STRIKA
USILIKOSE
Thursday, December 4, 2014
Mgendi aachia Wema ni Akiba, 'audio' albamu kabla ya X-mass
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi ameachia wimbo mpya uitwao 'Wema ni Akiba' ikiwa ni utambulisho wa albamu yake mpya ijayo.
Tayari wimbo huo wa Mgendi umeanza kutamba kwenye vituo vya redio na katika mitandao ya kijamii baada ya kuuachia mapema wiki hii.
Akizungumza na MICHARAZO Mgendi alisema kuwa albamu yake ijayo itakuwa na nyimbo saba na ameutanguliza uliobeba jina kwa nia ya kuitambulisha kabla ya kuja kuiachia rasmi baadaye.
"Nimeachia wimbo wangu mpya ambao ni utambulisho wa albamu ijayo itakayofahamika kwa jina la 'Wema ni Akiba' itakayokuwa na nyimbo saba," alisema Mgendi.
Muimbaji huyo alizitaja baadahi ya nyimbo za albamu hiyo kuwa ni 'Wema ni Akiba', 'Usiniache Njiani', 'Nimempata Yesu', 'Nani Kama Mungu' na 'Kimbilia Msalabani'.
Albamu hiyo mpya imekuja wakati albamu ya msanii huyo iitwayo 'Hongera Yesu' ikiwa bado haijachuja sokoni ambayo aliiachia mapema mwaka huu.
Kuhusu video ya albamu hiyo, Mgendi, amesema ataanza zoezi la upigwaji picha za video Januari mwakani kabla ya albamu hiyo kuachiwa sokoni Juni, 2015.
Alisema uchukuaji wa video utahusisha nyimbo zote saba zitakazokuwa katika albamu hiyo inayokuja baada ya kutamba na 'Hongera Yesu'.
Jennifer alisema ataanza kurekodi video ya wimbo wa 'Wema ni Akiba' ambao tayari ameshauachia hewani ili kuitambulisha albamu hiyo ambayo ni ya nane kwake.
"Mchakato wa kurekodi video ya albamu yangu ijayo utaanza mapema Januari na nitaitoa rasmi Juni 2015, ila kwa sasa nimeachia 'audio' ili kuwapa ladha mpya ya Jennifer Mgendi," alisema muimbaji huyo ambaye pi ni muigizaji, mtayarishaji na muongozaji filamu.
jennifer alifafanua kuwa 'audio' albamu ya Wema ni Akiba itaachiwa ndani ya mwezi huu kabla ya Sikukuu ya Xmass.
"Audio albamu ya Wema ni Akiba nitaiachia sokoni kabla uya Krismasi ila video yake ndiyo itatoka Juni baada ya kuanza kurekodi mwezi ujao," alisema Jennifer.
Jennifer ambaye kitaaluma ni mwalimu, alianza kutamba kwenye muziki wa Injili mwaka 1995 akitoa albamu saba sambamba na filamu zilizomjengea jina kubwa miongoni mwa wasanii wa kike nchini.
Sami Khadira atolewa hospitalini, majaliwa yake bado...!
KIUNGO nyota wa klabu ya Real
Madrid, Sami Khedira ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa kwa
siku moja kwa uangalizi kutokana na mtikisiko katika ubongo wakati
wa mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Cornella. Khedira aligongana na kiungo wa Cornella David Garcia muda mfupi baada ya mapumziko katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kabla ya kucheza kwa dakika chache na baadae kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Jese.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, Khedira alifanyiwa vipimo zaidi jana na kuruhusiwa lakini haijajulikana na muda gani atakaa nje ya uwanja.
Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo walitinga hatua ya timu 32 bora bada ya kushinda mchezo wao wa mkondo wa pili kwa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu hivyo kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-1.
Madrid sasa inakabiliwa na mchezo mwingine wa La Liga Jumamosi hii dhidi ya Celta Vigo huku wakiwa na matumaini ya kushinda na kuendelea pengo lao la alama mbili dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
Make Money at : http://bi
Dokii Hakuna Kama Mwanamke videoni
MSANII Ummy Wenceslaus 'Dokii' ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Hakuna Kama Mwanamke' huku akianza mchakato wa kutengenezea video ya wimbo wake mwingine uitwao 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema video yake mpya imetengenezwa na Pablo ambaye pia ndiye aliyepewa jukumu la kuitengeneza video ya wimbo wa 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
"Tayari nimeshaiachia video ya wimbo wangu wa 'Hakuna Kama Mwanamke' ambao 'audio' yake imetengenezwa studuio za Recho Records chini ya mtayarishaji aitwaye Shivo," alisema Dokii.
Alisema wimbo wake wa Nampenda Dereva wa Boda Boda' uliotengenezwa Akhenato Records chini ya Lil Ghetto, utaanza kurekodiwa video yake wiki ijayo kabla ya kuachiwa hewani.
"Video hiyo nayo itatengenezwa na Pablo, hivyo mashabiki wangu wajiandae kushuhudia kazi hiyo mapema kabla ya kumalizika kwa mwezi huu," alisema Dokii.
Muigizaji na mwanamitindo huyo alisema, ameamua kutoa kazi hizo mfululizo kuthibitisha alivyoelekeza nguvu zake katika fani ya muziki akiipa kisogo kwa muda kazi ya uigizaji filamu.
Hatari! Cameroon, Ivory Coast kundi moja AFCON 2015

SHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF, imetangaza droo ya makundi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea kwa kuziweka kundi moja timu za Ghana, Algeria, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa droo iliyofanywa usiku wa jana, timu hizo zimewekwa kundi moja la C ambalo ni la kifo kama lilivyo kundi D lenye timu za Ivory Coast, majirani za Cameroon, Guinea na Mali.
Makundi mengine mawili ya A na B yanaonekana siyo ya kutisha ingawa timu zote 16 zitakazochuana kwenye fainali hizo za mwakani zinapewa nafasi sawa ya kutwaa ubingwa huo ambao hauna mwenyewe baada ya Nigeria kuvuliwa hatua ya makundi.
Katika Kundi A zimepangwa timu wenyeji Equatorial Guinea sambamba na Burkina Faso, Gabon na Congo, huku Kundi B likiwa na timu za zambia, Tunias, Cape Verde na DR Congo.
Fainali hizo zinatarajiwa kuanza kuchezwa Januari 17 na kufikia tamati kwa bingwa kufahamika Februari 8.
Wednesday, December 3, 2014
Liverpool, Man Utd zaua, Arsenal, Chelsea kazi kwao leo
![]() |
| Steven Gerrard akishangilia bao lake usiku wa jana |
![]() |
| Nahodha akionyesha maujuzi yake |
![]() |
| Fellaini akichuana na mchezaji wa Stoke City |

KIUNGO wa kimataifa mkongwe, Steven Gerrard juzi alidhihirisha kuwa 'bado wamo' baada ya kuisaidia Liverpool kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England (EPL).Nahodha huyo ambaye aliwekwa benchi katika mechi iliyopita dhidi ya Stoke City, alianzishwa katika pambano hilo la ugenini lililochezwa kwenye uwanja wa King Power dhidi ya 'vibonde' Leicester City na kufunga bao moja kati ya mabao matatu yaliyozidi kuifufua Liverpool katika ligi hiyo.
Wenyeji ambao walimaliza pambano hilo wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja kutokana na Wes Morgan kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 63, ndiyo wlaikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 22 baada ya kipa Simon Mignolet kujifunga kufuatia shuti la Leonardo Ulloa kugonga mwamba na katika harakati za kuokoa akajikuta akijifunga.
Hata hivyo dakika nne baadaye Adam Lalana aliisawazishia Liverpool bao hilo dakika nne baadaye kutokana na kushirikiana vyema na Ricky Lambert na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe sare ya 1-1.
Gerrard aliiandikia Liverpool bao la pili dakika ya 54 kabla ya Jordan Henderson kuongeza la tatu dakika ya 83 na kumfanya Kocha Branden Rodgers kupumua baada ya Liverpool kuchupa kutoka nafasi ya 11 hadi ya 8 ikiwa na pointi 20.
Katika mapambano mengine ya ligi hiyo yaliyochezwa juzi, Manchester United ikiwa uwanja wa Old Trafford walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, huku West Ham United ilitokana nyuma ugenini na kuichapa West Bromwich Albion mabao 2-1 katika pambano jingine.
Vijana wa Luis Van Gaal walipata mabao yao kupitia kwa Marouane Fellaine aliyemaliza pasi safi ya Ander Herrera katika dakika ya 21 na Juan Mata aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 59, huku bao la wageni lilifungwa na Stephen N'Zonzi katika dakika ya 39.
Nao West Ham walipata ushindi wa mabao 2-1 ugenini baada ya kutanguliwa kufungwa, huku Burnley na Newcastle United zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, Swansea City ikiwa nyumbani ilitakata kwa kuichapa QPR kwa mabao 2-1 na Aston Villa kuiduwaza nyumbani Crystal Palace kwa kuinyuka bao 1-0.
Ligi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena usiku wa leo kwa michezo minne Arsenal itakuwa nyumbani kuwakabili
Southampton, vinara Chelsea wataialika Tottenham Hotspur, huku Everton na Hull City zikionyeshana umwamba na Sunderland kuwakabili Mabingwa watetezi Manchester City.
Vumbi jingine litaendelea Jumamosi kama hivi;
Newcastle United vs Chelsea
Hull City vs West Bromwich Albion
Liverpool vs Sunderland
QPR vs Burnley
Stoke City vs Arsenal
Tottenham Hotspur vs Crystal Palace
Manchester City vs Everton
Arsene Wenger awaonya wachezaji kuhusu Mitandao ya Kijamii
![]() |
| Arsene Wenger |
Kauli hiyo ya Wenger imekuja baada ya mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli kuomba radhi kwa ujumbe aliochapisha ambao ulionekana kama wa kibaguzi.
Akihojiwa Wenger amesema jambo kubwa wanalofanya ni kuwaonya athari zake lakini hakuna anaweza kuwalinda saa 24 kwa siku. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wachezaji wenyewe wanapaswa kuwajibika na kuelimika jinsi ya kudhibiti wanachokiongea.
Tuesday, December 2, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)




