Baadhi ya wachezaji wapya wa Coastal Union wakisalimiana na wachezaji wa URA ( walioipa mgongo kamera) |
KLABU ya soka ya Coastal Union imesitisha mipango wa kumsajili mshambuliaji chipukizi kutoka Uganda, Nelson Ssenkatuuka badala yake itafanya hivyo katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani ili wamchunguze kwanza kama atawafaa.
Aidha uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imesema haitaenda nje ya nchi kujifua kama ilivyofanya msimu uliopita badala yake itajinoa nyumbani kw akucheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kujiwinda na mechi yao ya ufunguzi wa ligi dhidi ya JKT Oljoro jijini Arusha.
Akizungumza na MICHARAZO, Afisa Habari wa Coastal Union, Edward 'Edo' Kumwembe, alisema wamesitisha mipango ya kumsajili Ssenkatuuka ili kumchunguza zaidi na kama wataridhika naye watafanya hivyo katika dirisha dogo.
Edo alisema wasingependa kukurupuka kusajili mchezaji hasa kwa nafasi hiyo ya ushambuliaji ambayo ndiyo iliyosalia kwa sasa kikosini mwao.
Hata hivyo alisema anaamini waliosajiliwa na timu hiyo wataibeba Coastal katika lipute chja Ligi kinachoanza Agosti 24.
Pia alisema tofauti na msimu uliopita walipoenda Kenya kucheza mechi kadhaa za kujipima nguvu safari suala hilo halitakuwepo na badala yake uongozi unajipanga kutafuta mechi mbili zaidi ya kirafiki hapa hapa nyumbani kabla ya kuanza kwa ligi.
"Uongozi unatarajiwa kukutana leo jioni kwa ajili ya kujadili namna ya kuoata mechi hizo mbili za kirafiki kabla ya kuanza kwa ligi," alisema Edo.
Coastal waliomaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita imesajili wachezaji wapya nane ambao ni viungo kutoka Simba, Haruna Moshi 'Boban' na Uhuru Seleman, beki Juma Nyosso, kipa Said Lubawa, Mkenya Crispian Odulla, Marcus Ndehele, Abdullah Othman Ali na Kenneth Masumbuko aliyeichezea Polisi Moro msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment