STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Ndanda Fc yakwanza kutimua kocha Ligi KUU 2014-2015

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/KITAMBI-FILEminimizer.jpg
Kocha Dennis Kitambi aliyetimuliwa kazi Ndanda
http://1.bp.blogspot.com/-fn1xOo2rNkk/TniMLQ56LTI/AAAAAAAAA1I/BzQhPuvhyZI/s1600/PICT0123.JPG
Dennis Kitambo katika moja ya mafunzo ya taaluma yake ya ukocha
WAKATI Ligi Kuu ikizidi kuchanja mbuga, klabu ya iliyopanda ligi hiyo, Ndanda ya Mtwara imekuwa klabu ya kwanza msimu huu kumtimua kocha wake baada ya kusitisha mkataba wake na Dennis Kitambi aliyeipandisha baada ya timu hiyo kupokea vipigo vitatu mfululizo.
Kitambi, aliyeitoa timu hiyo katika madaraja ya chini hadi kufikia kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza, alikumbana na kadhia hiyo baada ya Ndanda kupokea kipigoi cha mabao 3-1 nyumbani mbele ya Ruvu Shooting huku ikiwa imepoteza mechi mbili nyingine za nyuma dhidi ya Mtibwa Sugar waliowafunga mabao 3-1 na Cpastal Union waliowanyoosha mabao 2-1 katika mechi za ugenini.
Timu hiyo ilianza ligi kwa kishindo kwa kuilaza wageni wenzsao wa ligi hiyo Stand United kwa mabao 4-1 kabla ya kubainika kumbe ilikuwa nguvu ya soda kwa kugawa pointi hata nyumbani, huku wakielekea kuvaana na Azam katika mechi ijayo ambayo inatarajiwa kuwa kali na yenye upinzani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, uongozi umeona ni vema kusitisha mkataba na kocha huyo licha ya kumshukuru kwa mchango wake na wanafanya mipango ya kusaka kocha mwingine ambaye ataipeleka mbali zaidi klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment