STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 13, 2017

Barcelona, Real Madrid zatenganishwa

BAADA ya mechi za marudiano ya Kombe la Mfalme (Copa del Rey), droo ya Nane Bora ya michuano hiyo ya nchini Hispania imetoka, huku vigogo Barcelona na Real Madrid zikitenganishwa kwenye hatua hiyo.
Katika droo hiyo Real Sociedad itavaana na Barcelona, wakati Real Madrid wakipewa Celta Vigo wakianzia nyumbani, huku Alcorcon itamalizna na Alaves na Atletico Madrid itakwaruzana na Eibar.
Mechi hizo kwa mujibu wa ratiba zitaanza kuchezwa Januari 18-19 na marudiani zitachezwa kati ya Januari 25/26 kwa ajili ya kupata timu za kutinga nusu fainali.
Katika hatua hiyo ya Nane Bora ni klabu moja tu ya Ligi Daraja la Pili ya Alcorcon iliyopenya na zilizosalia zipo La Liga.

Ratiba kamili ipo hivi:

Real Sociedad   v Barcelona
Alcorcon           v Alaves
Atletico Madrid  v Eibar
Real Madrid      v Celta Vigo

No comments:

Post a Comment