STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 20, 2014

Gareth Bale aiweka Real Madrid njia panda Ulaya

http://cf.c.ooyala.com/1jcHI5bzoAOzj81t6e3WBQ9IKBHMte3P/promo230718654
Gareth Bale
KLABU ya Real Madrid bado haina hakika kama nyota wake kutola Wales, Gareth Bale kama atacheza katika mechi dhidi ya Liverpool katika Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumatano.
Bale, 25 anauguza jeraha la misuli ya paja, jeraha lililomfanya ashindwe kushiriki mechi ya La Liga dhidi ya Levante juzi Jumamosi ambapo timu yake ilishinda mabao 5-0, licha ya kuwa benchi kama mchezaji wa akiba.
Taarifa ya klabu hiyo haikufafanua muda ambao Bale atakuwa nje ya uwanja, hata hivyo walisema atazidi kukaguliwa jinsi anavyopata nafuu.
Baada ya mechi yao ya Kundi B itakayochezewa kwenye uwanja wa Anfield, Real Madrid inatarajiwa kukabana koo na mahasimu wao wa jadi Barcelona katika ligi ya El Clasico hapo jumamosi.
Bale aliichezea timu yake ya taifa ya Wales kwa vipindi vyote viwili dhidi ya Bosnia Hercegovina Oktoba 10 kisha akaichezea tena dhidi ya Cyprus siku tatu zilizofuata katika michuano ya kufuzu kwa Fainali za Uero 2016.
Bale ambaye alihamia Real Madrid kutoka Tottenham mwaka uliopita kwa kitita cha pauni milioni 85.3, ameichezea real Madrid mechi 12 huku akiwa amefunga mabao matano.

No comments:

Post a Comment