STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Mchezaji India afa akibinuka samasoti kushangilia bao

Hapa akiwa bado katika uangalizi wa madaktari hospitali
Hapa wakati akipiga samasoti yaani sarakasi

Hapa ni wakati wa kuugwa mwili wa marehemu
MCHEZAJI wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga 'samasoti' uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kwa timu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jeraha la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : 
"imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. "
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''

No comments:

Post a Comment