STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 30, 2014

Monaco yafungwa na kibonde na kuipa nafuu PSG

TIMU ya AS Monaco imetoa mwanya zaidi kwa PSG kunyakua taji la ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo baada ya usiku wa jana kukubali kipigo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya Evian TG.
Bao la 'jioni' la mkwaju wa penati lililotumbukizwa na  Mkongo Cedric Mongongu, lilitosha kuikwamisha Monaco kuendelea kuipulia japo kwa mbali PSG iliyowaacha kwa pointi 13 wakati ligi ikisaliwa mechi saba kabla ya kukamilishwa kwake.
PSG inaendeelea kuongoza katika msimamo ikiwa na pointi 76, na Monaco ikisaliwa na pointi 63 zote zikiwa zimecheza mechi 31 kila moja.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa jana Sochaux ilishindwa kutambiana na Olympique Marseille kwa kutoka sare ya 1-1,   Ajaccio  na  Toulouse zilitoksa mabao 2-2, huku Montpellier ikabanwa nyumbani kwake na  Valenciennes kwa kulazimishwa suluhu kama ilivyokuwa kwa pambano la  Nantes na Bordeaux nazo timu za  Reims na Lorient pia zilitoka sare ya 1-1.

Leo ni vita tupu ligi kuu Tanzania Bara, Yanga, Azam, Mbeya City kuvuna nini?

Mbeya City wataumana na Prisons Mbeya je wataendeleza ubabe wake kwa maafande hao
Yanga wapo kibaruani Mkwakwani Tanga dhidi ya maafande wa Mgambo

Azam kuendeeleza rekodi ya ubabe katika ligi kuu leo kwa Simba?
KITIMTIM cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea tena leo kwa viwanja sita kuwaka moto, huku vitatu kati ya hivyo vikisubiriwa kwa hamu kutoa picha halisi ya mbio za ubingwa kwa msimu huu kwa timu tatu kati ya nne zinazochuana kileleni.
Viwanja vya Mkwakwani-Tanga, Sokoine-Mbeya na Taifa- Dar es Salaam vitakavyofuatiliwa kwa vile bndivyo vilivyoshikilia hatma ya mbio za ubingwa kwa msimu baina ya timu za Azam, watetezi Yanga na Mbeya City.
Vinara Azam wanaoongoza msimamo wakiwa na pointi 50 watakuwa wenyeji wa Simba uwanja wa Taifa, huku Yanga watakuwa ugenini mjini Tanga kuvaana na Mgambo JKT na Mbeya City iliyo nafasi ya tatu itaumana na 'kaka' zao Prisons iliyotoka kupokea kipigo cha 'paka mwizi' cha mabao 5-0 toka kwa Yanga katikati ya wiki jijini Dar.
Azam iliyopania kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya misimu miwili mfululizo kumaliza nafasi ya pili, inaonekana kuwa na kazi rahisi kuliko Yanga na Mbeya City kutokana na vijana wa Msimbazi, Simba kupoteza 'dira' msimu huu.
Simba iliyopoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union haitarajiwi kuipa upinzani Azam walio kwenye kiwango bora kwa sasa ikiwa haijapoteza mchezo wowote katika ligi hiyo inayoelekea mwishoni.
Hata hivyo soka halitabiriki na Azam haipaswi kujiamini kupita kiasi mbele ya Simba, ambayo kama watageuzwa daraja na wapinzani wao itamaanisha kukosa uwakilishi wa nchi kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo na hata nafasi ya tatu kuipata itawahia vigumu.
Simba ina pointi 36 ikisaliwa na mechi nne ukiwamo wa leo na kama itashinda zote itafikisha pointi 48 zilizopitwa na Azam na zinakaribiwa kufikiwa na Yanga wenye 46 wakiwa nafasi ya pili.
Ukiondoa pambano hilo la uwanja wa Taiufa, Yanga wenyewe watakuwa na kibarua kigumu kwa Mgambo JKT walioapa mapema kuwatoa nishai kama walivyofanya kwa Simba mwezi uliopita walipowadungua bao 1-0.
Mgambo iliyo katika janga la kutaka kushuka daraja katikati ya wiki ilifumuliwa na Azam mabao 2-0 hivyo isingependa kupoteza mchi nyingine na ndipo inapooenekana Yanga ina kazi Mkwakwani.
Hata hivyo Yanga yenye safu kali ya ushambuliaji chini ya kocha aliyejijengea jina kubwa kwa kipindi kifupi Mholanzi, Johannes van der Pluijm, inatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi kama ilivyofanywa kwa Rhino Rangers na Prisons ili kutoipa nafasi Azam kuwakimbia zaidi kwenye mbio za ubingwa wakiwa na mechi moja mkononi.
Yanga kabla ya mechi ya leo imecheza michezo 21 na kubakisha mitano ambayo ikishinda yote itafikisha pointi 61, moja zaidi ya zile ambazo itazimaliza Azam iwapo itashinda mechi zake nne zilizosalia.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alinukuliwa  akisema wanaenda Tanga wakiwa na nia moja ya kushinda, ili wasiachwe mbali na Azam wanaowanyima raha hasa baada ya kupepesuka katika mechi mbili walizotoka sare.
Mechi nyingine yenye mvuto kwa leo ni ile ya Mbeya City dhidi ya Prisons-Mbeya ambazo zimekuwa na upinzani kama wa Simba na Yanga.
Katika mechi ya kwanza, Prisons wakiwa wenyeji walikubali kipigo cha mabao 2-0. hivyo kuilifanya pambano la leo kuwa na ushindani mkubwa ikizangatiwa Prisons wametoka kuchezea kipigo cha aibu toka Yanga a Mbeya wapo kwenye mbio za ubingwa.
Mechi nyingine zinazochezwa leo zitakutanisha Kagera Sugar dhidi ya Ruvu Shooting mjini Bukoba, Mtibwa Sugar itaialika Coastal Union mjini Manungu na JKT Ruvu wataikaribisha Rhino Rangers ambapo kipigo chochote kwao kinawashusha rasmi daraja.

Mashali amgaragaza Kaseba ka pointi na kutwaa mkanda wa UBO Afrika

Mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi 
Mtoto Zainabi 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa katika kona ya bondia Japhet Kaseba kabla ya kuanza kwa mpambano wao mkanda uho aliubeba kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki pamoja na mabondia waliokuwa wakiwania mkanda huo
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas Mashali kushoto na Japhet Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano huo 
Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba
Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo
Baadhi ya watoto ambao wanafanya mazoezi katika GYM mbalimbali walijitokeza kuamasisha ujumbe wa World Boxing Ordanization 'WBO'  kushoto nio Rashidi Matumla na kulia ni Promota kutoka tanga Ally Mwazoa ambaye anakuja kwa kasi uku akiwa na mapasmbano matatu mfululizo yatakayofanyika PTA Sabasaba
Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo
Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa
Baadhi ya watoto waliojitokeza katika kampeni ya kufanya mazoezi watoto wasipewe madawa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali uku wakiwa na zawadi zao walizopewa mabegi flana na glove zenye ubora wa hali ya juu
***
BONDIA Thomas Mashali usiku wa jana amethibitisha kuwa yeye kweli ni Simba Asiyefugika baada ya kumtwanga kwa pointi, Japhet Kaseba na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO Afrika.
Aidha mkali mwingine wa ngumi za kulipwa nchini, Allan Kamote wa Tanga alinyakua ukiwa wa kimataifa wa UBO baada ya kumshinda kwa KO Karage Suba katika michezo iliyochezwa kwenye ukumbi wa PTA-Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Katika pambano la Mashali na Kaseba mabondia walishambuliana kwa zamu, ingawa mshindi alionyesha uhai zaidi katika raudni mbili za mwisho.
Pambano hilo lililokuwa na raundi 10 uzito wa Lighheavy limemaliza ubishi baina ya mabondia hao ambao wiki kadhaa wamekuwa wakitambiana kila mmoja akidai ni zaidi ya mwenzake.
Katika pambano jingine la ubingwa waq kimataifa wa UBO Allan Kamote alimtwanga kwa TKO ya raundi ya tano Suba Karage aliyebadilishiwa dakika za mwisho baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Fadhil Awadh kufariki siku chache akijiandaa na pambano hilo.
Nalo pambano la Fred Sayuni dhidi ya Rajab Mahoja lilishindwa kuendelea baada ya Mahoja kuchanika na kushindwa kuendelea kuwania ubingwa wa Taifa wa PST na hivyo mpinzani wake kupeta.
Pambano hilo lilivunjika katika raundi ya nne, naye Said Mahundfi alimtwanga kwa pointi Jumanne Mohammmed katika pigano la uzito wa bantam na wakongwe Said Chaku Jocky Hamis walitoka sare, huku Issa Nampepeche akimtwanga kwa pointi Zuberi Kitandula na Majis Said kushinda pia kwa pointi dhidi ya Franki Zaga.
Mipambano yote iliandaliwa na promota Ali Mwazoa kutoka Tanga na kusimamiwa na PST chini ya Rais Emmanuel Mlundwa.

Saturday, March 29, 2014

Arsenal, Manchester City zashindwa kutambiana

Olivier Giroud and Mathieu FlaminiKLABU ya soka ya Arsenal imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Manchester City katika pambano la Ligi Kuu ya England.
Wageni wa walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 18 kupitia kwa David Silva na kudumu wakati wa mapumziko.
Hata hivyo wenyeji walifanikiwa kuchomoa bao hilo dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili kupitia kwa Mathieu Flamini akimalizia kazi nzuri ya Lucas Podolski.
Sare hiyo imeikwamisha Manchester City kukaa kileleni baada ya Chelsea kufungwa bao 1-0 na Crystal Palace kwani imefikisha pointi 67 kwa michezo 30 na kubakia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool yenye pointi 68 na itakayoshuka dimbani kesho Anfield kuumana na Tottenham Hotspur.
Arsenal yenyewe wamesalia kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi 64 na baada ya kushuka dimbani mara 32.

Samatta aivusha TP Mazembe 8 Bora

Shujaa Mbwana Samatta
TIMU ya TP Mazembe ya DR Congo imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sewe ya Ivory Coast.
Bao hjilo pekee lililoivusha Mazembe lilitupiwa kimiani na Mbwana Samatta  katika dakika ya 66, huku wakikosa pia penati baada ya Jonas Sakuwaha kushindwa kumtungia kipa wa Sewe Sylvain Gbohouo.
Ushindi huo uliopatikana mjini Lubumbashi, umeifanya Mazembe kufuzu kwa faida ya bao la ugenini kwani matokeo ya jumla yamekuwa 2-2 baada ya wiki iliyopita vijana hao wa Kongo kufungwa mabao 2-1 bao lililofungwa na Mbwana Samatta ambaye ni Mchezaji Bora wa Mwaka wa TP Mazembe kwa mwaka jana.

Ni Mwadui na Stand kupanda Ligi Kuu msimu ujao


Kocha wa Mwadui Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' akikaribia kuipandisha daraja timu hiyo
TIMU ya Mwadui Shinyanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu baada ya kuinyuka Toto Africans nyumbani kwao Mwanza kwa bao 1-0.
Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa ushindi huo wa ugenini imefikisha jumla ya pointi 28 na imesaliwa na mechi moja, huku Toto Africans ikipoteza matumaini ya kurejea katika ligi hiyo.
Hii inatokana na Stand Utd pia ya Shinyanga iliyopo nafasi ya pili kuibutua JKT Kanembwa nyumbani kwao mjini Kigoma kwa mabao 3-2 na kufikisha jumla ya pointi 26 na kuendelea kuibana Mwadui ambao wamekuwa na upinzani mkubwa baina yao.
Toto iliyopo nafasi ya tatu imebakia na pointi 21 ambapo hata kama itashinda mechi yao ya mwisho haitaweza kuwafikisha popote na kuziacha timu pinzani za Shinyanga, Mwadui na Stand zikisubiri kujua hatma ya mmoja wao kupanda Ligi Kuu msimu wa 2014-2015 siku ya Aprili 5 mwaka huu.
Tayari timu mbili za Polisi Moro na Ndanda Fc zimeshafuzu ligi ya msimu ujao baada ya kuongoza kwenye makundi yao ya A na B.