STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, October 11, 2013

SHANGWE ZA EID KUPAMBWA NA MASHAUZI CLASSIC


Kocha Wailes ampaisha Gareth Bale

http://www.scaryfootball.com/wp-content/uploads/2013/05/gareth-bale-and-ronaldo-real-madrid-transfer-2013-zidane.png
bale akiwa amebebwa na Ronaldo
KOCHA wa timu ya taifa ya Wales, John Toshack alizungumza na kituo cha radio cha 'La Xarxa' cha Hispania kuhusu mchezaji wake Gareth Bale na akasema kwamba nyota huyohayuko mbali sana na ubora walionao Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Alisema: "Sitaki kuingia katika mijadala kuhusu thamani yake, lakini ninaloweza kusema sasa ni kwamba Bale hayuko mbali sana na matawi aliyopo Cristiano Ronaldo na Messi."
Toshack pia alisema winga huyo wa zamani wa Tottenham hahusiki kwa lolote katika kiwango kikubwa cha pesa kilicholipwa ili kumhamishia Real Madrid, akisema: "Mchezaji si wa kulaumiwa kwa ada ya euro milioni 100 iliyolipwa ili kumsajili. Kama klabu mbili husika zimeafikiana bei hiyo, hayo ni makosa yao."
Pia aliwataka watu wawe wavumilivu kwa nyota huyo ili azoee mazingira mapya. "Alikuwa na bahati mbaya hakujifua katika kipindi cha kujiandaa na msimu, kutokatana na mvutano uliokuwapo baina ya Tottenham na Real Madrid, lakini Bale ni mchezaji mzuri. Hakuna sababu yoyote ya kutilia shaka uwezo wa Gareth Bale, nawahakikishia," alisema kwa kujiamini.
Kocha huyo wa Wales pia alizungumzia hali ya vipaji vinavyoibukia Real. "Kwa mfano watu kama Illarramendi, Isco au wachezaji yosso wa El Castilla (Real Madrid B), kama wakiangalia benchi la Ancelotti na Zidane linaleta matumaini. Kwa sasa ni wakati mgumu kwao kwa sababu Barcelona wanafanya vyema, huku Madrid wakiwa nyuma yao kwenye msimamo, lakini wanahitaji kupewa muda,” alisema kocha huyo Wales.

Thursday, October 10, 2013

Eid El Hajj kusherehekewa J'5 BAKWATA watoa taarifa


HATA hivyo wakati BAKWATA wakitoa taarifa hiyo ni kwamba kwa wale wanaofuata mwezi muandamo wa kimataifa ni kwamba Waislam watafunga Arafah kuwaunga mkono mahujaji siku ya Jumatatu na kuisherehekea sikukuu Jumanne itakayokuwa Oktoba 15, yaani siku moja kabla ya ile iliyotangazwa na BAKWATA.
Funga ya Arafah ni muhimu kwa waumini wa kiislam ambao hawakubahatika kwenda Hijja kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) kufunga Swawm siku ya 'Arafah kwa sababu ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili; mwaka uliopita na baada yake (Hadiyth katika Swahiyh Muslim).
Hivyo MICHARAZO inawakumbusha waumini wa dini hiyo kutoisahau swaumu hiyo, japo tumesisitizwa kufunga tangu Mfungo tatu unapoingia katika makundi ya mwanzoni, lakini kwa wale walioshindwa kutekeleza ibada hiyo shime wasiiache Arafah kwa manufaa yao ya kidunia na Ahera Inshallah

Minziro:Msituchonganishe Yanga



Wachezaji wa Yanga wakishuka, mbele ni Mbuyu Twite wakishuka uwanja wa Ndege Bukoba
Nizar Khalfani nae yupo kwenye kikosi
Wachezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege
Tayari wamekanyaga Ardhi ya Bukoba
Kama kawaida: kushoto ni Khalfan Ngassa kulia ni Niyonzima
Picha ya Pamoja Viongozi na wachezaji
Dida kushoto akipata picha ya pamoja na wenzake
Kocha mkuu wa timu ya Yanga
Asante tumefika salama kazi ni moja ...ushindi ni muhimu Kaitaba
Niyonzima akiwa na Mdau wake wa bukobasports.com
Kelvin Yondani akifurahia baada ya kutua Bukoba asubuhi hii.

