STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Meya Kinondoni kuzindua ngumi za 10 Bora J'mosi

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/mwenda-july19-2013.jpg
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuyazindua mashindano ya ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es Salaam yatakayoanza Agosti 30.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA) yanafahamika kama Kumi Bora na yataendeshwa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kufikia tamati Novemba 30.
Afisa Habari wa DABA, Mwamvita Jacob aliiambia MICHARAZO kuwa michuano hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Manyara uliopo Tandele CCM na siku ya ufunguzi Meya wa Mwenda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
Mwamvita alisema michuano hiyo itashirikisha klabu zote za ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es salaam.
"DABA inatarajia kuendesha mashindano ya ngumi ya Kumi Bora ambayo yatazinduliwa rasmi siku ya Jumamosi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda majira ya saa 10 na yatafikia tamati Novemba 30," alisema. Mwamvita alisema michuano hiyo itatumika pia kusaidia mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni kupata timu za kuziwakilisha kwenye mashindano ya taifa ya ngumi itakayofanyika Oktoba mwaka huu.

Mashindano ya Taifa ya Ngumi kufanyika Dar es Salaam

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhddcF-MxMlqN77vx2j6CNs-85ebzGojD4aTeLo4sW5wOZuB6p60bGAx7BrxG6fRYuzsdKszt6GavgOrodtapPnZKNoD44y6zavLzL4ku-NZ8H-rm-kigE-Ly7ftghKAYRHwF25sXLwyjg/s1600/MAKORE+MASHAGA.JPG
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWuMhlBsHqlimo-vs3x8ijj21c795yctomGWe_IU9i15wuzXi-qDbaao0gaC_fCRhdalp8189fj7rUjNEsvpif24sRt3zFjMjLbmGWBz0wyYDywnAsS7hPF4JJtHLi-9-eAUobfzO3Zo1N/s1600/IMG_1118.JPG
Mabondia kama hawa wataonyeshana kazi jijini Dar
MASHINDANO ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa yanatarajiwa kufanyika kuanzia  Oktoba 8-14 jijini Dar es Salaam.
Michuano hiyo itatumiwa kwa ajili ya kusaka wachezaji wa kuunda timu ya taifa kwa michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania itashiriki.
Baadhi ya mashindano ambayo Tanzania inatarajiwa kushiriki ni pamoja na Michezo ya Kanda ya tatu ya Afrika, Michezo ya Afrika na Ubingwa wa Dunia itakayochezwa mwakani na ile ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema kuwa michuano hiyo itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na vyombo vya Ulinzi na Usalama itafikia kilele siku ya Nyerere Day.
Siku hiyo huwa ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwl Julius Nyerere aliyefarikia Oktoba 14, 1999.
Mashaga alisema mashindano hayo yatahusisha mabondia vijana (youth), wakubwa (senior) na wanawake (women) kwa ratiba itatolewa siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Alisema timu shiriki zinatakiwa ziwe zimeshatuma majina ya vikosi vyao kabla ya Septemba 29 na timu zote zinatakiwa ziwe zimeshawasili jijini Dar es Salaam kabla ya Oktoba 7.
Mashaga alisema uzinduzi wa michuano hiyo itfanyika Oktoba 10 na mgeni rasmi watakayemtangaza baadaye.

As Vita, TP Mazembe hakuna mbabe Esperance yaua

http://voiceofcongo.net/wp-content/uploads/2014/05/as-vita-tp.jpg
WAKATI Esperance ya Tunisia ikimaliza mechi zake za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa heshima kwa kuilaza Al Ahly Benghaz ya Libya kwa bao 1-0, wapinzani wa soka wa DR Congo AS Vita na TP Mazembe zenyewe zimeshindwa kutambiana baada ya kutopka suluhu mjini Kinshasa.
Pambano la Mazembe na Vita lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na upinzani wa timu hizo mbili za Kongo ambazo zote zimeshafuzu hatua ya Nusu Fainali kutoka kundi A lilishuhudia dakika 90 zikiisha milango ikiwa migumu.
Katika mechi hiyo watanzania wanaoichezea TP Mazembe Mbwana Samatta na Ulimwengu Thomas aliyeingizwa kipindi cha pili wakijitahidi kuipigania timu hiyo wakishirikiana na wenzao lakini bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Mazembe wamemaliza kileleni kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa licha ya kuwa na pointi 11 sawa na wapinzani wao hao.
Katika mechi nyingine ya kundi B Esperance ya Tunisia ilikamilisha ratiba yake kwa kuilaza ndugu zao wa Libya Al Ahly Benghaz na kuishia kukamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7.
Katika mechi nyingine za kukamilisha ratiba kwa Kombe la Shirikisho, Sewe Sport ya Ivory Coast iliinyuka Nkana Red Devils kwa mabao 3-0, huku Al Ahly ya Misri ilibanwa nyumbani na Etoile du Sahel na kutoka suluhu licha ya kwamba imeshafuzu Nusu Fainali ikiungana na Sewe.
Mechi nyingine AC Leopards ya Congo iliifumua ASEC Memosa kwa mabao 4-1 na Real Bamako ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Coton Sport ambayo iliungana na Leopards kufusu hatua ya nusu fainali kutoka kundi B.

Mcameroon afa uwanjani kwa kupigwa na kitu kichwani

http://www.maracanafoot.com/wp-content/uploads/2013/09/Ebosse1.jpgMCHEZAJI kutoka nchini Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu na mashabiki katika mchezo wa ligi nchini Algeria.
Ebosse, 24, alithibitishwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi Ouzou, mashariki mwa mji mkuu, Algiers.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa amefunga goli moja katika mchezo huo waliopoteza kwa 2-1, dhidi ya USM Alger aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika, wakati wachezaji wakiwa wanatoka uwanjani.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka uchunguzi kufanyika mara moja.
Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa nacho, lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa na kufungwa na walikuwa wakirusha mawe.
Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema :”alikufa kutokana na jeraha la kichwani” baada ya kurushiwa kitu mwisho wa mchezo.
Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Issa Hayatou ametoa taarifa inayolaani tukio hilo.

Waziri Mwigulu Nchemba asitisha safari kuokoa majeruhi wa ajali


Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo. 

Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.


Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Lori Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
 
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Lori hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
 
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,
 
Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
 
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongeza sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.

Chriss Brown anusurika kufa kwa risasi Marekani

Chris Brown aliyenusurika kuchapwa risasi
http://www.vibe.com/sites/vibe.com/files/styles/article-bounds-718/public/photo_gallery_images/suge-knight-crazy-quotes.jpg
Suge Knight aliyejeruhiwa kwa risasi mbili
MUIMBAJI nyota wa Marekani Chris Brown amenusurika kuuawa katika shambulio la risasi ndani ya klabu ya usiku jijini Los Angeles ambapo prodyuza Suge Knight amejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika klabu ya usiku iitwayo 1OAK iliyopo magharibi mwa Hollywood wakati wa shoo iliyokuwa ikiongozwa na Cris Brown kabla ya zoezi la utoaji Tuzo za VMA ambapo watu watatu wamejeruhiwa mmoja akiwa mahututi.
Suge Knight alipigwa risasi mara mbili tumboni na mkononi na kukimbizwa hospitali ambapo anaendelea na matibabu.
Mastaa wengine waliokuwepo kwenye klabu hiyo wakati tukio hilo likitokea ni pamoja na Justin Bieber, rappa The Game, Pia Mia, Tyson Beckford, Robert Ri'chard  na wengineo.
Indaiwa mlengwa mkuu katika shambulio hilo alikuwa Chris Brown, lakini Mungu akamuepushia msala huo unaokumbusha matukio ya nyota wa hiphop 2 Pac Shakur na BIG Notorious waliouwawa katika mikasa tofauti ya ulipizaji kisasi baina ya kambi za East Coast and West Coast

Sunday, August 24, 2014

Maajabu! Maiti iliyozikwa miaka 700 yakutwa bado wamo!

Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza
Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme. 
Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kazi ya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.
Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu  na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini...
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti

Noma! Raia wa UK agundulika kuambulizwa Ebola


Daktari wa Ebola nchini Liberia
Raia mmoja wa Uingereza anayeishi nchini Sierra leone ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Idara ya afya imethibitisha kisa hicho.
Tangu mwezi machi zaidi ya watu 1400 wameripotiwa kufariki magharibi mwa Afrika.
Idara ya afya imesema kuwa raia wa kwanza mwingereza kuambukizwa ugonjwa huo alikuwa anaishi Sierra Leone.
Taifa hilo ni miongoni mwa mataifa ambayo yameathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Mwathiriwa wa Ebola aliyepona
Iwapo atapewa matibabu nchini Uingereza mgonjwa huyo ana uwezekano mkubwa wa kupata nafuu kwa sababu hospitali za Sierra Leone zimejaa waathiriwa wa ugonjwa huo hatari ambao unaendelea kuenea kwa kasi.
Eneo la kuwatenga wagonjwa tayari limebuniwa katika hospitali ya Royal free mjini London.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa ebola,ijapokuwa dawa ya majaribio iliwasaidia raia wawili wa Marekani kupona huku maafisa watatu wa afya pia wakionyesha dalili za kupata nafuu walipoitumia dawa hiyo nchini Liberia.
Katika mataifa ya afrika magharibi wakaazi wengi wamekuwa wakiogopa kuwatoa ndugu zao wanaoathiriwa na ebola kwa hofu ya kutowaona tena.
BBC SWAHILI

Shaaban Kisiga 'Marlone' anayeipa Simba ubingwa 2014-2015

WAPO baadhi ya mashabiki wa soka wanaishangaa Simba kwa kuamua kumrejesha kikosini kiungo wao wa zamani, Shaaban Kisiga 'Marlon' kwa kuamini kuwa ni 'zilipendwa'.
Hata hivyo kwa wanaotambua kipaji na uwezo mkubwa wa nyota huyo wa zamani wa Stars aliyetokea Mtibwa Sugar wanajua Simba itavuna nini kwa Kisiga.
Licha ya kuwepo dimbani kwa muda mrefu, bado uwezo wa Kisiga ni ule ule zaidi  umeongezeka kutokana na uzoefu alionao na jinsi anavyojitunza kama mwenyewe anavyosema.
"Kisiga ni yule yule, hajabadilika kitu sanasana ameongeza mzoefu zaidi. Nimerejea Simba baada ya miaka 9 ili kuirejeshea heshima," anasema.
Kisiga aliyefanya kazi na Phiri miaka 10 iliyopita anasema Mzambia huyo siyo bonge la kocha tu, bali ni baba mlezi anayejua kukaa na wachezaji na kuwafanya wafanye kazi zao kwa ufanisi dimbani.
"Binafsi nimefurahi kurejea Simba na kukutana tena na Phiri, Simba watarajie makubwa msimu huu chini ya kocha Phiri," anasema.
Kuhusu ushindani ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Kisiga anasema amejiandaa kupambana akitumia uzoefu alionao kuhakikisha anapata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
"Ndani ya Simba kuna ushindani mkubwa kwani kuanzia namba 6-11 kuna vipaji vikubwa hivyo kufanya kila mchezaji kupambana  kujihakikishia namba jambo ambalo hata mimi nalifanya," anasema.
Nyota huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa Umangani, anasema ubinafsi na chuki ndivyo zinavyoua vipaji vingi vya soka nchini na kuikwamisha Tanzania kutamba kimataifa kwenye michuano ya kimataifa.
Anasema wapo wachezaji waliokatishwa tamaa na kuacha soka wangali wana uwezo mkubwa dimbani na kuwataka wadau wabadilike kama wanataka Tanzania ifanye vyema kimataifa.
"Leo vipaji vya akina Said Sued, Nurdin Bakar au Boban (Haruna Moshi) vimepotea kwa sababu ya chuki na ubinafsi, siyo kama soka lao limeisha. Hatuwezi kufika mbali kwa hali hii," anasema.
Anasema uteuzi na usajili wa kujuana na kubebana umekuwa ukifanya timu za Tanzania kuachwa mbali na mataifa hata yaliyokuwa nyuma.
Shabiki huyo wa Liverpool na asiyemhofia mchezaji yeyote dimbani anasema lazima viongozi na wadau wa soka waangalie kile ambacho mchezaji anachokifanya dimbani na siyo yale ya nje ya dimba.
"Wapo watu wanawahukumu wachezaji kwa matendo yao ya mitaani wakati uwezo wao dimbani ni msaada mkubwa kwa taifa, japo ni kweli nidhamu ni kitu cha muhimu katika kila jambo," anasema.
Anasema pia wadau wa soka wamekuwa wakiwabeza wachezaji wazoefu kwa kuwaita 'wazee' wakati Ryan Giggs na wakali wengine wa Ulaya wanazichezea klabu zao hadi wakiwa na miaka zaidi ya 40.
"Watanzania waache tabia hizi, mtu kucheza muda mrefu haina maana mtu ni mzee. Hata wale wanaonibeza sasa ndiyo hao hao watakaokuwa wakinishangilia dimbani kwa sababu soka nalijua na bado nina uwezo mkubwa," anasema.
Juu ya pambano asilosahau, Kisiga anasema ni lile la Nusu Fainali la Kombe la Kagame 2004 kati ya Simba na APR lililochezwa Kigali, Rwanda na Simba kung'olewa kionevu kwa kufungwa mabao 2-1.
"Nalikumbuka kwa jinsi tulivyopambana, lakini wenyeji walikuja kubebwa na kutuondosha mashindano kwa mabo 2-1," anasema.
Kisiga ambaye hana mpango kabisa wa kustaafu kwa sasa anasema anaamini ligi kuu ijayo itakuwa ngumu na yenye ushindani zaidi ya msimu uliopita kwa jinsi timu zinavyofanya maandalizi mazuri.
Hata hivyo anasisitiza kuwa msimu wa 2014-2015 ni wa Simba iwe isiwe kwa sababu wamefanya usajili mzuri chini ya uongozi makini na kocha bora hivyo siyo rahisi kulikosa taji linaloshikiliwa na Azam.
"Naamini ni zamu ya Simba safari hii, tutapambana kuirejeshea ubingwa na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, muhimu tushikamane na kuwa wamoja ndani ya Simba," anasema Kisiga.

Newz Alert! Ajali mbaya yatokea Mbeya, 10 wajeruhiwa


















TAARIFA KAMILI BAADAE
PICHA NA MBEYA YETU

Mshale wa Aisha Bui kutupwa wiki ijayo siyo kesho tena

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXMubpSkoyEQuwMbeI-V_WEnpb2FZ55PnmSTksu9SQcbRJoiwNFcLnFxjnDHjjzi94I0uF5_h6NYkWE5ZClymhKjniWp9O0pMjTGLQRCQHBZRPqT21Lfx13uwenFVycRWQjPOaQzcETW0/s1600/DUI.jpg
Aisha Bui
FILAMU mpya ya muigizaji nyota wa filamu nchini, Aisha Fat'hi 'Aisha Bui' iitwayo 'Mshale wa Kifo' inatarajiwa kuingia sokoni wiki ijayo baada ya mipango ya kuitoa leo Jumatatu kushindikana.
Aidha mwanadada  ametamba kuwa filamu hiyo ni mwanzo wa uhondo ambao kampuni yake ya Bad Girl Film's imepanga kuwapa mashabiki wa filamu Tanzania.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo aliyoigiza na wakali kama Mzee Chilo, Gabo wa Zagamba na wengine ilikuwa itolewe leo, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake itaingia sokoni Septemba 4, huku ikijipanga kuandaa kazi nyingine kali zaidi na hiyo.
Aisha Bui, alisema japo filamu hiyo ni kazi yake ya kwanza kuiandaa, lakini kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa umakini mkubwa ni wazi mashabiki watajua ujio wake mpya siyo wa kubahatisha.
"Naiachia filamu yangu mapema mwezi ujao badala ya Jumatatu (leo), nawaomba mashabiki waniunge mkono kwa kununua nakala halisi, ili kuiwezesha kampuni ya Bad Girl kuendelea kuwapa uhondo zaidi, kuna makubwa yapo njiani kutoka kwangu," alitamba Aisha Bui.
Nyota huyo aliyecheza filamu mbalimbali ikiwamo ya Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife, alisema ndani ya filamu hiyo mpya inasimulia kisa cha mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye anamlazimisha askari Polisi kumsaidia kupitisha mzigo wake.
Hata hivyo kazi haiwi rahisi na kuibua kashkash kwa binti wa askari huyo Myrine nafasi iliyochezwa na Aisha kufanywa kama chambo.
"Ni simulizi linalosisimua na kutia simanzi na bahati nzuri walioiigiza kuanzia mimi mwenyewe, Gabo, Mzee Chilo na wengine tumeitendea haki," alisema Aisha.

KIVUMBI AFRIKA AS VITA vs TP MAZEMBE NI SHIIIDA!

http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/04/mazembe.jpg
TP Mazembe
https://lh5.googleusercontent.com/-WVEVQ9rwWPA/T4sgtVuUV_I/AAAAAAAASJ0/i37zP2UN0W0/IMG_0282.jpg?imgmax=800
AS VITA
KIVUMBI za mechi za kuhitimisha hatua ya makudni kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kinatarajiwa kutimka vumbi leo kwa klabu nane zitakazposhuka dimbani kumalizia viporo vyao kabla ya kuruhusu kuanza kwa mechi za nusu fainali za michuano hiyo mikubwa.
Vita Club itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kupepetana na 'ndugu' zao TP Mazembe kuwania uongozi wa kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku timu za Esperance ya Tunisia ikiialika Al Ahly Benghazi wa Libya mjini Tunis katika mechi nyingine kamambe.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho AC Leopard ya Congo itaialika ASEC Memosa ya Ivory Coast, huku Real Bamako ya Mali itaialika Coton Sports ya Cameroon katika pambano jingine la kukata na mundu la michuano hiyo.
Pambano la la mahasimu DR Congo As Vita dhidi ya Mazembe ndizo zinazosubiriwa kwa hamu na amshabiki kutokana na upinzani wao na wengi kutaka kuona kama Vita italipa kisasi kw akipigo ilichopewa na TP Mazembe katika mechi yao ya mkondo wa kwanza.
Pia Vita imekuwa nyonge kwa wapinzani wao hata kwenye Ligi Kuu ya DR Congo, hivyo mechi yao leo licha ya kutaka ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kwanza ya kundi hilo, lakini pia kulinda heshima yao dhidi ya mahasimu wao wanaotamba na nyota wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.