STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Juve yang'ang'aniwa, AC Milan ikishinda ugenini Italia

http://forzaitalianfootball.com/wp-content/uploads/2014/10/Honda-Hellas-Verona-v-AC-Milan.jpg
Kaisuke Honda kipongeza na wachezaji wenzake wa Ac MIlan baada ya kuifungia timu yake mabao mawili jana
http://hoofoot.com/images/pics/5320.jpg
http://images.cdn.fourfourtwo.com/sites/fourfourtwo.com/files/styles/main-image-landscape-small/public/paulpogba_vk8n8jqtapnz173kuqh1is5x3.jpg?itok=9INmTWtt
Paul Pogba aliyeifungia Juventus bao lililowapa pointi moja ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Sassuolo
MABINGWA watetezi wa Serie A, Juventus iking'ang'aniwa ugenini na Sassuolo kwa kulazimishwa sare ya 1-1, AC Milan imeendeleza libeneke kwa kupata ushindi wa pili mfululizo katika ligi hiyo wakiwa ugenini na kuwapandisha hadi kwenye nafasi ya Nne.
Milan wanaonolewa na Phillip Inzaghi 'Pippo' ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hellas Verona na kuwafanya wafikishe pointi 14, tano pungufu na ilizonazo Juventus iliyolazimishwa sare  siku ya Jumamosi.
Mabao ya washindi katika mchezo huo yalifungwa na Raphael Marques aliyejifunga katika dakika ya 21 wakati akiwa katika harakati za kuokoa shambulizi la Milan, kabla ya Kaisuke Honda kufunga mabao mawili dakika ya 27 na 56 na wenyeji kupata la kufutia machozi dakika tatu kabla ya pambano hilo kumalizika kupoita kwa Lopez.
Katika mechi nyingine za Ligi ya Serie A kwa siku ya jana Fiorentina ilikubali kukung'utwa nyumbani mabao 2-0 na Lazio, Atalanta ikatakata nyumbani kwa kushinda kiduchu kwa bao 1-0 dhidi ya Parma, huku Cagliari ililazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Sampdoria.
Palermo wakang'ara nyumbani kwa kuifumua Cesena kwa mabao 2-1, huku Udinese ikilala ugenini mbele ya wenyeji wao Torino kwa bao 1-0 na Inter Milan iking'ang'aniwa nyumbani kwa sare ya 2-2 na Napoli.
Ligi hiyo itaendelea tena kwa mchezo mmoja kati ya Genoa itakayoikaribisha Empoli.

No comments:

Post a Comment