STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 7, 2014

Prisons, Ruvu hapatoshi Mbeya kesho, FDL kutimka

Kikosi cha Prisons-Mbeya


Ruvu Shooting

Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 8 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi nyingine nne za ligi hiyo zitachezwa keshokutwa (Februari 9 mwaka huu) kwenye viwanja mbalimbali.
Mgambo Shooting vs Simba (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT vs Kagera Sugar (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers vs Coastal Union (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Mbeya City vs Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya).
Katika hatua nyingine, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) unaanza kesho (Februari 8 mwaka huu) kwa mechi za kundi A na B wakati kundi C lenyewe litaanza mechi zake Februari 22 mwaka huu. Mechi za kundi A ni Green Warriors vs Tessema (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi), Polisi Dar es Salaam vs Transit Camp (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Februari 9 mwaka huu ni African Lyon vs Villa Squad (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi) na Friends Rangers vs Ndanda (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Kundi B kwa kesho (Februari 8 mwaka huu) ni Polisi Morogoro vs Burkina Faso (Jamhuri, Morogoro), Lipuli vs Mkamba Rangers (Samora, Iringa), Kurugenzi vs Kimondo (Wambi, Mufindi) na Mlale JKT vs Majimaji (Majimaji, Songea).

Thursday, February 6, 2014

Kanembwa watatakiwa kuwasilisha utetezi TFF

WACHEZAJI tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).

Utetezi huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.

Kamati ilikutana jana Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko dhidi ya wachezaji hao na timu yao kwa tukio hilo lililotokea Novemba 2 mwaka jana kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Stand United FC iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Wachezaji hao ni Abdallah Mgonja, Bariki Abdul, Philipo Ndonde, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement, Mrisho Mussa, Nteze Raymond, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu. Mlalamikiwa mwingine ambaye naye anatakiwa kujitetea ni timu ya Kanembwa JKT.

Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, Kamati hiyo baada ya kusikiliza malalamiko dhidi ya wahusika na kupokea ushahidi wa aina mbalimbali kutoka kwa mlalamikaji imesema ili iweze kutenda haki katika shauri hilo ni lazima walalamikiwa wapate fursa ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliyokutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa imesema imesikitishwa na vitendo vya fujo ndani ya mpira wa miguu, na kuwataka watu wasijihusishe na aina yoyote ya fujo

Simanzi! Ajali nyingine tena Singida

WASOMAJI WETU TUNAOMBA RADHI KAMA UTAKWAZIKA NA PICHA ZIFUATAZO.
DSC06423
Mtoto mmoja aliyelalaliwa na kusababisha kifo chake na basi la Zuberi T.119 AZZ lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar-es-salaam na kupinduka katika eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi wakati likimkwepa bibi aliyekuwa akikatisha barabara.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC06430
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa katika Hosptali ya Mkoa ya Singida.
DSC06438
Mmoja wa majeruhi akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya mkoa mjini Singida.
DSC06410
Basi la Zuberi T.119 AZZ lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar-es-salaam na kupinduka katika eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi wakati likimkwepa bibi aliyekuwa akikatisha barabara.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC06407
Na Nathaniel Limu, Singida
BASI la kampuni ya Zuberi T.119 AZZ lililokuwa linatokea jijini Mwanza likielekea jijini Dar-es-salaam,limepinduka na kusababisha vifo vya abiria  wawili na kujeruhi vibaya wengine arobaini wakati likimkwepa bibi mmoja aliyekuwa anakatisha barabara.
 Ajali hiyo imetokea jana saa 7.30 mchana katika barabara kuu ya Sindida –Dodoma eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Afisa wa makosa ya jinai mkoa wa Singida (RCO), Thobias Sedoyeka amesema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Fadhili Kalembo (35),lilipofika eneo la tukio,bibi mmoja alijitokeza akiwa anavuka barabara.
Amesema dereva wa basi alijitahidi kumkwepa bibi huyo lakini ghafla bibi alirudi tena barabarani kitendo kilichosababisha basi hilo kupinduka na kuserereka hatua zaidi ya 50 wakati likimkwepa kwa mara ya pili.
 “Basi hili lilimlalia mtoto mdogo ambaye aliweza kutolewa baada ya basi la Zuberi kunyanyuliwa na wichi ya lori ambalo lilikuwa linapita katika barabara hiyo”,amesema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mjini Singida, Deogratus Banuba amesema kuwa wamepokea maiti moja iliyotokana na ajali ya basi la Zuberi na kwamba bado wanaendelea kusubiri mwili wa mtoto aliyefia eneo la ajali.
 “Kwa upande wa majeruhi,tumepokea majeruhi 40 ambao wameumia vibaya sehemu mbalimbali ya miili yao ikiwemo kuvunjika mikono na miguu.Kati yao wanne,mikono yao imesagika vibaya na tumejitahidi kuirudisha katika hali yake”,amesema Dk.Banuba.
Amesema kuwa majeruhi wengine wanne,wao wamewapa  rufaa ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi mjini mkoa wa Kilimanjaro.
Chanzo: Mo blog

