STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 6, 2013

SJMC, TASWA kuwapiga msasa Waandishi wa Michezo


CHAMA cha Waandishi wa harai za michezo (TASWA) kwa kushirikiana na Chuo cha uandishi wa habari na mawasiliano ya umma (SJMC) wameandaa mafunzo ya siku tano kwa ajili ya waandishi wa habari za michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Mkuu Chuo hicho, Michael Andindile, alisema mafunzo hayo ya siku tano yataendeshwa na Wahadhiri wa Chuo hicho pamoja na waandishi wakongwe wa habari nchini.
"Mafunzo haya yatagusa maeneo makuu ya habari za michezo ikiwemo soka, riadha, ndondi, gofu, mpira wa kikapu pamoja na michezo mingine," alisema Andindile na kueleza zaidi kuwa "tunalenga kuongeza umahiri wa wanahabari katika kuripoti habari za michezo."
Alisema mafunzo hayo yatafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema mafunzo hayo ni frsa adhimu kwa tasnia ya habari, hasa kwa waandishi wa habari za michezo nchini.
"Fulsa hii ni moja ya jitihada za TASWA kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanapatanafasi ya kujifunza zaidi kuhusu namna bora ya kuripoti habari za michezo kwa ujumla wake," alisema Mhando.
Alisema wanahabari waitumie fursa hiyo ya kuongeza ujuzi na uelewa katika habari za michezo nchini.

No comments:

Post a Comment