STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 1, 2013

Cheka, Mashali, King Class watoa vipigo kwa wapinzani wake

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Simba Watunduru wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee. King Class alishinda kwa pointi.
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Simba Watunduru wakati wa mpambano wao uliofanyika Ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee. King Class alishinda kwa pointi.
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Simba Watunduru wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee. King Class alishinda kwa pointi.
Bondia Chipaki Chipindi  kushoto akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Alphonce Mchumiatumbo katika mpambano wao Mchumiatumbo alishinda kwa TKO
Bondia Deo Njiku akioneshana kazi na Alain Kamote wakati wa mpambano wao wa utangulizi Kamote alishinda kwa Point
Bondia Mada Maugo akijikakamua kumpiga konde Thomasi Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika jana wa kugombania Ubingwa wa WBF-Afrika. Mashali alishinda kwa pointi mpambano huo.
Thomasi Mashali kushoto na Maa Maugo wakioneshana umwamba
Bondia Francis Cheka kushoto akioneshana umwamba na Phil Williams wa Marekani wakati wa kugombania  ubingwa wa WBF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Cheka alishinda kwa pointi.
Bondia Francis Cheka kushoto akioneshana umwamba na Phil Williams wa Marekani wakati wa kugombania  ubingwa wa WBF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Cheka alishinda kwa pointi.

Miss Utalii Tanzania 2013 kwenda Equatorial Guinea Sept 28

Top 3 ,Miss Tourism Tanzania 2012/13
nchini

Tanzania tunashiriki kwa mara ya tano katika Miss Tourism World, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2005. Katika fainali zote tulizo shiriki tumeshinda mataji ya Dunia , mataji hayo ni :
Miss Tuourism World 2005- Africa (Witness Manwingi – Tanzania),
MISS TOURISM TANZANIA & MISS TOURISM WORLD 2005- AFRICA- Witness Manwingi


Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2006 – SADC (Killy Janga Left),
Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2007 – Africa (Lillian Cyprian ),



Miss Tourism Tanzania & Miss Tourism World 2008- Internet (Lilly Kavishe 1ST Left)
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi (right)
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi
 Miss Tourism Model Of The World 2006 –Personality ( Witness Manwingi).
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi
Miss Tourism Tanzania ,the Miss Tourism World 2005- Africa witness Manwingi

 
MISS TOURISM TANZANIA 2013 ,Hadija Saidi Mswaga
Hadija saidi alishinda Taji la Miss Utalii Tanzania 2013, baada ya kuwashinda washiriki wengine 24 kutoka mikoa yote ya Tanzania, katika fainali zaTaifa zilizo fanyika Tanga Mei 19, 2013. Hajija Saidi Juma Mswaga, mwanafunzi wa Diploma ya Mahusiano ya Umma na Matangazo katika Chuo cha DSJ. 
MISS TOURISM TANZANIA 2013


TOP 5 MISS TOURISM TANZANIA 2013
Anawaomba watanzania kumpa ushirikiano wa hali na mali ikiwemo sala na Dua katika kufanikisha maandalizi, safari na kutwaa taji hilo la Dunia.
“ Kwakuwa nakwenda kuwakilisha Taifa, anaye shiriki sio Hadija tena bali ni Tanzania, najua jukumu kubwa la kuifanya Tanzania kushinda , najua pia kazi niliyo nayo ya kutangaza Utalii na Utamaduni wa Tanzania na  kulinda heshima ya  Miss Utalii Tanzania , ya kushinda kila mwaka na siyo kushindwa , nikifuata nyayo za walionitangulia. Naomba Dua na sala zenu

Friday, August 30, 2013

David Mwantika amrithi Kelvin Yondani Taifa Stars, kocha Kim Poulsen amuita kikosini

Beki David Mwantika (kulia) aliyeitwa Taifa Stars kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki wa Azam, David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. 

Mbali na Yondani Stars ina wachezaji majeruhi watatu ambao kocha Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao. 

Wachezaji hao ni Athuman Idd 'Chuji' , Shomari Kapombe na John Bocco 'Adebayor'.

Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. 

Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BIL. 5.5/-

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

Gervinho achekelea kuhama Arsenal

http://u.goal.com/310700/310729_heroa.jpg
MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho (26) amebainisha kwamba alifurahi sana kuondoka Arsenal.
Nyota huyo amesema alikuwa na maisha magumu London Kaskazini na kwamba ilipotokea ofa ya kuondoka aliichangamkia haraka.
Gervinho alishuka kiwango na akashindwa kuonyesha makali yake Arsenal baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa paundi milioni 10.8 akitokea Lille mwaka 2011.
Alikamilisha uhamisho wake wa kutua Roma mapema katika kipindi hiki cha usajili chini ya kocha wake wa zamani wa Ufaransa, Rudi Garcia na amesema atatisha chini ya kocha huyo.
Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 8 alisema: "Ilikuwa ni faraja kubwa kwangu kuchezea Arsenal, lakini baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka ilikuwa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.
"(Arsene) Wenger, nadhani ni kocha mkubwa. Ni mtu ambaye namheshimu sana na nina furaha kubwa kupata fursa ya kucheza katika timu yake. Nadhani washambuliaji wanahitaji kuaminiwa na kocha wao na kupewa muda mwingi wa kucheza. Nilitamani nami iwe hivyo. Lakini ukurasa huo umepita mambo yamebadilika. Naweka akiliyangu yote Roma.
"Roma ni timu kubwa yenye kocha mkubwa. Sikujiuliza kukubali ofa yao.
"Daima nina mahusiano mazuri na Garcia - amekuwa akinijengea kujiamiani daima, na alikuwa ndiye kocha wa kwanza kunichezesha kwenye wingi.
"Nataka kuonyesha naweza kuisaidia timu. Siko katika hali nzuri kimwili kwa sasa, lakini Garcia ananifahamu vyema, nina kazi ya kufanya ili niwe fiti tena."
(Talksport)

Diamond nouma, amzawadia Mzee Gurumo gari...wengine mpo...!

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Show.
Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

STAA wa nyimbo za 'Kesho', 'Nataka Kulewa', 'Mawazo' na vingine, Naseeb Abdul ameonyesha mfano kwa wadau wa muziki nchini baada ya kumzawadiwa gari mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyetangaza kustaafu, Muhidini Gurumo.
Diamond alimkabidhi Gurumo gari hilo kuonyesha kujali na kuthamini mchango wa mwanamuziki huyo, baada ya hivi karibuni kunukuliwa 'akilia' kwamba kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa mwanamuziki anastaafu akiwa hana hata baiskeli.
Alichokifanya Diamond ni jambo la kupongezwa na kuigwa na wadau wengine wa muziki kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe (Gurumo) kwamba angependa ale jasho na kupewa pongezi zake angali hai badala ya watu kumsubiri afe ndipo watu wajitokeze kumwagia sifa na kujifanya kumuenzi wakati akiwa hao walimtelekeza.
MICHARAZO inakupa pongezi Diamond na tunawaomba wengine wamsadie mkongwe huyo ambaye amestaafu siyo kwa sababu ya kuishiwa kimuziki, bali hali yake ya kiafya akisumbuliwa na maradhi na wenye kutaka kumchangia watume fedha kwa njia ya TiGO Pesa katika simu yake ya mkononi 0655-401383.

Thursday, August 29, 2013

Frank Ribery ndiye Mchezaji Bora Barani Ulaya awabwaga Messi na Ronaldo

Frank Ribery ambaye kiimani ni Muislam akiomba dua kabla ya kuanza pambano la soka la timu yake ya Bayern Munich

NYOTA wa Kifaransa anayeichezea klabu ya Bayern Munich, Frank Ribery amewagaragaza wakali wa Hispania, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo kwa kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2012-2013.
Mkali huyo aliyeisaidia Bayern Munich kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na mengine mawili ya Ligi ya Ujerumani alitangazwa kunyakua tuzo hiyo leo barani humo.
Ribery amenyakua tuzo hiyo akimpokea Iniesta wa Barcelona aliyenyakua msimu uliopita akitanguliwa na Messi aliyetwaa mwaka 2010-2011.
Nafasi ya pili katika kimyang'anyiro hicho ilienda kwa Messim kisha Ronaldo aliyeshina nafasi ya tatu, ingawa hjakuweza kuhudhuria sherehe hizo zilizoenda sambamba na kutangazwa kwa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013-2014.

Rais Kikwete amteua Kamishna Mkuu Idara ya Uhamiaji

Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza
 
Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
 
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 
 
 

Makundi UEFA League yatoka, Barca, Milan, Ajax chungu kimoja

MAKUNDI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yametangazwa leo ambapo mabingwa wa Hispania, Barcelona wametupwa kundi moja na AC Milan na Ajax, wakati Chelsea wameweka kundi moja na 'wasumbufu' Basel.
Makundi kamili ya ligi hiyo ambapo mabingwa wake watetezi ni Wajerumani Bayern Munich, ni kama yafuatayo;
 
Group A
Man. United (ENG)
Shakhtar Donetsk(UKR)
Leverkusen(GER)
Real Sociedad(ESP)
Group B
Real Madrid(ESP)
Juventus(ITA)
Galatasaray(TUR)
København(DEN)
Group C
Benfica(POR)
PSG(FRA)
Olympiacos(GRE)
Anderlecht(BEL)
Group D
Bayern(GER)
CSKA Moskva(RUS)
Man. City(ENG)
Plzeň(CZE)
Group E
Chelsea(ENG)
Schalke(GER)
Basel(SUI)
Steaua(ROU)
Group F
Arsenal(ENG)
Marseille(FRA)
Dortmund(GER)
Napoli(ITA)
Group G
Porto(POR)
Atlético(ESP)
Zenit(RUS)
Austria Wien(AUT)
Group H
Barcelona(ESP)
Milan(ITA)
Ajax(NED)
Celtic(SCO)