STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 13, 2017

Taifa Stars, Uganda The Cranes hapatoshi Afcon 2019

Kikosi chja Tanzania
Droo ya kuwania fainali za Afcon 2019
DROO ya kuwania fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon imefanyika jana usiku na Tanzania kuwekwa kundi moja pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho.
Tanzania ambayo haijashiriki fainali hizo tangu mwaka 1980 kama itakomaa katika maandalizi mazuri inaweza kusonga mbele kwani safari hii kundi lao sio tishio kama ilivyokuwa katika mbio za  kwenda Afcon 2017.
Katika mbio Tanzania ilipangwa na vigogo Misri, Nigeria na Chad kabla nchi hii haijajitoa kundini.
Katika droo hiyo Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na Sierra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR).
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora.
Michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo, Raundi ya Awali itakayohusisha timu za Comoro, Djibout, Madagascar, Mauritius, Sao Tome E Principe na Sudan Kusini.
Timu zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye makundi A, B na C kukamilisha idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu za Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco na Malawi na C kuna Mali, Gabon n Burundi.
Cameroon ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja na kama itashika nafasi ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu moja kwa moja na mshindi wa pili atawania nafasi tatu za ziada za kufuzu kama mmoja wa washindi wa pili bora.
Hatua ya mchujo itachezwa kati ya Machi 20 na 28 wakati mechi za kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na 13, za pili Machi 19 na 27 2018, za tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8 na 16, 2018 na za tano Novemba 5 na 13, 2018.
Mbali za Afcon 2019 Tanzania pia itakuwa na kibarua cha kuwania fainali za Chan 2018 zitakazofanyika nchi ya Kenya.

No comments:

Post a Comment