STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 25, 2013

Awadh Juma alitoa bao lake kwa familia, amtetea Kaseja

Awadh Juma alipomtesa Kaseja katika mechi ya Simba na Yanga

KIUNGO mpya klabu ya Simba, Awadh Juma amesema anajisikia furaha kubwa kuitungua Yanga katika ushindi wa 3-1 wa mechi yao ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe na kwamba amelitoa bao hilo kama zawadi kwa familia yake.
Awadh alifunga goli hilo katika nyavu tupu baada ya kumpa 'presha' kipa Juma Kaseja aliyejikanganya na kuanguka nje ya boksi wakati akijaribu kuurudisha mpira kwenye eneo lake la kujidai ili audake na kumruhusu mfungaji kumtungua kiulaini.
Akizungumza na MICHARAZO, Juma alisema analitoa bao hilo lililomletea matatizo kipa anayeaminiwa kuwa bora zaidi nchini, Juma Kaseja, kama zawadi kwa familia yake inayomuunga mkono katika kila kitu chake katika soka.
Mkali huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Zanzibar, alisema bao lake lililokuja baada ya kumzidi ujanja Kaseja na kumnyang'anya mpira ulioonekana hauna madhara kwa Yanga ni mwanzo nzuri kwake ndani ya Simba na kudai amefurahi mno kuitungua Yanga na kupata bahati ya kuanza kwenye mechi kubwa kama hiyo.
"Siku zote nilikuwa naota kucheza pambano la watani za jadi na nimefurahia Simba kunisajili na kubahatika kupangwa katika pambano hilo na kufunga bao ambalo nalitoa kwa familia yangu kama zawadi kwao," alisema.
Aidha, mchezaji huyo amewaahidi wanachama na mashabiki wa Msimbazi kusubiri raha zaidi wakati mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakapoanza akisema alichokionyesha uwanjani siku ya Jumamosi ni sehemu tu ya ujuzi wake.
Awadh aliyesajiliwa akitokea Mtibwa Sugar alisema pamoja na watu kumsifia kwa kuonyesha kiwango kizuri katika pambano hilo lililochezwa uwanja wa Taifa, yeye anajiona kama amecheza kiwango cha chini na kuwaomba mashabiki na wanachama wa Simba kusubiri kuona ujuzi wake duru la pili litakapoanza.
"Tuombe uzima ligi ianze watu waone kiwango changu halisi, ila kwa kweli nashukuru na nimefurahi kutua Simba na kuanza kuitumikia kwenye mechi ya watani wa jadi," alisema.
Aidha Awadh alisema kosa lililofanywa na Kaseja linaweza kufanywa na yeyote hivyo asibebeshwe lawama kwani ni tukio la kwaida la mchezo.
"Sidhani kama kuna sababu ya Kaseja kusakamwa ni mmoja wa makipa hodari na lililomtokea huweza kumtokea yeyote asisakamwe," alisema Awadh aliyepo visiwani Zanzibar kwa sasa kwa mapumziko mafupi.

Huyu ndiye Katibu Mkuu wa TFF

Rais Jamal Malinzi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemuajiri Katibu wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Celestine Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirishiko hilo.
Taarifa ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi imesema kwamba, Mwesigwa amekidhi sifa za nafasi hiyo, akiwa na kiwango cha elimu ya Shahaha ya Uhusiano wa Kimataifa na Stashahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha, TFF pia imemuajiri katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF- ambaye ana Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia na Shahada ya Uzamili ya uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha ESAMI.
Jamal Malinzi amemuajiri Mwesigwa kuwa Katibu mpya Yanga SC anarithi nafasi ya Angetile Osiah

Malinzi amesema, Iddi Mshangama atakaimu ya nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, iliyokuwa inashikiliwa na Saad Kawemba, wakati Danny Msangi atakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TFF na Boniphace Wambura Mgoyo ataendelea kuwa Ofisa Habari wa shirikisho.
Malinzi aliyesema ajira zote zitaanza rasmi Januari 1 mwakani, pia ameteua Kamati tatu, ya Uchaguzi, Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF nay a Soka ya Ufukweni.
Kamati ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema, Makamu wake Wakili Walter Chipeta na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Hassan Daalal.
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, Makamu wake Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu, wakati Kamati ya Soka ya Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi na Wajumbe Deo Lucas, Juma Mgunda, Boniphace Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.

