Wasiofungika nyumbani, Atletico Madrid wakishangilia moja ya mabao yao jana dhidi ya Espanol |
WAKATI Barcelona wakiendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote atika La Liga, mabingwa watetezi, Atletico
Madrid yenyewe imeendeleza rekodi yake ya kutokufungwa katika uwanja wake wa
nyumbani wa Vincent Calderon katika Ligi hiyo.
Watetezi hao jana walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi Espanol na kufikisha mechi ya 24 katika uwanjani huo bila kuonja kipigo.
Tiago Mendes aliiandikia timu yake bao la uongozi baada
ya kupokea pasi ya Gabi Fernandez na kupiga kichwa mpira ulimshinda
mlinda mlango Kiko Casilla.
Mabingwa hao walifanikiwa kuongeza bao la pili katika kipindi cha
pili kupitia kwa Mario Suarez aliyeupata mpira wa kichwa ulipigwa na
Gimenez kutoka katika eneo la kona.
Ushindi huu una maana kuwa kikosi cha Diego Simeone kinasalia na
nyuma kwa alama tano dhidi ya Barcelona ambao walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elber kwa mabao ya Xavi, Neymar na Lionel Messi lakini wakikamata nafasi ya tano baada ya Sevilla kuopata ushindi ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Elche.
Timu hiyo Atletico itashuka tena dimba lake la nyumbani keshokutwa wakati watakapoikaribisha Malmo ya Sweden katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya
mchezo wa kundi A.
Katika mechi nyingine za La Liga kwa wikiendi Córdoba ililala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Malaga, Deportivo La Coruna ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Valencia, huku Villarreal ikishinda nyumbani 2-0 dhidi ya Almeria na leo kutakuwa na pambano moja kati ya Real Sociedad itakayoikaribisha Getafe.
No comments:
Post a Comment