STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Mourinho 'amchongea' Wenger kwa FA

http://www.independent.co.uk/incoming/article9775470.ece/alternates/w620/Wenger-1.jpg
Makocha Jose Mourinho (kulia) na Arsene Wenger (kushoto) katika mzozo wao uliokaribia kuchapana makonde kabla ya kuamuliwa kama inavyoonekana pichani.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini kushindwa kwa Chama cha Soka cha Uingereza-FA kumuadhibu Arsene Wenger kwa kumsukuma kinawaacha katika hatia na kusisitiza kama ingekuwa yeye ndiye aliyefanya tukio hilo wangemuadhibu.
Kufuatia kuchezewa vibaya Alexis Sanchez na Gary Cahill wakati wa mchezo Chelsea walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal mapema mwezi huu, Wenger alivamia eneo la Mourinho kulalamikia faulo hiyo na kumsukuma Mreno huyo wakati akimwambia arejee eneo lake. 
Akihojiwa Mourinho amesema ameshangazwa kwa Wenger kutoadhibiwa na FA kwa kitendo chake hicho kwani anaamini ingekuwa yeye lazima angechukuliwa hatua. 
Wenger mwenyewe tayari aliomba radhi kwa tukio hilo na kudai kuwa alichokuwa akilalamikia ni kuchezewa faulo mchezaji wake na sio vinginevyo.
Makocha hao wawili wamekuwa kwenye 'bifu' kwa muda mrefu hasa zinapokutana timu zao na wakati mwingine kupigana vijembe hata kama hawana mchezo wowote.

No comments:

Post a Comment