Mwenyekiti BASATA awaasa wasanii nchini


Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akikagua nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga jana, kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza

Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akikagua nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga jana, kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza


Na Peter Mwenda, Mkuranga

MWENYEKITI wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Profesa Penina Mlama ametoa wito kwa wasanii kuchangamkia kuchangia ujenzi wa nyumba unaratibiwa na Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) ili kujiandalia makazi.


Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Profesa Mlama alisema makazi ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo wasidharau mradi huo ni faida kubwa kwao.



Alisema nyumba ambazo ameziona ni nzuri, imara na zinauzwa bei ya chini ambayo huwezi kuzipata sehemu nyingine yoyote nchini Tanzania na kuongeza kuwa kujenga kwa lengo la kuishi pamoja kunatoa fursa ya wasanii kubuni njia nyingine ya kuanzisha miradi mbalimbali.



Profesa Mlama alitaka SHIWATA isikate tamaa bali iendelee kuwashawishi wasanii wajiunge na kuchangia ujenzi wa nyumba ili baadaye wasitafute visingizio kuwa hawakupewa fursa hiyo.



Naye Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza alisifu SHIWATA kubuni njia ya kuwasainia wasanii kupata makazi na kuahidi kuwa baraza hilo litatoa ushirikiano na kutoa ushauri kila unapohitajika.



Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba za wasanii utaendelea kote nchini na kuwataka wasanii waungane kufanya kazi zao kwa pamoja.



Alisema mpaka sasa nyumba 38 zimekabidhiwa kwa wasanii waliochangia ujenzi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na nyingine 21 zinatarajiwa kukabidhiwa Machi mwaka huu.



SHIWATA mbali ya kusimamia ujenzi wa nyumba za wasanii inasimamia matamasha ya wasanii wachanga (Underground) kuendesha makongamano ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya na kutoa elimu na maadili kwa wasanii.

Mbunge Mchungaji Msigwa mahakamani kwa kujeruhi

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa sambamba na mtuhumiwa mwingine
akiwa ndani ya mahakama ya wilaya ya Iringa jana kabla ya kuahirishwa kwa kesi yakeya kujeruhi mtu
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa akizungumza na wakili anayemtetea
katika kesi yake ya kujeruhi mtu kwenye kampeni za siasa, Lwezaula Kaijage 
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa sambamba na mtuhumiwa mwingine akiingizwa mahakama ya wilaya ya Iringa jana kujibu mashataka ya kujeruhi yanayomkabili

48 wanaswa vurugu za Morogoro


  Wakazi wa doma wilayani Mvomero wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji kuondolewa eneo hilo.
WATU 48 wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji wa jamii ya Kimasai kuhamisha katika eneo la Doma wilayani Mvomero.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi.
Kamanda huyo alisema kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kuwatia mbaroni wanawake 24 na wanaume 24 ambao wanadaiwa kufanya vurugu hizo.
Alisema kuwa fujo hizo zilitokea baada ya watu hao kudai kuwa wafugaji hao waliwapiga na fimbo wananchi wenzao waliokwenda porini kukata mkaa jambo lililowafanya nao kuamua kufunga barabara hiyo.
Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa walifanikiwa kufungua barabara hiyo majira ya saa 7 mchana baada ya kupiga mabomu ya mchozi kwa lengo la kuwatawanya wananchi hao.
Alisema kuwa hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliotokea ingawa watu hao walijaribu kuwapiga mawe polisi hao .
Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho ili kuweza kujibu tuhuma hizo.
Kwa upande wao wananchi hao wamalalamikia wafugaji hao kitendo chao cha kuingiza mifugo mashambani na kuharibu mazao njambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Pia walilalamikia uongozi wa kijiji hicho cha Doma kwa kuwaingiza wafugaji kinyemela hali inayofanya kuwa wengi huku eneo la malisho likiwa dogo hali inayofanya wafugaji hao kuingiza mifugo yao mashambani.
Ibrahim Ndegalo alisema kuwa mbali na wafugaji hao kuwapiga lakini pia wamakuwa wakiwanyang’anya mali zao bila sabababu na kwamba maisha yao yamekuwa hayana amani.
 Credit:MACHAKU

FF watumia mabomu kutawanya wakulima Morogoro


Askari wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima  Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera  Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya  mvomero


 Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wamishika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.

Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barbara kuu ya Morogoro Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi 
baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo
Askari wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya

Rais Kikwete ahutubia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi na viongozi  wa vyama mbalimbali vya siasa na maafisa wa serikali wakitoka kupata chakula cha mchana baada ya kufungua  mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad  katika picha ya pamoja na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya kufungua  mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad  katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua  mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Sehemu ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Picha na Issa Michuzi

Mchungaji afa maji akiiga kutembea juu ya maji kama YESU

KUTEMBEA juu ya maji siyo kazi rahisi na pengine inaweza kugeuka kilio kama mtu huna imani ya kutosha. 
Huko Nigeria mwanzoni mwa mwezi uliopita ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile Nabii Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. 
Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake. 
Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.
chanzo-http://www.zimeye.org/

Tuesday, February 4, 2014

Mwakilishi wa Kiembe Samaki alivyoapishwa rasmi

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yahya Khamis Hamad, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alipowasili katika Ofisi ya Katibu wa Baraza kwa ajili kujitambulisha na kuhudhuria kuapishwa kwake kuingia katika Baraza la Wawakilishi baada ya kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika wiki iliopita.
 Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuaza kwa taratibu za shughuli za Kikao na kumapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakati wa Kikao cha asubuhi leo.
Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho akisoma Dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza cha Asubuhi leo.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake wakimshindikiza Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiingia katika ukumbi wa Mkutano tayari kwa kuapishwa kwake kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
 Mhe Mhmoud Thaib Kombo, akiapishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuwa Mwakilishi wa Jimbola Kiembesamaki, baada ya kushinda Jimbo hilo na kuwa Mwakilishi Mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.   
  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar kwa kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Mapinduzi Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Vitendea Kazi vya Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
 Waheshimiwa Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mwakilishi wao wa Jimbo la Kiembesamaki wakati akiapishwa katika ukumbi wa Mkutanona Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho leo asubuhi.
 Wanafamilia ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakihudhuria sherehe za kuapishwa kwake leo asubuhi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wageni walioongozana na Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakisimama wakati wa kusomwa kwa Dua kabla ya kuaza kwa shughuli za Kikao cha Baraza leo asubuhi.
Mhe. Mahmoud Thabi Kombo akiwashukuru wananchi wa jimbo la kiembesamaki kwa mashirikiano yao tangu mwazo wa kampeni hadi kupiga kura na kumchagua kuwa mwakilishi wao.Picha Zote na Ramadhan Othman Mapara-Zanzibar

Mzee Kingunge aibuka, ashangaa wanamuandama Lowassa, ashtushwa Mawaziri kuitwa Mizigo

