SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
wamekutana mwishoni mwa wiki na kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha
maendeleo ya mchezo huo nchini.
Mkutano
huo uliofanyika Dar es Salaam uliongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi
na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na
wanyeviti wa klabu za VPL.
Masuala
yaliyozungumzwa ni leseni za klabu (club licensing), maboresho ya Taifa
Stars, Kanuni za Ligi Kuu, Kombe la FA (Shirikisho) na mchango wa klabu
hizo katika kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana.
Uwasilishaji
katika mkutano huo kuhusu maboresho ya Taifa Stars ulifanywa na Kocha
Mkuu wa timu hiyo Mart Nooij wakati leseni kwa klabu ulifanywa na
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura.
Kuhusu
Kombe la FA, klabu zilifahamishwa kuwa mazungumzo kati ya TFF na
mdhamini yanaendelea, ambapo zilikaribisha wazo hilo kwa vile michuano
hiyo itatoa fursa kwa timu zao kucheza mechi nyingi za mashindano, hivyo
kutoa nafasi ya kucheza kwa wachezaji wengi zaidi.
Bingwa wa michuano ya FA ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Rais
Malinzi aliziomba klabu kukutana na kuwasilisha mapendekezo yao ya jinsi
ya kuchangia/kuboresha maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana,
kuboresha Kanuni za Ligi Kuu na kuboresha Kanuni za Bodi ya Ligi ili
yaweze kufanyiwa kazi
No comments:
Post a Comment