Simba na Yanga zilipokuatana zenyewe siku ya Jumamosi na kushindwa kutambiana uwanja wa Taifa |
Makipa wa Simba na Yanga, Peter Manyika na Deo Munishi 'Dida' wakipongezana |
Kazi tumeimaliza kati yetu sasa tuangalie mechi zetu zijazo, makocha Marcio Maximo na Patrick Phiri wakisalimiana |
Yanga wanaokamata nafasi ya nne kwa sasa katika msimamo itakuwa na mechi ngumu mbili mfululizo kuanzia Jumamosi hii kwa kuumana na Stand United mjini Shinyanga kabla ya kuvaana tena na Kagera Sugar ambao wamekuwa wakiwatesa mara kadhaa wakiwafuata uwanja wa Kaitaba.
Iwapo Yanga itashinda mechi hizo za ugenini au kumaliza salama bila kupoteza itakuwa imevuka kikwazo cha mbio zake za ubingwa msimu huu.
Stand United licha ya kuwa ni timu ngeni katika ligi baada ya kupata msimu huu, lakini haitabiriki kwani iliwabania Simba uwanja wa Taifa kwa kutoka nao sare ya 1-1, kadhalika Kagera Sugar haitabiriki kabisa.
Wakati Yanga wakiwa na kibarua hicho, watani zao wenyewe wataanza wiki hii kwa kucheza ugenini kama Yanga kwa kuwafuata Prisons-Mbeya ambayo imekuwa ikisumbua kwenye uwanja wa Sokoine.
Baada ya kibarua hicho Simba itasafiri hadi Morogoro kuwafuata Mtibwa Sugar ambao wamekuwa wakiwajeruhi kwenye uwanja wa Jamhuri kila wakikutana.
Simba yenye pointi nne kama Prisons haijaonja ushindi katika ligi ya msimu huu, hivyo watakuwa na kazi ngumu kuhakikisha wanavunja mwiko wa kucheza mechi 10 za ligi tangu msimu uliopita bila kushinda.
Hata hivyo tayari benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo ya Msimbazi imekuwa ikisisitiza kuwa mambo yanaelekea kutengemaa na kwamba mashabiki wao watarajie faraja ya kuonja ushindi katika mechi zijazo
Baada ya mechi za mwishoni mwa wiki MICHARAZO inakuletea msimamo kamili wa sasa wa ligi hiyo sambamba na mechi zitakazofuata katika ligi hiyo inayozidi kuchanja mbuga.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
P W D L F A GD Pts
01. Azam 04 03 01 00 06 01 +5 10
02. Mtibwa Sugar 04 03 01 00 06 01 +5 10
03.Coastal Union 04 02 01 01 06 04 02 07
04.Yanga 04 02 01 01 04 04 00 07
05. Kagera Sugar 04 01 02 01 03 02 +1 05
06. Mbeya City 04 01 02 01 01 01 00 05
07.Stand Utd 04 01 02 01 03 05 -2 05
08.Prisons 04 01 01 02 04 04 00 04
09.Simba 04 00 04 00 04 04 00 04
10. JKT Ruvu 04 01 01 02 03 05 -2 04
11. Ruvu Shooting 04 01 01 02 03 05 -2 04
12. Ndanda Fc 04 01 00 03 07 09 -2 03
13. Polisi Moro 04 00 03 01 03 05 -2 03
14. Mgambo JKT 04 01 00 03 01 04 -3 03
RATIBA
Okt 25, 2004
Stand United v Yanga (Kambarage-Shinyanga)
Azam v JKT Ruvu (Chamazi-Dar es Salaam)
Prisons-Mbeya vs Simba (Sokoine-Mbeya)
Ndanda v Mgambo JKT (Nangwanda Sijaona-Mtwara)
Kagera Sugar v Coastal Union (Kaitaba-Bukoba)
Ruvu Shooting v Polisi Moro (Mabatini-Mlandizi)
Okt 26, 2014
Mbeya City v Mtibwa Sugar (Sokoine-Mbeya)
Nov 1, 2014
Kagera Sugar v Yanga (Kaitaba-Bukoba)
Coastal Union v Ruvu Shooting (Mkwakwani-Tanga)
JKT Ruvu vs Polisi Moro (Chamazi-Dar es Salaam)
Ndanda Fc Azam (Nangwanda Sijaona-Mtwara)
Stand Utd v Prisons-Mbeya (Kambarage-Shinyanga)
Mtibwa Sugar v Simba (Jamhuri-Morogoro)
Nov 2, 2014
Mgambo JKT vs Mbeya City (Mkwakwani-Tanga)
No comments:
Post a Comment