Tuesday, December 24, 2013

TCAA yamwaga msaada kwa yatima wa New Life Orphans

 Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya  ambao ni watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
 Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo  cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwa kabidhi msaada wa vyakula mbalimbali yakiwemo mafuta ya kupikia , mchele na sukari.
 Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa mafuta ya kula Mohamed Achume ambaye ni miongoni mwa  watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
Mohamed Achume anayelelewa katika kituo cha kule yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam akikabidhiwa  msaada  wa gunia la mchele na  Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka hiyo kwa ajiri ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya krismasi.

Arsenal yashindwa kurejea kileleni, yabanwa nyumbani na Chelsea



Chance: Olivier Giroud fires wide towards the end of the game
Oliver Giroud akikosa bao la wazi katika pambano lao la jana dhidi ya Chelsea
So close: Giroud looks on in disbelief after missing his chance to win the game
Hekaheka tupu langoni mwa Chelsea, Goroud akikosa tena bao la wazi
Agony: Giroud looks frustrated after missing the chance late on
Kudadeki imekuwaje lakini! Kama anasema Goroud wakati akisikitikia kukosa bao
High jump: Fernando Torres jumps for the ball in the Chelsea penalty area
Up close and personal: Lampard gets in tight on Mesut Ozil
Lampard na Ozil wakitunishia ubavu katika mechi ya jana
Sliding in: Per Mertesacker challenges Chelsea's Fernando Torres as he tries to get his shot away
Torres akijaribu kutumbukiza mpira wavuni bila mafanikio
Hitting the woodwork: Frank Lampard sees his effort hit the crossbar and bounce to safety
Hollaaaa! Lampard anakosa naye bao la wazi
Stop there: Eden Hazard is chased by Arsenal midfielder Aaron Ramsey
Eden Hazard akiwatoka mabeki wa Arsenal
LICHA ya kuwa uwanja wake wa nyumbani, Arsena jana imeshindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa suluhu na Chelsea waliorejea nafasi ya nne wakiishusha Everton.
Arsena ilikuwa kileleni kwa muda mrefu hata hivyo imetoka nafasi ya tatu iliyokuwa inashika baada ya matokeo ya mechi za wikiendi na kukaa nafasi ya pili nyuma ya vinara Liverpool wakilingana pointi 36 ila wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mchezo huo wa usiku wa jana timu zote zilikosa mabao ya wazi na wachezaji kuchezeana kitemi wakati fulani licha ya mwamuzi Mike Dean kudhibiti hali hiyo.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Alhamis kwa michezo kadhaa 10 itakazozikutanisha timu zote 20 zinzoshiriki ligi hiyo ambapo kivumbi kitakuwa kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool itakayochezwa uwanja wa Itihad.
Mechi nyingine siku hiyo kwa mujibu wa ratiba ya EPL ni kama ifuatavyo hapo chini;
Hull City  vs  Manchester United
Aston Villa  vs  Crystal Palace
Cardiff City  vs  Southampton 
Chelsea  vs Swansea City
Everton  vs  Sunderland 
Newcastle United vs  Stoke City
Norwich City  vs  Fulham 
Tottenham Hotspur  vs  West Bromwich
West Ham United   vs  Arsenal
Manchester City  vs  Liverpool

Monday, December 23, 2013

Hii ndiyo taarifa rasmi ya Yanga juu ya kocha Brandts

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjs2pxO5gXemOLQOz0BzMGxg7KsY0sYochSKjsWZaF1oKOTTlUVNFgR_JMNw07QVEN5ekr_bKv4ARveeZdHj-10ViLQ1qYWyQkJbM9rhkzi2CWkVzXC8PL5iqQI-BmNbq3m4la63z0rQc7I/s1600/BIN+KLEB.jpg
UONGOZI wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
 
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
 
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
 
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
 
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
 
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
 
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
 
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.

Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013
 

Yanga, Simba waingia Mil. 422

PAMBANO la Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba lililochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 limeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

Mwesigwa ndiye Katibu Mkuu TFF?

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/mweigwachequetbl.jpg
Celestine Mwesigwa
HABARI zilitufikia hivi karibuni zinasema kuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Celestine Mwesigwa ndiye Katibu Mkuu  mpya wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa Simba Evodias Mtawala ameukwaa ukurugenzi ndani ya shirikisho hilo.
Hata hivyo taarifa rasmi juu ya jambo hilo litawekwa bayana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kesho atakapotangaza safu mpya ya waajiriwa wa shirikisho hilo ikiwa ni mwezi mmoja na ushei tangu ashinde Urais katika Uchaguzi Mkuu wa TFF uliofanyika Oktoba 27.
Ila MICHARAZO inazo habari kwamba Mwesigwa aliyetimuliwa kihuni Yanga, ametwaa nafasi hiyo akiwashinda waombaji wengine. Ila vuteni subira hadi hiyo kesho mpate uhakika wa jambo hili toka mdomoni mwa Malinzi mwenyewe.

Kimenuka Yanga! Brandts atimuliwa kisa 3-1 za Simba


KWA wanaokumbuka jana blog hii iliwadokeza kuwa kulikuwa na fununu kwamba Yanga kupitia Mwenyekiti wake, Yusuf Manji angemfuta kazi kocha wa Yanga, Ernie Brandts.
Ingawa Manji alichomoa kiaina kusema moja kwa moja kwamba Brandts ndiyo basi tena Jangwani, na kuonekana kama anamtetea, imebainika kuwa Mholanzi huyo hana chake tena Yanga.
Mchana huu klabu hiyo ya Yanga ilitangaza kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hiyo.
“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.
Tetesi za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.
Uamuzi huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Breaking News! Lunyamila mahututi tumuombeeni




akiishuhudia Yanga ikichehzea kichapo cha mabao 3-0 mjini Morogoro toka kwa Mtibwa Sugar msimu uliopita

WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine.

Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.

Shaffihdauda.com imemshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni.



Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri.

“Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema Pascal.

Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.




 Lunyamila alivyokuwa enzi anaichezea Yanga..
“Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.
Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja... Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo. ''Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha '' ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.
SHAFII Dauda

Inter Milan waikausha AC MIlan Seria A, Muntari akilimwa RC jioni

AC Milan's forward Mario Balotelli kicks the ball during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
Mario Balotelli akikosa bao la wazi langoni mwa Inter Milan
AC Milan's French defender Kevin Constant fights for the ball with Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio during the Italian Serie A football match on December 22, 2013
Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio celebrates after scoring during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
'Muuaji; akishangilia bao lake
BAO lililofungwa na Rodrigo Palacio dakika nne kabla ya kumalizika kwa pambano la watani wa jadi wa mji wa Milan, liliisaidia Inter Milan kupata ushindi muhimu dhidi ya mahasimu wao Ac Milan katika mechi ya Ligi Kuu ya Italia, Seria A lililochezwa usiku wa kumakia leo.
Licha ya kipigo hicho pia, Milan ilipata pigo dakika za lala salama wakati kiungo wake, Sulley Muntari alipolimwa kadi nyekundu wakati mchezo ukielekea kumalizika.
Palacio raia wa  Argentina aliifungia Inter bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Fredy  Guarin na kuzidi kuicha Milan izidi kuchechemea kwenye ligi hiyo ikishika nafasi ya 13, huku wapinzani wao kwa ushindi huo wamekwea hadi nafasi ya tano ikifikisha pointi 31.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Milan kupata sare mfululizo katika mechi zake za hivi karibuni katika ligi na kuliacha benchi la ufundi la mabingwa hao wa zamani wa Ulaya wakiweweseka kujiweka sawa kabla ya kuwakuta yaliyowakuta makocha wa klabu nyingine waliotimuliwa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Livorno ililala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Udinese, Cagliari ililazlimishwa sare ya 1-1 na Napoli kwa mechi zilizochezwa Jumamosi.
Mechi zilizochezwa jana Bologna ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa, Atlanta ikalala kwa mabao 4-1 nyumbani kwake mbele ya mabingwa watetezi Juventus, huku Hellas Verona ikiishindilia Lazio kwa mabao 4-1.
Nayo Roma iliendeleza mauaji kwa kuilaza Catania kwa mabao 4-0,  Sampodoria na Parma zikitoka sare ya 1-1 na Fiorentina ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sassuolo na Chievo Verona ikilala ugeninikjwa mabao 4-1 toka kwa Torino.

