STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Polisi yaua wanayedai kuwa ni 'Mlipuaji' mabomu ya Arusha

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Jeshi la polisi mkoani Arusha limemuua kwa kumpiga risasi mtu wanayedai kuwa ni mtuhumiwa namba moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko na mmwagiajie tindikali viongozi wa kidini.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo aliuwawa kwa risasi wakati akijaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi akiwa njiani kuelekea Kondoa, Dodoma kuonyesha bomu alilokuwa amelificha maeneo hayo.
Taarifa zinamtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Hassan Omar na Polisi wamedai ndiye aliyekuwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini Arusha, akiwa amewahi kukiri mwenyewe kuhusiana na matukio hayo.

No comments:

Post a Comment