Vijana hao wa Brendan Rodgers, walianza kutangulia kufunga baada ya beki wa QPR Richard Dunne kujifunga katika dakika ya 67 kabla ya mtokea benchi Vargas kuisawazishia wenyeji katika dakika ya 87 na kuongeza la pili dakika 90.
Hata hivyo Coutinho wa Liverpool aliiandika timu yake bao la pili na Steven Caulker akajifunga kwenye dakika za nyongeza na kuwapa LIverpool ushindi huo muhimu.
Katika pambano jingine la ligi hiyo timu ya Stoke City ikiwa nyumbani iliinyoosha Swansea City kwa kuilaza mabao 2-1. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo Jumatatu wakati Manchester United wastakapokuwa ugenini kuwakabiliWest Bromwich Albion kusaka pointi tatu zitakazowaingiza kwenye Nne Bora kwa mara ya kwanza msimu huu.
No comments:
Post a Comment