Everton yaua ugenini, Chelsea ikiifuata Arsenal Emirates leo

Everton wakishangiulia bao lao la ushindi jana usiku mbele ya Swansea City
WAKATI Everton wakipata ushindi muhimu jana ugenini dhidi ya Swansea City, Arsenal na Chelsea leo zitakuwa kibaruani kutaka kurejea kwenye nafasi zao ilizokuwa ikizishikilia awali.
Arsena ilienguliwa kileleni na kuporomoshwa hadi nafasi ya tatu katika msimamo itakuwa nyumbani kuikaribisha Chelsea iliyoshushwa jana hadi nafasi ya tano baada ya Everton kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Swansea City.
Timu hizo mbili zinakutana zote zikitokea kupoteza mechi zao za mwisho, Arsena ikipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Napoli katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manachester City waliowasulubu kwa mabao 6-3.
Chelsea wenyewe walitoka kupokea kipigo cha aibu cha mabao 2-1 toka kwa vibonde wa Ligi Kuu, Sunderland katika mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One), huku ikishuhudiwa mabao yote matatu ya mchezo huo yakifungwa na vibonde hao na kutinga Nusu Fainali.
Ushidni wowote kwa timu hizo utakuwa na maana ya kurejea kwenye nafasi zao za awali, Arsena kurejea kileleni kunakoshikiliwa kwa sasa na Liverpool na Chelsea yenye pointi 33 ikishinda itakwea nafasi ya pili nyuma ya Liverpool wenye pointi 36 kwa sasa baada ya Jumamosi kushinda mabao 3-1 dhidi ya Cardiff City.
Arsena yenyewe ikishinda itafikisha jumla ya pointi 38 na kuziporomosha Liverpool; Manchester City inayokamata kwa sasa nafasi ya pili na hivyo itashuka dimbani katika pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Micheal Dean ikiwa na usongo wa kuizuia Chelsea ambayo katika mechi tatu mfululizo zilizopita baina yao wamekuwa wanyonge kwa kufungwa zote.
Katika mechi ya jana usiku, Swansea ikiwa nyumbani ilishindwa kuhimili vishindo vya wageni wao Everton ambao walifunga mabao yote matatu yaliyopataikana jana yakiwemo mawili yao ya ushindi na lile la kufutia machozi la wenyeji hao.
Everton waliandikisha bao la kwanza dakika ya 66 kupitia kwa Seamus Coleman kabla ya Bryan Oviedo kujifunga dakika nne baadaye na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Hata hivyo alikuwa ni Ross Barkley aliyeihakikishia wageni ushindi kwa kufunga bao dakika sita kabla ya pambano hilo kumalizika kwa mkwaju wa frikiki na kuifanya Everton kufikisha pointi  34 na kushika nafasi ya nne nyuma ya Arsenal yenye pointi 35.