STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

JKT Ruvu watuma Salamu kwa Azam, yaibanjua Prisons

http://3.bp.blogspot.com/-c532IntfwI0/VB22abeE7MI/AAAAAAAAKPw/70WqIq2oVc0/s1600/1.jpg
Kikosi cha JKT Ruvu
TIMU ya maafande wa JKT Ruvu wamefuata 'nyayo' za ndugu zao Ruvu Shooting kwa kupata ushindi wao wa kwanza katika msimu huu uwanja wa ugenini dhidi ya Prisons-Mbeya na kuonekana kama wanatuma salamu za mapema kwa Azam watakaokutana nao mechi ijayo jijini Dar.
Ruvu Shooting walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda Fc Jumamosi kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara na JKT walipata ushindi wao wa mabao 2-1 Jumapili kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mafaande hao wanaonolewa na kocha Fred Minziro walipata ushindi huo wa kwanza kwao baada ya kuanza msimu kwa sare ya bila kufunga dhidi ya Mbeya City, kisha kupoteza mara mbili mfululizo dhidi ya Kagera Sugar na Yanga.
Mabao ya washindi katika mchezo huo ambao Kocha David Mwamaja ameelekeza lawama zake kwa kipa wake, Benno Kakolanya yalifungwa na Najim Magulu na Jabir Aziz wakati la wenyeji liliwekwa kimiani na Amri Omary.
Kwa ushindi huo JKT Ruvu wameondoka mkiani kwa kufikisha pointi nne kawa Ruvu Shooting, isipokuwa wenyewe JKT wanatangulia mbele kwa sababu ya herufi ili wakifunga kila kitu wakiwa nafasi ya 10.
Mgambo JKT kwa sasa ndiyo wanaokamata mkia wa ligi hiyo kwa kuwa na idadi ndogo ya mabao ya kufungwa licha ya kuwa na pointi tatu sawa na timu za Ndanda na Polisi Morogoro wanaofuatana nao mkiani.
Mechi ijayo kwa JKT Ruvu itakuwa uwanja wa Chamazi jijini Dar kuumana na mabingwa watetezi Azam ambayo ipo kileleni mwa msimamo kwa sasa kwa kubebwa na Herufi licha ya kuwa sawa kwa kila kitu na Mtibwa Sugar.
Mara kadhaa Azam imekuwa ikiiotea JKT Ruvu hali inayofanya pambano lijalo kushindwa kutabirika baada ya JKT Ruvu chini na Minziro kuonekana kuanza kuamka tofauti na ilivyoanza, huku pia kikosi chao msimu huu kikiimarishwa na nyota kadhaa waliowahi kukipiga Simba, Yanga na Azam wenyewe kama Jabir Aziz, Jackson Chove na Haruna Shamte aliyekuwa nahodha msaidizi wa Simba msimu uliopita..

No comments:

Post a Comment