Bw. Jamal kalumuna kushoto akiwa na kiongozi wa Yanga
Smart Hotel
Wachezaji wakiingia Smart Hotel
Bw. Ernest Nyambo na Jamal Kalumuna wadau wakubwa wa Yanga Bukoba. (Picha: Lenzi ya Michezo)
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro amewajia juu baadhi ya waandishi wa habari na kuwaambia 'msituchonganishe'.
Minziro alitoa kauli hiyo alipoigiwa simu na MICHARAZO kujua msafara mzima wa timu yao kuelekea Bukoba kuumana na Kagera Sugar siku ya Jumamosi na iwapo kama walimjumuisha beki wa kati Kelvin Yondani aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba alikirofichana na kocha mkuu, Ernie Brandts kiasi cha kuvua jezi na kutupa chini kisha kususia mazoezi.
Kocha huyo, nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema hakuna tukio lolote lililotokea baina ya Yondani na kocha mkuu na ndiyo maana mchezaji huyo yupo kwenye msafara wa wachezaji 21 kwa ajili ya kuivaa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba.
"Ndugu yangu huyo aliyekuambia kwamba Yondani kagombana na kocha ana yake, na ningependa kuwaambia wazi Yanga hatutaki mtuchonganishe, tupo shwari na hivi sasa tumetua Bukoba salama," alisema Minziro.
Alisema Yondani ni miongoni mwa wachezaji 21 wa Yanga walioenda Bukoba kuhakikish Yanga itaibuka na ushindi dhidi ya wenyeji wao ambao anakiri huwa wasumbufu kwenye dimba lao la nyumbani.
"Msitugombanishe kabisa, tupo shwari tayari kwa kuisulubu Kagera, tumekuja kusaka ushindi huku hivyo tuacheni," alisisitiza Minziro.
Alidokeza kuwa kwa maandalizi waliyofanya dhidi ya mchezo huo ana imani kubwa ya kuibuka na ushindi Jumamosi licha ya kutarajia upinzani mkali wa wenyeji wao hao walkiowatungua katika mechi kama hiyo ya msimu uliopita iliyochezwa Oktoba 8, 2012 ambapo Yanga walilala kwa bao 1-0.

P Square kutua Bongo na wasanii 13

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,(kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wake leo na wanahabari kuhusu ujio wa P Square. Kushoto ni Mtangazaji, Hillary Daud 'Zembwela'.
WASANII mapacha kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye, watatumbuiza kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambapo wanaletwa na East Africa Radio na TV chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, mtangazaji wa kituo hicho, Hillary Daudi maarufu kama Zembwela alisema show hiyo itakuwa ya aina yake.
“Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema.
“Hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa Bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi.”Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema Vodacom inafurahi kuendelea kuwa sehemu ya kutoa burudani kwa jamii ya Watanzania na safari hii ikiwaleta wasanii ambao ni kipenzi cha Watanzania wengi.
“Siku zote Vodacom imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa Watanzania, kuanzia katika burudani na hata huduma nyingine za mawasiliano na kijamii. Tunaendelea kuunga jitihada za kuwainua wasanii wetu wa ndani kwa kuwapatia fursa ya kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao wakubwa waliofanyikiwa kufanya kazi zao Kimataifa,” alisema.
“Kwa wateja wa Vodacom ambao pia ni mashabiki wa wasanii hawa ambao wanatamba na kibao chao kitamu cha ‘Personally’ kwa sasa wanayo fursa ya kufurahia nyimbo hizi kwa kuzidownload au kuzitumia kama miito ya simu (RBT) na kuweza kujishindia tiketi za onesho hilo. Natoa wito kwa Watanzania wapenda burudani kutembelea ukurasa wetu wa Facebook na Twitter kwa taarifa zaidi na kujua namna ya kujishindia tiketi za onesho hilo.”

Henry, Redondo, Baba Ubaya kuwakosa Prisons

Henry Joseph



Redondo



NYOTA watatu wa Simba, Issa Rashid 'Baba Ubaya', Henry Joseph na Ramadhani Chombo 'Redondo' wamefahamika hawatakuwepo kwenye pambano kati ya timu yao na Prisons-Mbeya siku ya Jumamosi.
Baba Ubaya atalikosa pambano hilo kwa sababu ya kuwa majeruhi sawa na ilivyo kwa kiungo mkabaji Abdallah Seseme na beki wa pembeni Miraj Adam waliovishwa POP.
Henry na Redondo watakosekana katika mechi hiyo kutokana na kuenguliwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach, Kigamboni.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ni kwamba klabu yao imekuwa na utaratibu wa kuingia kambini kila wanapokabiliwa na mechi na wachezaji wanaofanya vyema kwenye mechi iliyopita na mazoezini ndiyo hujumuishwa kambini kutokana na mapendekezo ya makocha.
Kamwaga alisema hivyo kwa mtazamo wa makocha wao, Henry na Redondo hawakuwaridhisha na ndiyo maana wameungana na makinda wengine waliosajiliwa katika kikosi hicho kutoitwa kambini.
"Huu ni utaratibu wa kawaida na umekuwa ukitumiwa tangu alipokuwepo kocha Patrick Liewig, huwa nasema Simba ya sasa ni 'Simba-LUKU', yaani kadri unavyonunua umeme ndivyo utakavyoutumia na wachezaji kadri wanavyofanya vyema ndivyo wanavyopimwa na makocha," alisema.
Kamwaga alisema hajaelewa ni kwa nini  baadhi ya vyombo vya habari vimeliona tukio la kutoitwa kambini kwa akina Redondo na Henry kuwa kitu cha ajabu wakati ni utaratibu uliopo siku zote Simba.
"Klabu imesajili wachezaji 36 wakiwamo wale wa U20, na kambini huingia wachezaji 25 hasa wanaofanya vyema na kushawishi makocha, hivyo kuachwa kwa akina Henry na Redondo sidhani kama ni issue kubwa wakati msimu uliopita tulikuwa tunaingia kambini bila akina Boban, Kazimoto na watu hawakusema lolote," alisema Kamwaga.
Simba ina kibarua kigumu mbele ya Prisons ambayo imeonyesha kuzinduka hivi sasa ili kuweza kulinda nafasi yao kileleni kwani tayari inapumuliwa na timu za Azam na Mbeya City na iwapo itateleza na Yanga kushinda Kagera siku ya Jumamosi inaweza kuwaengua katika nafasi hiyo.
Mechi nyingine kwa wikiendi hii ni zile zitakazochezwa Jumapili kwa Ashanti kuvaana na Coastal Union kenye uwanja wa Chamazi, Ruvu Shooting kuvaana na Rhino Rangers uwanja wa Mabatini-Mlandizi, Mgambo JKT kujiuliza kwa Mbeya City jijini Tanga, Azam kuwaalika JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa wakati Mtibvwa itapepetana na Oljoro JKT kwenye mashamba ya Miwa ya Manungu Turiani Morogoro.

Kibadeni kupasua la rohoni kesho Msimbazi


Kocha wa Simba  Abdallah Kibadeni akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo
KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni kesho anatarajiwa kuteta na wanahabari kuweka mambo sawa juu ya kinachoendelea katika kambi ya klabu yake pamoja na maandalizi yao dhidi ya mchezo wao na Prisons-Mbeya utakaochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza na MICHARAZO, Kibadeni alisema amelazimika kuitisha mkutano huo kutokana na baadhi ya magazeti kuripoti taarifa 'mbaya' dhidi ya kambi yake na benchi nzima la Simba kitu alichodai kinachafua taswira ya Simba na kuleta sintofahamu miongoni mwa wanachama na mashabiki wao.
Kibadeni aliyeichukua timu hiyo baada ya Mfaransa Patric Liewig kutimuliwa alisema mkutano huo utafanyika majira ya saa 5 asubuhi ya kesho kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi.
"Kuna baadhi ya wanahabari wamekuwa wakituchonganisha Simba, hivyo nimeitisha mkutano kesho nizungumze kuweka mambo sawa, kadhalika kuelezea maandalizi ya jumla dhidi ya pambano leo na Prisons," alisema Kibadeni maarufu kama King Mputa.
Kibadeni aliongeza kuwa, kuanza sasa wanahabari watakaotaka kujua chochote kuhusu Simba ni lazima wapate taarifa hizo kwa Msemaji wa Klabu, Ezekiel Kamwaga hata yale ya ufundi ambapo atakuwa anawauliza benchi la ufundi na kutoa majibu kwa wanahabari ili kuhofia kuivuruga Simba inayoongoza Ligi Kuu kwa sasa ikiwa na pointi 15.
Naye Msemaji wa Simba, Kamwaga alithibitisha kuwepo kwa mkutano huo wa kesho, akidai kocha wao hajafurahia na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa zinazoonekana kama zina lengo la kuivuruga timu yao.

Hatimaye Mwananchi lamaliza kifungo kuanza kutoka tena kesho

GAZETI LA MWANANCHI LATOKA KIFUNGONI
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications limited(MCL)Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji wa gazeti la Mwananchi kuanzia Oktoba 11, lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Bernard Mukasa.

Wednesday, October 9, 2013

Diamond, Wema Sepetu, kitu na box

BAADA YA kuzikanusha taarifa kwamba amerudiana na zilipendwa wake, Wema Sepetu imefahamika wazi kwamba Diamond Platnumz sasa ni kitu na box na mlimbwende huyo.
aada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Awali kulikuwa na taarifa wawili hao wamerudiana walipokuwa Malaysia Diamond alipoenda kutumbuiza na Wema kwa shughuli zake binafsi, lakini msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya alikanusha.
Hata hivyo picha zilizonaswa zimewaonyesha wawili hao walikuwa wakiuhadaa umma kwani hakuna ubishi ni ng'ari ng'ari mwanzo mwisho.


Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny

Nini nitakachofuata...TUSUBIRI!

BaabKubwa

Mbeya City yazidi kupepea, Azam, Mtibwa Sugar wazinduka


Mbeya City

WAKATI Azam ikizinduka na kuondoka na 'mdudu' wa sare baada ya kuitungua Mgambo JKT mabao 2-0, wageni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mbeya City ya jijini Mbeya imeendelea kutakata baada ya kuisasambua Rhino Rangers nyumbani kwao mjini Tabora kwa kuilaza mabao 3-1.

Ushindi wa timu hizo mbili zimezifanya ziisogelee Simba kwa kufikisha pointi 14, moja pungufu na zile ilizonazo vinara hao ambao leo hawakushuka dimbani.
Azam ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na shukrani zikienda kwa kinda Faridi Mussa Maliki na Kipre Tchetche na kuipeleka Azam hadi nafasi ya pili mbele ya Mbeya City wakizidi kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine, Ruvu Shooting imetoshana nguvu dhidi ya maafande wenzao wa Oljoro JKT baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, mabao ya timu hizo yakifungwa na Elias Maguri wa Ruvu na Fikiri Mohammed wa Oljoro waliyofunga kila mmoja mawili.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Mtibwa Sugar imezinduka nyumbani kwao Manungu Morogoro baada ya kuwatungua JKT Ruvu mabao 2-1 na kujivuta hadi nafasi ya tisa.
Mabao mawili ya Juma Luizio yalitosha kuibeba Mtibwa ambao mwishoni mwa wiki walinyanyaswa na Yanga kwa kulazwa mabao 2-0, na mkongwe Salum Machaku akiifungia JKT bao pekee la kufutia machozi.

Mfanyabiashara mwingine amwagiwa Tindikali, safari hii Arusha

 
MFANYABIASHARA mkazi wa Sakina jijini Arusha, Japhet Minja anadaiwa kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni tindikali na watu wasiofahamika na kuachwa na majeraha usoni na mikononi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha zinasema kuwa Minja alikumbwa na tukio hilo eneo la Shamsi Kata ya Elarai baada ya kumwagiwa kimiminika hicho na kuachwa na maumivu makali.
Akizungumza katika hospital ya Seriani alikola wa, Minja ambae ni mfanyabiashara adai alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya masuala ya kibiashara na ghafla wakiwa njiani ghafla alizuiwa na watu hao waliofunga njia na kumdhuru.
Daktari wa zamu aliyempokea mgonjwa huyo Godbless Masawe amesema walimpokea
mgonjwa huyo jana asubuhi akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na
kulazimika kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi na kwa sasa Minja anaendela vyema kwa sasa.

Yaillah Toba, Ajali nyingine tena yahusisha magari matatu

  GA
 Lori la Mizigo likiwa limeacha njia leo, baada ya kugongana na basi katika eneo la Kabuku mkoani Tanga na kuyahusisha magari matatu katika ajali hiyo. (Picha na Francis Dande) 
 Askari wa usalama barabara wakiwa katika eneo la tukio.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali iliyoyakutanisha malori mawili pamoja na basi la abiria lenye namba za usajili T 158 BXG, iliyotokea leo katika eneo la Kabuku, mkoani Tanga

Uchaguzi Bodi ya Ligi wapigwa dochi, Rufaa za wagoimbea TFF kupitiwa kesho


Na Boniface Wambura
UCHAGUZI wa viongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) sasa utafanyika Oktoba 25 mwaka huu badala ya Oktoba 18 mwaka huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesogeza mbele uchaguzi huo kutokana na maombi ya Kamati ya Ligi kwa vile baadhi ya wajumbe wa Baraza la Bodi hiyo kuwa vilevile wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.

TFF itafanya Mkutano Mkuu wake Oktoba 26 mwaka huu ambao utakuwa na ajenda za kawaida kama zilivyoainishwa katika Katiba yake wakati ajenda ya uchaguzi itakuwa Oktoba 27 mwaka huu.

Wagombea uongozi TPL Board ni Hamad Yahya Juma anayewania nafasi ya Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Abeid. Wanaowania nafasi za ujumbe katika Kamati ya Uongozi ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni inatarajia wakati wowote kutangaza tarehe ya kuanza kampeni kwa wagombea katika uchaguzi huo. Baraza la Bodi linaundwa na wajumbe 38 ambao ni wenyeviti 14 wa klabu za Ligi Kuu na wenyeviti 24 wa klabu za Daraja la Kwanza.
Wakati huo huo Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda itakutana keshokutwa (Oktoba 10 mwaka huu) kusikiliza rufani zilizowasilishwa mbele yake.

Waombaji uongozi watatu wamekata rufani katika Kamati ya Jaji Luanda wakipinga kutopitishwa kugombea katika uchaguzi wa TFF, uamuzi uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ajili ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Warufani ni Samwel Nyalla aliyeondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 2 ya mikoa ya Mara na Mwanza kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi TFF kwa kutoonesha malengo yake.

Ayoub Nyaulingo yeye anapinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 6 (Katavi na Rukwa) kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Naye Ayoub Nyenzi amekata rufani kupinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha Kanda namba 7 (Iringa na Mbeya) kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.

Ndanda, Green Warriors hapatoshi leo FDL

Na Boniface Wambura
GREEN Warriors ya Dar es Salaam na Ndanda ya Mtwara zinaumana kesho (Oktoba 9 mwaka huu) katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mshindi atakamata uongozi wa kundi A.

Mechi hiyo ya raundi ya tano itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo timu itakayoshinda itafikisha pointi kumi na kuipiku African Lyon inayoongoza sasa kundi hilo ikiwa na pointi tisa.

Kwa upande wa kundi B kutakuwa na mechi tatu ambapo Polisi Morogoro inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi tisa itakuwa ugenini dhidi ya Majimaji inayokamata mkia ikiwa na pointi moja. Mechi itachezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kurugenzi itakuwa kwenye uwanja wake wa Wambi ulioko Mafinga mkoani Iringa kuikabili Burkina Faso ya Morogoro wakati Uwanja wa CCM Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Kimondo na Mkamba Rangers.