TIMU ya AS Monaco imetoa mwanya zaidi kwa PSG kunyakua taji la ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo baada ya usiku wa jana kukubali kipigo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya Evian TG.
Bao la 'jioni' la mkwaju wa penati lililotumbukizwa na Mkongo Cedric Mongongu, lilitosha kuikwamisha Monaco kuendelea kuipulia japo kwa mbali PSG iliyowaacha kwa pointi 13 wakati ligi ikisaliwa mechi saba kabla ya kukamilishwa kwake.
PSG inaendeelea kuongoza katika msimamo ikiwa na pointi 76, na Monaco ikisaliwa na pointi 63 zote zikiwa zimecheza mechi 31 kila moja.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa jana Sochaux ilishindwa kutambiana na Olympique Marseille kwa kutoka sare ya 1-1, Ajaccio na Toulouse zilitoksa mabao 2-2, huku Montpellier ikabanwa nyumbani kwake na Valenciennes kwa kulazimishwa suluhu kama ilivyokuwa kwa pambano la Nantes na Bordeaux nazo timu za Reims na Lorient pia zilitoka sare ya 1-1.
No comments:
Post a Comment