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na MICHARAZO nyumbani kwake jana jijini Dar es salaam.
WAKATI makada wa CCM wakilumbana juu ya kitendo cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kujitokeza hadharani na kuonyesha nia ya kuwania Urais Uchaguzi wa 2015, mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru ameibuka na kusema haoni tatizo na kilichofanya na Mbunge huyo wa Monduli.
Aidha Kingunge amesema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wakuu wa CCM kuwaumbua na kuwadhalilisha baadhi ya mawaziri wa serikali yao kwa kuwaita 'mizigo', akidai kama walikuwa na makosa katika utendaji wao walipaswa kukosolewa ndani ya vikao vya ndani vya chama chao badala ya kuvuana nguo hadharani na kukiaibisha chama.
Kwa wiki sasa kumekuwa na malumbano baina ya wanaCCM wakimnyooshea kidole Lowassa anayedaiwa kuanza kufanya kampeni zinazohisiwa ni harakati zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Miongoni mwa waliomshambulia Lowassa ni Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi-UVCCM, Paul Makonda na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Viongozi hao wameonyeshwa kukerwa na kitendo kinachofanywa na Lowassa kwa kudai anausaka urais kwa kutumia fedha na kutaka chama kimdhibiti, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula naye akigusia suala hilo na kuwaonya wanachama walioanza kampeni kabla ya wakati.
Hata hivyo Kingunge, akizungumza na MICHARAZO jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, alisema haoni tatizo kwa Lowassa na hata mwanachama yeyote ndani ya CCM kujitokeza na kuonyesha dhamira ya kutaka uongozi mapema.
Kingunge alisema kujitokeza mapema kwa mtu mwingine yeyote mwenye dhamira ya kutaka uongozi ni jambo litakalowasaidia wananchi kuwafahamu, kuwajadili na kuwapima kwa kina kuona kama wanafaa kuongoza au la.
Alisema  haoni sababu ya kuibuka malumbano baina ya wanaCCM au kusakamwa kwa Lowassa kwa kitendo chake akidai wengine wanaotaka kufanya hivyo wafanye ili kutoa nafasi kwa wanachama wenzao na wananchi kwa ujumla kuwafahamu na kuwajadili ili ukifika wa uchaguzi wajue la kufanya dhidi yao.
"Sipendi kuingia kwenye malumbano na wanachama wenzangu kwa sababu najua mwishowe watu tunaweza kuvuana nguo, ila kwa mtazamo wangu sioni kama ni kosa kwa wanachama na raia yeyote mwenye nia ya kutaka uongozi kujitokeza na kujionyesha mapema," alisema.
"Kujitokeza kwao mapema kutawafanya wananchi wawaone, wawafahamu, pia wawapime na kuwajadili kwa kina kama wanafaa kubeba majukumu ya uongozi au la, pia sidhani kama ni Lowassa pekee aliyefanya hivyo, vipi asakamwe yeye tu! Siyo dhambi watu wenye nia iwe katika ubunge, udiwani, uenyekiti wa serikali za mitaa na hata urais kuwangong'oneza rafiki na ndugu zao juu ya dhamira yao. Bora hao kuliko wanaofanya mambo yao kwa usiri," alisema.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kwa waziri katika serikali za awamu zote nne nchini tangu enzi za Mwalimu Nyerere, alisema tangu enzi za TANU mpaka kuzaliwa kwa CCM upo msisitizo unaosema raia wote wana haki mbili kuu ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa, ingawa hawalazimishwi.
"Hakuna anayelazimishwa kuchagua au kuchaguliwa kwa maana ya kuwania uongozi, hivyo kujitokeza kwa wanasiasa na watu wengine kuonyesha nia yao yakutaka uongozi hawafanyi dhambi, hivyo sidhani kuna haja ya suala hili kuwa mjadala mkubwa wakati kuna mambo ya msingi ambayo CCM inapaswa kuyazungumza na kuyajadili kwa kina kwa manufaa ya wananchi," alisema.
Juu ya kitendo cha viongozi wakuu wa Sekretarieti ya CCM kufanya ziara mikoani kisha kutangaza majukwaani majina ya mawaziri walioitwa mizigo, Kingunge kwanza alipongeza ziara hiyo akidai itasaidia kukijenga na kuinua uhai wa CCM, lakini alidai hakubaliani na kilichofanywa na viongozi wao kuwavua nguo watendaji hao wa serikali yao.
Alihoji ina maana viongozi wa CCM hawajui mipaka ya uongozi iliyopo baina yao na serikali iliyopatikana kwa ridhaa ya wananchi.
"Zipo taratibu za kukosoana ndani ya chama, mawaziri ni wabunge, wanaCCM kama wamefanya makosa ilipaswa waitwe na kukosolewa katika vikao vya ndani ya chama badala ya kuwavua nguo hadharani kwa kisingizio wananachi ndiyo wanaowalalamikia. Haya hatukuwatuma," alisema.
alisema yapo mambo ya msingi viongozi wa CCM wanapaswa kuyazungumza na kuyajadili mbele ya wananchi ikiwemo mikakati ya kuwaletea maendeleo ili wafurahie uhuru, pia akidai kwa miaka mingi tangu enzi za TANU, CCM kilifahamika kuwa ni chama cha wanyonge, lakini kwa sasa hilo halipo na kuhoji viongozi hao wanapaswa kuliangalia hilo na kukirejesha chama katika mstari.
"Kama wameshindwa kazi ni vyema wakawapisha wengine wakiongoze, kuliko kukiyumbisha chama na kukifanya kipoteze mvuto mbele ya wananchi kwa kujadili mambo yasiyo na maana kwa wananchi hata kama wanapigiwa makofi, CCM ina sera na taratibu zake za kukosoana kupitia vikaoni, siyo kilichofanywa na viongozi wetu," alisema.
Alisema viongozi wa CCM kwa sasa ni kama wanaoanzisha vita baina yao na watendaji wa serikali kitu ambacho siyo tu kinaonyesha chama chao kuyumba, pia kinaonyesha namna gani wanavyofanya kazi ya kuwasaidia wapinzani badala ya kujijenga na kusaidia serikali yao ili waje kushinda katika chaguzi zijazo.
Kingunge alihoji viongozi waliowaita wanachama wenzao 'mizigo' ndani ya serikali  inayotokana na CCM wanatazamanaje na mawaziri hao kuliorejeshwa.
"Sidhani kama ni jambo zuri, watu waheshimu mipaka ya madaraka yao, wajikite katika kukijenga chama na serikali kwa ujumla badala ya vitu visivyo na tija kwa wananchi iliwayowapa ridhaa ya kuongoza," alisema Kingunge.