STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 10, 2013

Washindi wa tuzo za Kili Music Awards 2013 hawa hapa



Add caption









WIMBO BORA WA RNB; RAMA DEE ft MAPACHA-KUWA NA SUBIRA

KIKUNDI BORA CHA TAARABU-JAHAZI MODERN TAARAB

MTUNZI BORA WA TAARABU-THABIT ABDUL

WIMBO BORA WA TAARABU;KHADIJA KOPA-MJINI CHUO KIKUU

MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA KWA TAARABU-ENRICO


MSANII BORA WA KIKE -TAARBU; ISHA MASHAUZI

MSANII BORA WA KIUME -TAARABU; MZEE YUSUPH

WIMBO WENYE VIONJO VYA ASILI-MRISHO MPOTO ft DITTO-CHOCHEENI KUNI

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI BONGO FLAVA-BEN POL

MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA-MUZIKI WA KIZAZI KIPYA; MAN WALTER

MSANII BORA WA KIUME BONGO FLAVA-DIAMOND
MSANII BORA WA KIKE BONGO FLAVA-RECHO

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI HIP HOP-KALA JEREMIAH

WIMBO BORA WA BONGO POP;OMMY DIMPOZ-ME AND YOU

MSANII BORA ANAYECHIPUKIA-ALLY NIPISHE

MSANII BORA WA KIUME-DIAMOND

KIKUNDI BORA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA-JAMBO SQUAD

MTAYARISHAJI CHIPUKIZI WA MWAKA-MENSEN SELECTA

WIMBO BORA WA BENDI;MASHUJAA-RISASI KIDOLE

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI -BENDI; CHARLS BABA

MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA-BENDI ;AMOROSSO

MSANII BORA WA KIKE-BENDI ;LUIZA MBUTU

MSANII BORA WA KIUME-BENDI ;CHARLS BABA

BENDI BORA YA MWAKA-MASHUJAA BAND

WIMBO BORA WA ZOUK; AMINI -NI WEWE

WIMBO BORA WA REGGAE;WARRIORS FROM THE EAST-KILIMANJARO

WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL; DABO-PREDATOR

MSANII BORA WA HIP HOP-KALA JEREMIAH

WIMBO BORA WA HIP HOP; NAY WA MITEGO-NASEMA NAO

WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI;JOSE CHAMELEONE-VALUVALU

WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA;OMMY DIMPOZ ft VANESSA-ME AND YOU

WIMBO BORA WA MWAKA; KALA JEREMIAH-DEAR GOD

VIDEO BORA YA MWAKA;OMMY DIMPOZ-BAADAE

HALL OF FAME-KILIMANJARO BAND WANA NJENJE

HALL OF FAME-SALUM ABDALLAH YAZIDU

MSANII BORA WA KIKE-LADY JAY DEE



KASEBA ALIVYOMSAMBARATISHA SIMWANZA WA MALAWI

Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana kazi na
JOSEPHER NJELEKELA(KAMANDA WA KAMANDA) wakati wa mpambano wao Maokola alishinda kwa KO ya raundi ya tatu
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Juma Fundi akioneshana umwamba na Moro Best wakati wa mpambano huo

Bondia Juma Fundi akioneshana umwamba na Moro Best wakati wa mpambano huo
Juma fundi alishinda kwa KO raundi ya sita

Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Rasco Simwanza kutoka Malawi kushoto akipambana na Japhet Kaseba wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Kimataifa wa PST kaseba alishinda raundi ya tano

Bondia Japhet Kaseba akiwa amevishwa mkanda wake wa kimataifa wa PST

Bondia Kaseba akishangilia ushindi zaidi tembelea www.superdboxingcoach.blogspot.com

Watanzania wang'ara katika mbio nchini Kenya

KATIKA kuhakikisha riadha nchini Tanzania inafuta uteja kwa wakimbiaji
wake kwa wafukuza upepo wa Kenya, Klabu ya Holili (HYAC) ya Mkoani
Kilimanjaro imedhihirisha hilo katika Taveta Athletics Championship
kwa kuwabwaga Wakenya katika mbio za meta 5000, 1500, 800 na 100.

Michuano hiyo ya Taveta imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kaunti ya
Taita-Taveta katika Mkoa wa Pwani nchini Kenya katika wilaya ya Taveta
kwa kuwakutanisha wanariadha wa nchini Kenya huku Holili Youth
Athletics Club ikialikwa kutoka nchini Tanzania.

