
ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao
ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja
kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni
Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na
Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane
(Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey
Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey
Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga
(Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro,
Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na
Nassoro Idrissa.
Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao
Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus
Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin,
Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana
inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali
Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali
Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa
Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti),
Zena Chande, Amina Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder,
Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum
Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala
(Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor
Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni
Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf
Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela
na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti),
Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na
Imani Madega.
Kiongozi
wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni
Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora,
Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias
Mwanjala.
Dk.
Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred
Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro
Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.
TFF yamrejesha Rage madarakani yamtaka aitishe mkutano wa dharura
![]() |
| Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliyetoa taarifa za Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage aitishe mkutano haraka baada ya awali kupiunduliwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu yake akiwa nje ya nchi |
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu
baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea
kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo
ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi
wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba
inayosema:
“Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba,
kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa
zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF
itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa
Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya
kusikilizwa.
Mahafali ya Tano ya Kidato cha Nne Mwandege Boy's yalivyofana leo Mkuranga
| Wanafunzi waliosalia shuleni wakisimama kumpokea mgeni rasmi |
| Hata wazazi na walezi nao walisimama wima |
| Pre Form One nao walikuwapo katika mahafali hayo |
| Wanafunzi wa kidato wa tatu wakionyesha onyesho la lugha ya Kiswahili kusherehesha mahafali hayo ya leo |
| Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wakiwa wametulia vitini |
| Mwandege Boys kuna vipaji vya uigizaji usipime! |
| Yaani ni Full Kidigitali Mwandege Boys |
| Igizo likiendelea kuhusiana na umuhimu wa kuzingatia masomo shuleni |
| Hata Bongo Movie hawaoni ndani kwa madogo hawa, vipaji vitupu |
| Wahitimu wa kidato cha Nne Jesse na Godwin wakisoma taarifa ya habari hawa jamaa nouma |
| Hashim Abdallah (kulia) akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne |
| Wanafunzi wa kidato cha nne wakitumbuiza |
| Leo tunawaaga kwaherini tuliwazoea kaka zetu, ndivyo wanavyoimbiwa wahitimu waliokaa na wanafunzi wenzao wa kidato cha tatu |
| Yaani ni full burudani |
| Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Mercy Silla (wa pili kulia) akiwasili eneo la tukio akisindikizwa na Mkuu wa Shule, Mwl Enock Walter (kulia) |
| Meza kuu ikishuhudia vipaji vya wanafunzi wa Mwandege Boys Sec |
| Mashairi nayo yalisomwa kuwaaga wahitimu |
| Mmoja wa wazazi akitoa nasaha zake |
| Mzazi wa kiume naye alitoa nasaha zake. |
| Mkuu wa Shule ya Mwandege Boys, Mwl Enock Walter akisoma risala |
| Mwanafunzi wa Pre Form One, Benard Deogratius aliyefanya vizuri katika masomo yake hayo akikabidhiwa zawadi na Mgeni rasmi |
| Mhitimu akikadhiwa cheti chake |
| Hata walimu nao walitunukiwa vyeti kwa kufanya vyema shuleni MwandegeBoys Sec |
| Mmoja ya wahitimu akikabidhiwa cheti na DC Mercy Sillah |
Friday, November 22, 2013
Maguli aomba sapoti nje ndani Kili Stars ibebe Chalenji Kenya
![]() |
| Elias Maguli |
Maguli alisema kwa watanzania wanaobaki nyumbani waiunge mkono timu hiyo kwa kuiombea dua na kuifanyia maombi, huku wale wa wanaishi Kenya kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwashangili ili timu hiyo ifanye vyema katika michuano hiyo inayoshirikisha timu za nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza na MICHARAZO mchana huu katika mahojiano maalum, Maguli anayeichezea Ruvu Shooting na kushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, alisema bila kuungwa mkono ni vigumu Kili Stars kufanya vyema katika michuano hiyo.
Maguli alisema wachezaji wa kikosi hicho kinachotarajiwa kuondoka Jumatatu kabla ya Alhamisi kuwavaa Chipolopolo ya Zambia wamejiandaa vya kutosha kuwapa raha watanzania kutokana na maandilizi waliyofanya chini ya kocha wao, Kim Poulsen, lakini sapoti ya mashabiki ni muhimu.
"Wachezaji tumejiandaa vya kutosha kutowaangusha watanzania, nasi tunaomba tuungwe mkono kwa wlaiopo Kenya wajitokeze uwanjani na wale wa nyumbani watuunge mkono kwa sala na maombi na hatimaye tutarejea na kikombe Mungu akipenda," alisema.
Kuhusu kuwemo kwenye kikosi hicho cha Kili Stars, Maguli alisema anajisikia fahari kwa kuwa Tanzania ina wachezaji bora na nyota lakini kocha amemuona anastahili kuiwakilisha nchi na atapigana kiume akishirikiana na wenzake ili kuipa timu hiyo taji lake la nne.
Tanzania Bara imenyakua ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1974, 1994 na 2010 na mara nyingine zote tangu michuano hiyo ianze kutambuliwa kama Chalenji miaka 40 iliyopita imekuwa kama msindikizaji tu.
Breaking Newzz: Zitto Kabwe apigwa 'stop' CHADEMA
![]() |
| Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeeman Mbowe akizungumza kwenye kikao hicho (Picha:CHADEMA Blog) |
MICHARAZO inafuatilia kwa kina na itawafahamisha, hii ni ikiwa ni maamuzi ya kikao cha Kamati kuu ya chama hicho kilichoanza kukutana tangu juzi.
Nyilawila awashukia mabondia wenzake wanaendekeza wanga
BONDIA Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani
za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema hapendezwi na
vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini.
Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa
wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia
kufanya vema,"alisema.
Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano
lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake
jitihada zake binafsi ulingoni ndizo zitakazomfaa.
Alisema watu wasitafute mchawi aliyesababisha Tanzania isifanye vema
kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa
wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake
Seleman Zugo na kwamba amejipanga
kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za
mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa KO ya raundi
ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika Novemba 10 jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)













