STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 30, 2014

Leo ni vita tupu ligi kuu Tanzania Bara, Yanga, Azam, Mbeya City kuvuna nini?

Mbeya City wataumana na Prisons Mbeya je wataendeleza ubabe wake kwa maafande hao
Yanga wapo kibaruani Mkwakwani Tanga dhidi ya maafande wa Mgambo

Azam kuendeeleza rekodi ya ubabe katika ligi kuu leo kwa Simba?
KITIMTIM cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea tena leo kwa viwanja sita kuwaka moto, huku vitatu kati ya hivyo vikisubiriwa kwa hamu kutoa picha halisi ya mbio za ubingwa kwa msimu huu kwa timu tatu kati ya nne zinazochuana kileleni.
Viwanja vya Mkwakwani-Tanga, Sokoine-Mbeya na Taifa- Dar es Salaam vitakavyofuatiliwa kwa vile bndivyo vilivyoshikilia hatma ya mbio za ubingwa kwa msimu baina ya timu za Azam, watetezi Yanga na Mbeya City.
Vinara Azam wanaoongoza msimamo wakiwa na pointi 50 watakuwa wenyeji wa Simba uwanja wa Taifa, huku Yanga watakuwa ugenini mjini Tanga kuvaana na Mgambo JKT na Mbeya City iliyo nafasi ya tatu itaumana na 'kaka' zao Prisons iliyotoka kupokea kipigo cha 'paka mwizi' cha mabao 5-0 toka kwa Yanga katikati ya wiki jijini Dar.
Azam iliyopania kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya misimu miwili mfululizo kumaliza nafasi ya pili, inaonekana kuwa na kazi rahisi kuliko Yanga na Mbeya City kutokana na vijana wa Msimbazi, Simba kupoteza 'dira' msimu huu.
Simba iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union haitarajiwi kuipa upinzani Azam walio kwenye kiwango bora kwa sasa ikiwa haijapoteza mchezo wowote katika ligi hiyo inayoelekea mwishoni.
Hata hivyo soka halitabiriki na Azam haipaswi kujiamini kupita kiasi mbele ya Simba, ambayo kama watageuzwa daraja na wapinzani wao itamaanisha kukosa uwakilishi wa nchi kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo na hata nafasi ya tatu kuipata itawahia vigumu.
Simba ina pointi 36 ikisaliwa na mechi nne ukiwamo wa leo na kama itashinda zote itafikisha pointi 48 zilizopitwa na Azam na zinakaribiwa kufikiwa na Yanga wenye 46 wakiwa nafasi ya pili.
Ukiondoa pambano hilo la uwanja wa Taiufa, Yanga wenyewe watakuwa na kibarua kigumu kwa Mgambo JKT walioapa mapema kuwatoa nishai kama walivyofanya kwa Simba mwezi uliopita walipowadungua bao 1-0.
Mgambo iliyo katika janga la kutaka kushuka daraja katikati ya wiki ilifumuliwa na Azam mabao 2-0 hivyo isingependa kupoteza mchi nyingine na ndipo inapooenekana Yanga ina kazi Mkwakwani.
Hata hivyo Yanga yenye safu kali ya ushambuliaji chini ya kocha aliyejijengea jina kubwa kwa kipindi kifupi Mholanzi, Johannes van der Pluijm, inatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi kama ilivyofanywa kwa Rhino Rangers na Prisons ili kutoipa nafasi Azam kuwakimbia zaidi kwenye mbio za ubingwa wakiwa na mechi moja mkononi.
Yanga kabla ya mechi ya leo imecheza michezo 21 na kubakisha mitano ambayo ikishinda yote itafikisha pointi 61, moja zaidi ya zile ambazo itazimaliza Azam iwapo itashinda mechi zake nne zilizosalia.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alinukuliwa  akisema wanaenda Tanga wakiwa na nia moja ya kushinda, ili wasiachwe mbali na Azam wanaowanyima raha hasa baada ya kupepesuka katika mechi mbili walizotoka sare.
Mechi nyingine yenye mvuto kwa leo ni ile ya Mbeya City dhidi ya Prisons-Mbeya ambazo zimekuwa na upinzani kama wa Simba na Yanga.
Katika mechi ya kwanza, Prisons wakiwa wenyeji walikubali kipigo cha mabao 2-0. hivyo kuilifanya pambano la leo kuwa na ushindani mkubwa ikizangatiwa Prisons wametoka kuchezea kipigo cha aibu toka Yanga a Mbeya wapo kwenye mbio za ubingwa.
Mechi nyingine zinazochezwa leo zitakutanisha Kagera Sugar dhidi ya Ruvu Shooting mjini Bukoba, Mtibwa Sugar itaialika Coastal Union mjini Manungu na JKT Ruvu wataikaribisha Rhino Rangers ambapo kipigo chochote kwao kinawashusha rasmi daraja.

No comments:

Post a Comment