Katika Mbio za meta 5,000 alikuwa ni Baraka Williams aliyekimbia kwa
dakika 14:45:22 nafasi ya pili ikishikwa na Mtanzania mwingine
Abubakar  Joel aliyekimbia kwa muda wa 16:00:00  na nafasi ya tatu
ikashikwa na Mkenya Kivoko Makao ambaye alikimbia kwa muda wa
16:34:00.

Wambura Lameck, Mtanzania kutoka katika klabu ya Riadha kwa vijana
(HYAC) alionyesha uwezo katika mbio za meta 100 na 800 kwa wanaume;
katika mbio za meta 100 Wambura alikimbia kwa muda wa sekunde 12:67
akiwatupa Wakenya Walter Kamujalo (13:12), Emmanuel Paulo (13:70) na
Joseph Daudi (14:20).

Mbio za mita 800 Wambura Lameck alikimbikia kwa muda wa dakika 2:02:16
akimwacha Mkenya Ropya Nyingi ambaye alichukua muda wa dakika 2:04::14
na nafasi ya Tatu ikishikwa na Mtanzania kutoka HYAC Paulo Jackson
aliyekimbia kwa muda wa dakika 2:05:98, Wakenya wengine Joseph Daudi
(3:00:00) na Philip Matheka (3:04) walisshika nafasi mbili za mwisho.

Pia Watanzania waliwaonyesha kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta
1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC alipowakimbiza na kuongoza baada
ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77 akifuatiwa na Mkenya Vicent
Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda wa dakika 4:16:85
nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC Paulo
Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick
akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.

Kwa upande wa wanawake Watanzania Furaha Sambeke na Pendo Pamba
walifanya kweli katika meta 800 kwa kushika nafasi mbili za juu.

Furaha Sambeke anayenolewa na Klabu ya Holili Youth Athletics
alikimbia kwa muda wa dakika 2:30:00 na Pendo Pamba akimaliza kwa
dakika 3:10, nafasi ya tatu ilishikwa na Mkenya Emily Wamboi na ya nne
ikishikwa na Mkenya mwingine Cecily Kimale ambao wote walikimbia kwa
kuda wa dakika 3:22:00 na 4:12:00.

Taveta Athletics Championship imefanyika ikiwa na makusudi ya
kutengeneza Timu ya Riadha ya Taifa la Kenya ambako mchujo rasmi
utafanyika Mjini Mombasa kwa watanzania walioshinda katika mbio hizo
nao watakuwemo katika kinyang’anyiro hicho kwa ajili ya kupata uzoefu
zaidi kutokana na ukweli kwamba taifa la Kenya limekuwa bora katika
riadha barani Afrika.

Mwandishi: Johnsona Jabir, Moshi-Kilimanjaro

Saturday, June 8, 2013

Wajasiriamali wanawake wazidi kupiga hatua Tanzania


EBU angalia matangazo ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa kike wa Tanzania...unadhani wakiwezesha zaidi si watafika mbali zaidi?!

LICHA YA HUJUMA, STARS YAAPA KUIFANYIZIA MOROCCO

Straika wa Taifa Stars, John Bocco (wa pili kulia) akimiliki mpira huku akichungwa na Athuumani Idd 'Chuji' nyuma yake wakati wa mazoezi yao kuelekea mechi yao ya leo usiku ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco mjini Marrakech.

Beki wa Stars, Erasto Nyoni (kulia) akikokota ngoma huku akichungwa na Frank Domayo huku Kelvin Yondani ( wa tatu kulia) na Mrisho Ngasa (kushoto) wakishuhudia wakati wa mazoezi yao kuelekea mechi yao ya leo usiku ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco mjini Marrakech.

Straika wa Stars, Mbwana Samata (kushoto)akimiliki mpira wakati wa mazoezi yao kuelekea mechi yao ya leo usiku ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco mjini Marrakech.

Ulimwengu (kushoto), Aggrey Morris, Mwinyi Kazimoto wakiwania mpira  wakati wa mazoezi yao kuelekea mechi yao ya leo usiku ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco mjini Marrakech.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku wa kuamkia leo ilifanyiwa kilichoonekana kuwa hujuma baada ya kufanyiwa vurugu na kuzimiwa taa ishindwe kufanya mazoezi kwenye uwanja wa utakaotumika kwa mechi ya leo, siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya wenyeji wao Morocco ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014.

Sheria za FIFA zinasema timu mgeni, itapewa fursa ya kufanya mazoezi katika uwanja utakaotumika kwa mechi dhidi ya wenyeji katika muda ambao mechi itachezwa, lakini jana msafara wa Stars ulipofika Uwanja wa Marakech ulizuiwa kuingia ndani na askari wa uwanjani hapo.

Juhudi za kocha wa Stars, Kim Poulsen kuwaelewesha askari wa uwanja huo sheria ili wairuhusu timu kuingia uwanjani hazikuzaa matunda na ikabidi viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waingilie kati, nao pia wakachemsha.

Ikawadia zamu ya viongozi wa Kamati ya Ushindi ya Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager, ambao nao walichemsha, ndipo baadhi wa Watanzania waishio hapa na wachache waliosafiri kutoka Dar es Salaam walipoongeza nguvu.

Walikwenda kufungua geti kwa nguvu, wakawaweka kando askari waliokuwa wanawazuia na kuiingiza timu uwanjani kufanya mazoezi.

Hata hivyo, Stars ilipofika uwanjani ililazimika kusubiri tena, kwani wenyeji Simba wa Atlas walikuwa wakiendelea na mazoezi.

Baada ya nusu saa, Morocco walimaliza awamu yao na Stars wakaanza kupasha misuli moto. Hata hivyo, baada ya dakika 34, taa za uwanja huo zilizimwa na uwanjani kuwa giza totoro, lakini viongozi wa TFF wakaenda kuomba, zikawashwa na timu ikafanya mazoezi kwa dakika 10 zaidi.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla aliyekuwapo wakati wa vurumai zote hizo, alisikitishwa mno na kitendo hicho akisema si cha kiungwana na si cha kiunamichezo.

Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani alisema Morocco walikuja kucheza Dar es Salaam walipokewa vizuri na wakahudumiwa vizuri hadi wanaondoka, ajabu leo wanaifanyia ‘unyama’ Tanzania.

Mkuu wa Msafara wa Stars hapa, Crescentius John Magori alisema watapeleka malalamiko FIFA, waandaji wa michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na kwa kuwa ushahidi upo, anaamini Morocco watachukuliwa hatua.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alishauri Stars icheze chini ya angalizo kwa kuwasilisha barua FIFA mapema ili wakae wanajua kuhusu hali halisi Morocco.

Kwa ujumla kilichotokea leo kimewatia woga Watanzania wengi waliopo hapa kuelekea mchezo wa leo, ambao Stars inahitaji ushindi ili kujiimarisha katika mbio za kuelekea Brazil 2014.

Hata ulinzi wa msafara wa Stars kutoka hotelini hadi uwanjani hakuwa wa kutosha na ilishuhuidiwa mara kadhaa ukiingiliwa na magari mengine barabarani wakati timu ikienda uwanjani kwa mazoezi.

Wenyeji nchini Morocco wanasema inapowadia mechi, huwa wanaogopa kwa sababu mara nyingi hutokea vurugu ya damu kumwagika.

Kwa ujumla Stars inaingia katika mchezo wa leo katika hali ya wasiwasi na woga mkubwa.

Stars itashuka dimbani saa 3:00 usiku leo kwa saa za hapa sawa na saa 5:00 za Tanzania kucheza na Morocco.

Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo.

Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao.

Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri.

Waziri Makamba avisuta vyama vya upinzani


Naibu Waziri, Januari Makamba
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema dhamira ya kuwepo kwa vyama vingi bado haijafikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kukosa vyama na viongozi  wenye dira kwa Taifa.
Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es Salaam.
Makamba ambaye pia ni Mlezi wa Vyuo Vikuu Tanzania alisema  vyama hivyo vimekuwa vikijikita katika kulalamika bila kuonyesha dira na mwelekeo tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya fujo ambazo zinakwamisha jitihada za serikali.
Makamba alisema Serikali inafanya kazi kutokana na mipango yake ambayo imejiwekea yenyewe hivyo inaamini kuwa itafikia malengo yake bila kusukumwa na mtu.
“Kwa  kweli najuta kwanini tuliruhusu uwepo wa vyama vingi hapa nchini kwani lengo letu lilikuwa ni kudumisha demokrasia kitu ambacho kimekuwa kinyume kwani vyama na  viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na dhima ya lengo husika,” alisema
Naibu Waziri alisema CCM ni chama ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa hivyo wao wanaamini kuwa heshima hiyo itaendelea kuwepo milele kwa milele.
Alisema vijana wa CCM wahakikishe kuwa wanakisaidia chama na  nchi kwa ujumla ili nchi isije kuchukuliwa na vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa na kuipeleka nchi kuzimu.
Aidha Mlezi huyo aliwataka vijana  hao wanaomaliza kujiamini na kuthubutu kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza ili waweze kupata urahisi wa kushiriki katika chama na serikali kwani ni wajibu wao kulitumikia Taifa.
Makamba alisema vijana wanapaswa kushiriki katika harakati za kisiasa kwani hayupo mtu amnbaye atapata jambo bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana na dhana ya kutafutiwa kazi kama wengi wanaofikiri.
Aliwataka wingi wao uwe ni sehemu muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la Tanzania ijao ikiwa ni kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuondokana na dhana kuwa mwenye uwezo wa fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi huyo alisema dhana ya fedha katika kutafuta uongozi  ipo kwa baadhi ya watu kutokana na tabia ya mtu mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia kama kigezo.
Naibu Waziri aliwataka vijana wa CCM kuondoa uoga katika maamuzi ambayo yanahusu maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla iwapo sifa za uongozi unazo.
Makamba aliwaambia vijana kutambua kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na kuachana na tabia ya kulalamika kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee jambo ambalo wanalitengeneza wenyewe.
 
Aidha aliwataka wasomi kutafuta maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu Nyerere kwani yana msingi mkubwa katika kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu nchi yao na uongozi kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti  Vyuo Vikuu Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari Asenga alisema katika mahafal;i hayo wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28 vya mkoa wa Dar es Salaam walishiriki katika sherehe hiyo.
Asenga alisema huo ni uataratibu ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa shirikisho hilo lengo likiwa ni kuwatambua na kuwapatia vyeti vya utambulisho wao ndani ya CCM.
Alitaja vyuo ambavyo vilishiriki ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT, TSJ na vingine vingi.
Kwa upande wa msoma risala kwa niaba ya wahitimu Innocent Nsena  alisema wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana na  changamoto za jamii pamoja na vyama vya upinzani hapa nchini.
Aidha alisema wanavyuo wanapendekeza maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo wanaomba nchi ya Tanzania kutokubali kuwa na serikali ya shirikisho kwani uwezo wa nchi bado ni mdogo kuendesha nchi ambayo bado ni change kuichumi.
Pia wanapendekeza upatikanaji mpya wa kupata mgombea urais ili kuondoa mpasuko ambao unatokea mara kwa mara baada ya uchaguzi kufanyika.
Alisema katika mazingira yoyote yale Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana na mazingira mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni vyema wakatumia mfumo wa kujaza dodoso ili wana CCM wapendekeze Rais wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.

Huyu ndiye Miss Sinza 2013 arithi taji la Miss Tanzania 2012



Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte Alfred

MREMBO Prisca Element jana usiku alifanikiwa kumvua taji la kwanza Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Sinza katika mchuano mkali uliofanyika ukumbi wa Meeda, uliopo Sinza Mori, Dar es Salaam.
Brigitte mbali na kushikilia taji la Redd’s Miss Tanzania ndiye pia aliyekuwa mrembo wa Redd’s Miss Tanzania, hivyo kuvuliwa taji hilo la kwanza ni kudhihirisha kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi wake kimeshika kasi.
Katika shindano hilo lililokuwa kali na la kuvutia, huku burudani ikinogeshwa na kundi la African Stars ‘Twanga Pepeta’, nafasi ya pili ilichukuliwa na Happynes Maira na ile ya tatu akaitwaa Sarah Paul.
Warembo wengine wawili waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Nicole Michael na Nasra Hassan, ambao walitoa upinzani mkali katika shindano hilo lililokuwa likifuatiliwa kwa karibu na watu wengi.
Akizungumza mara baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo, Prisca alisema ana uhakika mkubwa wa kufuata nyayo za Brigitte na kudai atahakikisha anaipigania Sinza kwa nguvu zake zote ili iweze kufanya vyema katika Redd’s Miss Tanzania.
Brigitte alipoulizwa kuhusu shindano hilo na kuvuliwa kwake taji, alisema anaamini kwa dhati mrembo aliyechaguliwa atahakikisha kitongoji cha Sinza kinaendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo.
“Kikubwa zaidi ni kujiamini na kufuata maelekezo unayopewa, lakini mrembo wetu naamini ana sifa zote zinazostahili na ni matumaini yangu atasonga mbele zaidi katika hatua inayofuata,” alisema.
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Mfanyabiashara mbaroni kwa kulawiti wanafunzi


MFANYABIASHARA maarufu mjini Morogoro, Mohamed Mauji, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaingilia kinyume na maumbile wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Mwere B.

Tukio hilo linadaiwa kutokea wiki iliyopita kwenye eneo la mazingira ya ofisi ya mfanyabiashara huyo anayeuza vinywaji laini kwa jumla.

Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro, Sadick Tindwa, alisema kuwa inadaiwa kutokea Mei 31 na kuripotiwa katika kituo hicho Juni 3 na wazazi wa watoto hao.

Alisema kuwa wazazi hao walieleza kuwa waliwabaini watoto wao baada ya kupewa taarifa na walimu wa shule hiyo kuwa watoto hao wamekuwa wakija shuleni na fedha nyingi za matumizi pamoja na vitu mbalimbali.

Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Morogoro alisema kuwa baada ya wazazi hao kupewa taarifa hizo, waliwauliza watoto hao na kueleza kuwa wamekuwa wakipewa na mtu waliyemtaja kwa jina la mzungu na kuwafanyia vitendo hivyo.

Alisema kuwa wazazi hao walipowapekua watoto wao waliwakuta wana michubuko katika sehemu za kutolea haja kubwa na kuamua kulifikisha suala hilo kwa afisa mtendaji wa kata Kingo jirani na mfanyabiashara huyo.

Mkuu huyo wa Polisi Wilaya ya Morogoro alisema kuwa afisa huyo mtendaji wa kata ya Kingo aliamuru suala hilo lifikishwe kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kufanyiwa upelelezi.

Alisema kuwa baada ya kulifikisha , jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi ikiwa pamoja na watoto hao kupelekwa hospitali ya rufaa ya Morogoro kuchunguzwa afya zao.

Hata hivyo, alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na tuhuma hizo, mfanyabiashara huyo alikiri kuwafahamu wanafunzi hao ambao wamekuwa wakipita nje ya ofisi yake na kuomba pesa ya soda na yeye aliwahi kuwapatia kiasi cha sh 500 lakini hajawahi kuwafanyia kitendo hicho.

Moyes, Wenger katika vita ya kumwania Fabregas

2013 cesc fabregas barcelona
KLABU ya Manchester United imeingia vitani dhidi ya mahasimu wao Arsenal baada ya kocha wake David Moyes kuweka bayana kwamba ipo tayari kumnyakua kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas anayewindwa pia kurejeshwa Emirates na klabu yake ya zamani.
Moyes, amenukulia akisema angependa kumsajili kiungo wa zamani wa Gunners ambaye hata hivuo majuzi aliweka bayana nia yake ya kuendelea kusalia kwa mabingwa wa Hispania, Barcelona.
Kiungo alikaririwa akisema angependa kusalia Nou Camp Nou ili kupigania namba yake licha ya kusajiliwa Mbrazili mwenye thamani ya Paundi Mil 50, Neymer.
Hata hivyo Moyes amesema atafanya kila njia kumnyakua mshindi huyo wa Kombe la Dunia aliyenyakua na timu yake ya taifa katika fainali zilizopita za 2010 ili kujenga kikosi chake.
Mipango ya Fabregas kurejeshwa Ligi Kuu ya England ilianza kitambo hata kabla Moyes kuchukua nafasi ya Ferguson mwzi uliopita.
Mabingwa hao wanamhitaji kiungo huyo baada ya Paul Scholes kustaafu na Michal Carrick kuondoka huku Tom Cleverley akibebeshwa majukumu yote.
Licha ya viungo toka Brazil, Anderson na Mjapan Shinji Kagawa kufanya vyema Old Trafford, lakini wanaelezwa sio wa daraja la Fabregas na ndiyo maana Moyes anamtolea macho akichuana na Wenger aliyetangaza kutaka kumrejesha nyota wake huyo wa zamani aliyemuuza mwaka uliopita.