Mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi |
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point |
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati
akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais
wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas
Mashali kushoto na Japhet Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano
huo
Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba |
Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO |
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo |
Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo |
Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa |
BONDIA Thomas Mashali usiku wa jana amethibitisha kuwa yeye kweli ni Simba Asiyefugika baada ya kumtwanga kwa pointi, Japhet Kaseba na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO Afrika.
Aidha mkali mwingine wa ngumi za kulipwa nchini, Allan Kamote wa Tanga alinyakua ukiwa wa kimataifa wa UBO baada ya kumshinda kwa KO Karage Suba katika michezo iliyochezwa kwenye ukumbi wa PTA-Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Katika pambano la Mashali na Kaseba mabondia walishambuliana kwa zamu, ingawa mshindi alionyesha uhai zaidi katika raudni mbili za mwisho.
Pambano hilo lililokuwa na raundi 10 uzito wa Lighheavy limemaliza ubishi baina ya mabondia hao ambao wiki kadhaa wamekuwa wakitambiana kila mmoja akidai ni zaidi ya mwenzake.
Katika pambano jingine la ubingwa waq kimataifa wa UBO Allan Kamote alimtwanga kwa TKO ya raundi ya tano Suba Karage aliyebadilishiwa dakika za mwisho baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Fadhil Awadh kufariki siku chache akijiandaa na pambano hilo.
Nalo pambano la Fred Sayuni dhidi ya Rajab Mahoja lilishindwa kuendelea baada ya Mahoja kuchanika na kushindwa kuendelea kuwania ubingwa wa Taifa wa PST na hivyo mpinzani wake kupeta.
Pambano hilo lilivunjika katika raundi ya nne, naye Said Mahundfi alimtwanga kwa pointi Jumanne Mohammmed katika pigano la uzito wa bantam na wakongwe Said Chaku Jocky Hamis walitoka sare, huku Issa Nampepeche akimtwanga kwa pointi Zuberi Kitandula na Majis Said kushinda pia kwa pointi dhidi ya Franki Zaga.
Mipambano yote iliandaliwa na promota Ali Mwazoa kutoka Tanga na kusimamiwa na PST chini ya Rais Emmanuel Mlundwa.
No comments:
Post a Comment