Na Prince Akbar
YANGA
SC imetuma salamu Johannesrbug, Afrika Kusini ambako Azam FC wameweka
kambi kujiandaa na msimu mpya- kufuatia ushindi wa mabao 5-1 leo katika
mchezo wa kirafiki dhidi SC Villa ya Uganda, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Yanga
na Azam zitamenyana Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, katika mechi ya
kuwania Ngao ya Jamii, kuashiria ujio wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara.
Azam
imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na mechi hiyo ya kufungua msimu
na Yanga wanaendelea na maandalizi yao Dar es Salaam, wakitarajiwa
kuingia kambini baada ya mechi ya leo kisiwani Pemba, au Bagamoyo,
Pwani.
Katika
mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa 3-1,
mabao yake yakifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya saba, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ dakika ya 27 na Didier Kavumbangu dakika ya 30, wakati la
nne lilifungwa kipindi cha pili na Haruna Niyonzima dakika ya 62.
Bao
la kufutia machozi la Villa ambayo jana ilifungwa 4-1 pia na Simba
Uwanja huo huo wa Taifa, lilifungwa na Moses Ndaula dakika ya 18.
Katika
mechi zake za awali za kujiandaa na msimu, Yanga SC ilitoa sare ya 2-2
na URA ya Uganda kabla ya kuzifunga 3-1 Mtibwa Sugar na 3Pillars ya
Nigeria 1-0.
Azam
nayo imekwishacheza mechi tatu za kujipima nguvu Afrika Kusini,
imeshinda moja tu dhidi ya Mamelodi Sundwons 1-0, imefungwa mbili, 3-0
na Kaizer Chiefs na 2-1 na Orlando Pirates na kesho itacheza mechi ya
mwisho na Moroka Swallows kabla ya kurejea nyumbani keshokutwa.
Kikosi
cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David
Luhende/Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Rajab
Zahir, Athumani Iddi ‘Chuji’/Bakari Masoud, Mrisho Ngassa, Salum Telela,
Didier Kavumbangu, Jerry Tegete/Hussein Javu na Haruna Niyonzima/Said
Bahanuzi.
Akaunti mpya; Ngassa amefungua akaunti mpya ya mabao Yanga leo |
No comments:
Post a Comment