BAADA ya vipigo viwili mfululizo klabu ya Real Madrid ikiongozwa na nyota wake Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walirejesha matumaini yao ya ubingwa baada ya kupata ushindi mnono nyumbani kwa kuilaza Rayo Vallecano kwa mabao 5-0.
Bale na Ronaldo walihusika katika mabao manne katia ya matano yaliyowafanya wafikishe jumla ya pointi 73 japo inaendelea kusalia nafasi ya tatu nyuma ya Barceola na Atletico Madridi zilizoshinda mechi zao jana pia.
Bale alimtengenezea mpira Ronaldo na mchezaji huyo bora wa dunia alifunga katika dakika ya 14 kabla ya kumtengenezea Caevajal aliyefunga la pili katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 54.
Hata hivyo winga huyo alifunga mwenyewe mabao mawili katika dakika ya 67 na 70 na bao la mwisho lilifungwa na Morata dakika ya 77.
Atletico Madrid iliyokuwa ugenini ilipata ushindiwa mabao 2-1 dhidi ya Athletico Club kwa mabao ya Diego Costa na Koke, huku bao la wenyeji likifungwa mapema na Muniain.
Kwa ushindi huo Atletico imerejea kileleni ikiwa na pointi 76, moja zaidi ya Barcelona iliyewashusha kwa muda baada ya kupata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Espanyol.
No comments:
Post a Comment