Na Boniface Wambura
SEMINA
kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) kwa waamuzi
wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa
2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es
Salaam na Mwanza.
Mafunzo
hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi
Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam
wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.
Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kituo
cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita,
Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,
Singida na Tabora.
Kituo
cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya,
Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment