STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, July 2, 2013
Wakora wamkata binti mikono, kisa kinasikitisha
| Picha hii haihusiani na habari hii |
GENGE moja nchini India limekata
mkono wa binti mmoja mwenye miaka minane kwa kutumia fyekeo huku familia
yake ikijaribu kuhakikisha kuachiwa kwa kaka yake aliyetekwa nyara.
Uzma Ara alisafiri kwenda Patna, mjini Bihar, mashariki mwa India, akiwa na familia yake kwa lengo la kumkomboa mtoto huyo wa kiume mwenye miaka minne ambaye alikuwa amenyakuliwa kwenye mtaa mmoja karibu na nyumbani kwao katika wikaya ya Darbhanga.
Baba wa Uzma, Ainul Ansari anadai genge hilo lilimlenga binti huyo kutokana na kuwa shuhuda mkuu wa tukio hilo la utekwaji wa mtoto wake, Julfikar.
Vyombo vya habari vya India vimeripoti binti huyo yuko mahututi kwenye hospitali moja ya serikali mjini Patna baada ya kupoteza sehemu ya mkono wake wa kulia.
Familia hiyo imesema binti huyo alishambuliwa karibu na stesheni ya treni mjini humo Ijumaa wakati wakitafuta hoteli ya kukaa.
Ansari alisema kundi hilo liliwafuata hadi Patna ambako walikuwa wanatarajia kufungua mashitaka polisi.
Serikali ya Janata Dal inayoongozwa na Waziri Mkuu Nitish Kumar sasa imeamuru uchunguzi mpya wa shambulio hilo na mtoto wao wa kiume aliyepotea.
Mama wa Uzma, Nasreem Khatoon alimpinga moja kwa moja waziri mkuu huyo kwenye mkutano wake wa kila wiki.
Familia hiyo inasema polisi wa eneo hilo wameendelea kumshikilia mtoto huyo aliyepoteza mkono wake kwenye ajali ya treni.
Ansari ambaye ni fundi cherehani, alisema amekuwa akilazimishwa kulilipa genge hilo Pauni za Uingereza 3,300 kwa miezi michache iliyopita, imeripotiwa.
Anasema kwamba polisi wamegoma kuchunguza pale familia hiyo ilipogoma kulipia zaidi, genge hilo lililomteka mtoto wao.
Wanasiasa wa upinzani sasa wameishutumu serikali ya mjini humo kwa kushindwa kuchunguza madai hayo moja kwa moja.
Msemaji wa chama cha Bharatiya Janata, Shahnawaz Hussain alinukuliwa na Shirika la habari la Gulf akisema kwamba waziri mkuu huyo amechangia 'kuanguka kabisa kwa sheria' mjini Bihar.

Julio kutupiwa virago Simba kama Kaseja
![]() |
| Julio kwenye kijitabu akiwa na makocha wenzake kwenye mazoezi ya Simba uwanja wa Kines hivi karibuni |
Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na gazeti la NIPASHE ni kwamba maamuzi ya kutimuliwa kwa Julio kunatokana na kumaliza mkataba wake wa muda mfupi na tayari maamuzi yameshapitishwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ili nafasi yake ichukuliwe na Seleman Matola.
Mmoja wa vigogo wa Simba aliyenukuliwa na gazeti hilo alisema kuwa tayari maamuzi ya kuachana na Julio yameshatolewa na nafasi yake itachukuliwa na kiungo na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Matola.
Kigogo huyo alisema vilevile kuwa katika kikao hicho, watajadili maandalizi na kupanga siku ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
"Sasa presha imehamia kwa Julio ambaye hatma yake haijulikani ndani ya Simba, lakini kilichopo ni kama ilivyokuwa kwa Kaseja," alisema kigogo huyo.
Julio alipotafutwa kuelezea hatma yake, alisema yuko kwenye kelele na atafutwe baadaye ambapo hakupatikana tena kupitia simu yake ya mkononi.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliliambia gazeti hilo kuwa ni kweli kesho kamati ya utendaji itakutana lakini kubwa watakalojadili ni kupanga maandalizi ya wiki ya Simba.
Mtawala alisema kuwa kikao hicho kitabariki shughuli zote za kijamii zilizopangwa kufanyika na kumalizika kwa tukio la kutambulishwa kwa wachezaji wapya wa Simba katika siku ijulikanayo kama 'Simba Day'.
Alieleza pia zoezi la usajili wa wachezaji wapya limeenda kwa umakini na kwa zaidi ya asilimia 80 wamekamilisha mchakato huo.
Alisema kabla ya kuanza kwa msimu mpya, timu hiyo inatarajia kuweka kambi nje ya jiji la kucheza mechi za kirafiki zaidi ya tatu kwa ajili ya kuwaandaa na kuwaweka tayari kukabiliana na ushindani katika msimu ujao wa ligi.
Simba sasa inaendelea na mazoezi chini ya kocha wake mkuu, Abdallah Kibaden 'King' wakati Matola akiendelea kuisimamia timu ya vijana (Simba B).
Mfalme Mswati aitimka zake kwao Swaziland
Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Julai 1,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kiataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Arsenal yamnyakuwa kinda la kifaransa ni Yaya Sanogo
![]() |
| Yaya Sanogo |
KLABU ya Arsenal imethibitisha katika tovuti yake kwamba mwanasoka kinda
wa kimataifa wa Ufaransa, Yaya Sanogo amesaini Mkataba wa muda mrefu
kwao.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amejiunga kwa ada ndogo tu
baada ya kumaliza Mkataba wake klabu ya Daraja la Kwanza Ufaransa,
Auxerre.
Sanogo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya
umri wa miaka 20, katika Kombe la Dunia la U-20, akiwa amefunga mabao
mawili kati ya matatu ya timu yake nchini Uturuki, na amefunga mabao
tisa katika mechi 13 katika msimu alioandamwa na majeruhi Ufaransa.
Gonzalo Higuain na Wayne Rooney ni washambuliaji wengine walioripotiwa
kutakiwa The Gunners msimu huu, lakini Wenger anavutiwa mno na uwezo wa
Sanogo."Sanogo ni usajili mzuri wa kinda kwetu,"aliiambia Arsenal.com. "Ameonyesha uwezo wake siku za karibuni akiwa na Auxerre na poa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 cha Ufaransa.
"Tunasonga mbele kwa Yaya kujiunga nasi na kuendeleza kukuza kiwango chake,"alisema Wenger.
Zoezi hilo lipo kwenye kukamilisha taratibu za kawaida za usajili na Sanogo atajiunga na wenzake baada ya mashindano ya Uturuki.
Hivi ndivyo Rais Obama alivyopokelewa Tanzania
RAIS OBAMA akiteremka kwenye Air Force One na mtoto wake pembeni mara baada ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania wakati akitokea afrika ya Kusini jana mchana kwa ziara ya kikazi nchini.
Barack Obama akipokewa na Wananchi wa Tanzanian huku wanaband
wakitumbuiza nyimbo mbalimbali kwenye uwanja wa Mwl.Julius Kambarage
jijini Dar es Salaam jana mchana akitoka Africa kusini.
Rais Obama akipita kwenye kapeti jekundu huku akiwa na furaha na kucheza nyimbo za wabongo kwenye uwanja wa jijini Dar es salaam wa Mwl. Julius Kambarage mchana wa jana.
Karibu Tanzania....karibu!!!
Ilikuwa ni patashika kwa wacheza ngoma hapa!!! Obama mpaka akaachia Tabasamu
Rais Obama akicheza nyimbo za hapa kwetu Bongo huku akiwa na furaha kwa mapokezi baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania jana.
Rais na First Lady Obama wakisalimia wananchi wa Tanzanian baada ya kupokewa na Rais Jakaya Kikwete na First Lady Salma
Ni furaha hapa baada ya Rais Obama kutua Bongo, hapa anaonekana na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakipokewa kwa ngoma
Ni mimi jamani ...tupo pamoja !.
Karibu jamani ....jaribu mzee!!! Tunakupenda!!
Mapokezi haya!!! angalia mavazi!!
Rais
Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na
Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam
jioni YA JANA ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini
Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa
ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.
Monday, July 1, 2013
Simba kutambulisha nyota wake wapya mkoani
KLABU ya Simba
ya jijini Dar es Salaam, imesema mara baada ya kuondoka kwa Rais wa Marekani,
Barrack Obama nchini, itafanya ziara katika mikoa ya Katavi, Tabora na Rukwa
kwa kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Mbali na kwenda katika mikoa hiyo, pia ipo katika mchakato wa kupiga kambi katika moja ya nchi jirani kwa ajili ya maandalizi zaidi ya ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alisema wamepata mwaliko kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Rajab Rutengwe akiomba timu hiyo iende mkoani kwake.
“Tumepokea mwaliko kutoka kwa rafiki yangu Shehe Rajab ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi akituomba tukamtembelee na kikosi changu chote, na sisi tupo tayari hatuna tatizo katika hilo,”.

“Kikubwa tunachosubili kama unavyojua hivi sasa nchi ina ugeni mkubwa wa Rais Obama, hivyo kila mtu yupo katika pilikapilika hizo lakini baada ya kuondoka tutasema tarehe rasmi ya kuondoka,”.
Alisema wakiwa huko wanatarajia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi katika mechi watakazocheza ambapo pia waziri huyo ameiomba timu yake ifike mpaka Jimboni kwake Mpanda Magharibi, Rukwa.
Alisema wakiwa katika mikoa hiyo pia watakwenda Tabora kucheza mechi ya kirafiki na baada ya kumaliza ziara hizo watarejea jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa wapo katika mipango ya kuhakikisha timu yake inaweka kambi moja ya nchi jirani ambapo ana uhakika baada ya kufanya hivyo, kikosi chake kitakuwa tayari kwa ligi kuu ya msimu ujao.
Wakati Simba ikijinadi hivyo, watani wao Yanga, wanatarajia kuondoka Ijumaa kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kulitembeza kombe lao la ligi kuu pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya KCC ya Uganda.
Mbali na hayo, pia itaingiza wanachama wapya pamoja na kuuza vifaa mbalimbali walivyonavyo.
Baada ya Obama leo, George Bush, mkewe nao kutua kesho Tanzania

RAIS
mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho
kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais
katika kuinua wanawake duniani.
Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa.
Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama.
Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.
Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake wa marais katika kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.

Ujio wa rais huyo mstaafu wa Marekani utakuja ikiwa ni saa kadhaa tangu mrithi wake, Barack Obama kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili ambapo anatarajiwa kuondoka kesho baada ya kumaliza shughuli mbalimbali alizopangiwa.
MAUAJI YA KUTISHA KWA VICHANGA MKOANI MBEYA, INATISHA!
| Kichanga kikiwa kinaelea kwenye mto mita chache toka eneo la Mabatini |
| Wakazi wa Mbeya wakishuhudia unyama aliofanyiwa kichanga hicho |
| Askari Polisi aklikiopoa kitoto hicho toka mtoni |
| ASKARI WA JESHI LA POLISI AKIWA ANAKIWEKA KICHANGA HICHO NDANI MFUKO BAADA YA KUKITOA KUTOKA MTONI |
![]() |
| Watoto nao wakishangaa kichanga hicho kilipokuwa kikiopolewa mtoni. |
| Huyu ndiye aliyebainika kukitupa kichanga chooni eneo la Stereo, Maanga, mjini Mbeya |
| Mwenyekiti wa mtaa wa Maanga, Mary Mwansankinga akiwa haamini alichokiona machoni mwake. |
| Asakri wa Jeshi la Zimamoto na Ukokozi wakihangaika kutaka kukiokoa kichanga kilichotuipwa chooni. |
| Baadhi ya mashuhuda wa tukio la mtaa wa Maanga |
| Hatimaye askari wanafanikiwa kukiopoa kichanga hicho cha kiume kutoka chooni. |
BAADHI YA WAKAZI WAKISHANGAA BAADA YA KITOTO KUOPOLEWA
ASKARI WA ZIMAMOTO BAADA YA KUOSHA KICHANGA HICHO AMBACHO KILIZALIWA KATIKA UMRI WAKE
WANANCHI WAKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUSHUHUDIA KICHANGA HICHO BAADA YA KUOPOLEWA
JESHI LA POLISI PAMOJA NA ASKARI WA ZIMA MOTO WAKIONDOKA ENEO LA TUKIO
HII
NI NYUMBA AMBAMO MTOTO ALITUPWA CHOONI , WATU WANAJIULIZA WENGINE
WANAANDAMANA KWENYE NYUMBA ZA MAOMBI NA WAGANGA KUTAFUTA WATOTO WENGINE
WANAWATUPA BILA YA KUWA NA HURUMA WALA HOFU YA MUNGU.
PICHA NA MBEYA YETU
Mke wa Obama akutana na Mama Kikwete WAMA
Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo...
Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana na watoto wao jioni hii ....
Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.
Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii.
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.
Rais Obama atua salama ardhi ya Tanzania atapa mapokezi ya aina yake
![]() |
| Rais Barack Obama akiburudishwa na ngoma asilia za Tanzania |
| Add caption |
RAIS wa Marekani ametua nchini salama na msafara wake ikiwamo familia yake na kupokewa na mapokezi ya aina yake na watanzania wakiongozwa na Rais Jakate Mrisho Kikwete na viongozi wengine waandamizi.
Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda mchache uliopita katia kuhitimisha ziara yake barani Afrika.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza ngoma za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam mara aliopowasilia majira ya saa nane mchana.
Mara baada ya ukaguzi wa gwaride na mambo mengine msafara wa Rais huyo anayetokea Afrika Kusini aliambatana na mwenyeji wake kwa ajili ya kuelekea Ikulu ya Tanzania kuendelea na ratiba zake ambapo inaelezwa anatarajiwa kufanyiwa dhifa maalum jioni hii katika makazi ya rais, Ikulu.
Subscribe to:
Posts (Atom)