Mada Maugo aliyekung'utwa Ko ya raundi ya 5 |
Karama Nyilawila aliyepigwa KO ya raundi ya 6 |
Ramadhani Shauri aliyepigwa KO ya raundi ya kwanza |
Mabondia hao walikumbana na vipigo hivyo katika michezo yao ya kimataifa ya kuwania mataji ya Dunia ya UBO na WBC iliyochezwa siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Express, mjini Rostov-na-Donu nchini Russia.
Bondia Mada Maugo aliyekuwa akiwania ubingwa wa Dunia wa UBO katika uzani wa Middle dhidi ya Aliklych Kanbolatov wa Russia na kupigwa kwa KO ya raundi ya tano kati ya 12 alizokuwa akipigane.
Maugo alipigwa katika pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Express, katika mji wa Rostov-na-Donu, kuwania taji hilo lililokuwa wazi, ukumbi ambao pia ulishuhudia wenzake wawili wakipigwa.
Bondia Ramadhani Shauri aliyekuwa akiwania ubingwa wa Mabara Dunia wa WBC kwa Vijana alipigwa na Viskhan Murzabekov kwa KO ya raundi ya kwanza kati ya 12 za pambano hilo la uzani wa Welter.
Kama ilivyokuwa kwa watanzania hao wawili, pia Karama Nyilawila alikumbana na kipigo cha KO ya raundi ya sita ya pambano la raundi 12 dhidi ya Varazdat Chernikov.
Bingwa huyo wa zamani wa WBF alikuwa akiwania taji la Mabara la UBO la uzito wa Super Middle lililokuwa pia wazi na kuendeleza rekodi za mabondia wa Tanzania kushindwa kutamba nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment