STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Real Madrid haishikiki Hispania yapiga mtu 4-0

Gareth Bale akiwajibika uwanjani usikuwa jana
KLABU ya Real Madrid imeendelea kugawa dozi kwa wapinzani wao baada ya usiku ya jana kuifumua Real Sociedad kwa mabao 4-0 licha ya kucheza ugenini.
Mabao ya Illarramendi katika dakika ya 45 na mengine ya kipindi cha pili kupitia Gareth Bale, Pepe na Alvaro Morata yalitosha kuipa uipa ushindi muhimu vijana hao wa Carlo Ancelotte wakati wakielekea kwenye pambano lao la marudiano la Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Borussia Dortmund.
Ushindi huo umeifanya Madrid kufikisha pointi 76 baada ya kucheza mechi 32 na kuendelea kupumua nyuma ya Barcelona na Atletico Madrid wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 79 moja zaidi ya Barca yenye 78.

Ni kusuka au kunyoa jimbo la Chalinze leo

Mgombea wea CCM, Ridhiwani Kikwete
Mathayo Torongey wa CHADEMA
UCHAGUZI mdogo wa ubunge Chalinze, Bagamoyo, mkoani Pwani unaofanyika leo ambapo jumla ya vituo 288 vya kupigia kura vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 vitatumika tena.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo jana, msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Samuel Salianga, alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 95 na vifaa muhimu vimesambazwa kwenye vituo hivyo.

Alivitaja vyama vitano vinavyoshiriki uchaguzi huo kuwa ni CCM, CHADEMA, CUF, NRA na AFP huku akibainisha idadi ya wapiga kura kuwa ni 92,939.

Kwa upande mwingine Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Chalinze kuhakikisha vinawatumia mawakala wanaotoka eneo la vituo ili wawatambue wapiga kura wa eneo hilo.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema sheria haikatazi vyama hivyo kuteua mawakala kutoka majimbo mengine ya uchaguzi lakini ni vema kuwateua wale wanaotoka eneo lenye wapiga kura wanaowafahamu.

Licha ya kuwepo kwa idadi hiyo ya waliojiandikisha katika daftari la kupiga kura lakini kuna wasiwasi wa wapiga kura kutofikia idadi hiyo kutokana na miundombinu ya baadhi ya maeneo kuharibiwa na mvua zinazonyesha mkoani hapa.

Kufanyika kwa uchaguzi huo kunatokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Said Bwanamdogo, ambaye alifariki dunia Januari 22, mwaka huu.

Hospitali ya TMJ yanusurika kuungua, wagonjwa waokolewa kijeshi

Baadhi ya wagonjwa wakiwa wametolewa hospitali ya TMJ baada ya nyumba ya jirani kuwaka moto. Walitolewa wodini kwa tahadhari.
Mgonjwa alitolewa nje ya wodi na jamaa yake.
Askari wakiwa katika hekaheka za kuzima moto.
Mama huyu mgonjwa akitolewa wodini na ndugu yake baada ya nyumba  jirani kuwaka moto.
Gari la Zima Moto likiwa nje ya hospitali ya TMJ.
Mhudumu akimtoa nje ya wodi mgonjwa, kwa tahadhari baada ya nyumba jirani na hospitali hiyo kuwaka moto.
 
Kikosi cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa iliyokuwa ikiungua ni hospitali.
 
Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya nyumba jirani kuwaka moto.
Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam ilizushiwa kuwaka moto baada ya nyumba jirani kulipuka moto, hali iliyosababisha hekaheka kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya kuwatoa nje wagonjwa kwa tahadhari.
Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana na wasiwasi kuwa moto huo ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini ulidhibitiwa na kikosi cha zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya jirani.
Picha: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging

Ajabu! Huyu jamaa nouma, hali chakula ila matofauti tu

3
Mama yake  huwa anamuandalia kuku kama chakula cha siku lakini anakataa na kutaka apewe vipande vya matofali.
Kwa siku moja anakula vipande kadhaa vya matofali ambapo kwa makadirio huwa anakula kilo 3 kila siku.
Fundi huyo wa kujenga nyumba Pakkirappa Hunagundi anasema kwamba ameanza kula vitu kama hivyo tangu akiwa na miaka 10 na anaweza kukosa chakula lakini hawezi kukosa kula vipande vya matofali.
Akiwa anapata chakula chake hicho akipendacho(matofali) huwa anahitaji kikombe cha maji tu ili kushushia na mwenyewe anasisitiza kwamba hajisikii tofauti kabisa.
Mkazi huyo wa kijiji cha Karnataka nchini India anasema anataka kuzunguka India nzima akionyesha watu uwezo wake huo na kujipatia pesa kwa kuonyesha maajabu hayo.
Angalia hii video uone jinsi jamaa anavyomega matofali.
a
1
b

Side Boy Mnyamwezi hana mpango na albamu

Side Boy katika pozi tofauti
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Said Saleh 'Side Boy Mnyamwezi' amaesema hana mpango wa kutoa albamu kama alivyowahi kufanya siku za nyuma badala yake ataendelea kuangusha 'singo' moja moja baada ya kutofaidika na albamu zake za awali.
Akizungumza na MICHARAZO, Side aliyeachia wimbo mpya wa 'Usimdharau Usiyemjua' aliyoimba na Ney wa Mitego, alisema kutokana na unyonyaji na uharamia wanaofanyiwa wasanii kupitia mauzo ya albamu, jambo ambalo hate yeye limemkuta ameamua kutotoa tena albamu kama alivyokuwa amepanga.
Side Boy, alisema ni bora kutoa wimbo mmoja mmoja na video yake kuliko kutoa albamu inayogharimu mamilioni ya fedha na kuishia kuambulia patupu.
"Sina mpango wa kutoa albamu kama nilivyowahi kufanya siku za nyuma, kwa sasa nitakuwa natoa 'singo' tu kwa lengo la kujitengenezea nafasi ya kuvuna fedha na kupata mialiko ya maonyesho," alisema.
Side Boy siyo msanii wa kwanza kutoa msimamo huo kwani, kauli kama hiyo iliwahi kutolewa na wasanii mbalimbali kutokana na kinachoelezwa wizi na unyonyaji unaowafanya wasanii wasinufaike na jasho lao

Yanga, JKT Ruvu vita ya 'wajuanao', mambo yapo Tanga!

Yanga yenye mtihani mzio kwa JKT Ruvu
MABINGWA watetezi leo wataikabili JKT Ruvu katika mechi inayotazamwa kama 'vita' na mtihani wake wa kwanza kuendelea kuipa presha Azam kwenye mbio za kunyakua taji lao la kwanza, lakini pia ni pambano linalokutanisha timu zinazofundishwa na makocha wanaofahamiana.
Fred Felix Minziro aliyekuwa kocha Msaidizi wa Yanga kwa sasa ndiye kocha mkuu wa JKT akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyemrithi nafasi yake Yanga, kitu ambacho ni wazi timu hizo zinakutana huku kila mmoja akifahamu udhaifu na uimara wa adui yake.
Pambano hulo ambalo litatoa picha halisi kwa Yanga kama inautema ubingwa au itaendelea kusubiri mpaka mechi zake nyingine tatu, litachezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Ingawa ina mechi moja mkononi dhidi ya viongozi wa ligi kuu ya Bara, kimahesabu Yanga iliyo nafasi ya pili imeshavuliwa ubingwa kutokana na kuwa nyuma ya Azam (53) kwa tofauti ya pointi saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya Bara.
Matumaini pekee ya Yanga (46) kutetea taji hilo ni kuomba Azam ipoteze angalau mechi mbili katika michezo yake mitatu iliyobaki. Tatizo ni kuwa 'Wauza Koni' hao hawajafungwa msimu mzima.
Aidha, kwa kuwa kocha msaidizi wa Yanga mpaka Desemba mwaka jana, Minziro amesema anajua siri za udhaifu wa mabingwa watetezi hao na atajaribu kuzitumia katika mchezo wa leo.
Yanga ambayo ilikuwa ikipaa kwenye ligi ya kuu ya Bara, imepoteza uelekeo tangu itolewe kwa taabu na Al Ahly ya Misri kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwanzoni mwa mwezi uliopita, ikishinda mechi moja tu kati ya nne zilizopita.
Tangu kushinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kuikabili Ahly, Yanga imetoka sare na Mtibwa Sugar na Azam, kukifunga kibonde Rhino na kulazwa 2-1 na timu dhaifu ya Mgambo JKT iliyocheza na watu 10 kwa saa moja.
Hata hivyo kocha msaidizi wa Yanga Cherles Boniface Mkwasa alisema licha ya kuwa katika mazingira magumu timu yake haijakata tamaa ya kutetea ubingwa huo hata hivyo.
"Kikubwa ni kushinda michezo yote iliyobakia. JKT Ruvu ni timu nzuri lakini naamini sisi ni wazuri zaidi yao na tunaomba ushindi Jumapili," alisema Mkwasa na kueleza zaidi:
"(Kimsingi) tumezidiwa kwa pointi nne na Azam lakini bado hatujakata tamaa kwa sababu kwenye mpira lolote linaweza kutokea."
Ingawa maandalizi ya Yanga kwa ajili ya mchezo huo yalifunikwa na taarifa za kutimuliwa kwa baadhi ya wachezaji muhimu na Emmanuel Okwi kugomea mazoezi, uongozi wa Yanga ulikanusha taarifa hizo za kwenye vyombo vya habari.
Mechi nyingine za ligi kuu ya Bara leo zinakutanisha Coastal Union na Mgambo JKT, JKT Oljoro na Prisons, na Rhino Rangers na Mtibwa Sugar.
Pambano la jijini Tanga baina ya wanadugu Coastal na Mgambo ndilo lenye mvuto kutokana na Mgambo kuonyesha ukali wake kwa vigogo kwa kuwatungua Simba na Yanga, huku Coastal yenyewe ikionekana imeridhika na nafasi iliyonayo baada ya makeke yao ya awali kuwatumbukia nyongo mashabiki wake.
Mgambo inahitaji ushindi ili ijiondoe kwenye janga la kushuka daraja na Coastal itataka kushinda kuendelea ubabe kwa vijana hao na pia kulinda heshima yake.