STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 1, 2015

CHELSEA, SPURS KATIKA FAINALI YA KISASI

KLABU za Chelsea na Tottenham Hotspur zinatarajiwa kuvaana leo katika pambano la kisasi la fainali za Kombe la Ligi (Capital One).
Pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa Wembley linarejesha mchezo wa fainali za mwaka 2008 ilizozikutanisha timu hizo kwenye uwanja huo na Spurs kuitambia Chelsea kwa mabao 2-1.
Katika pambano hilo lililochezwa Februari 24, 2008, Spurs ilinyakua taji hilo katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1 Chelsea wakitangulia kabla ya Spurs kurejesha.
Kadhalika pambano hilo la Fainali hizo za Kombe la Ligi limekuja ikiwa ni wiki kadhaa tangu Spurs walipoitoa nishai Chelsea kwa kuichapa mabao 5-3 katika pambano la marudiano ya Ligi Kuu ya England.
Awali Spurs ilicharazwa mabao 3-0 nyumbani kwa Chelsea mwaka uliopita na waliporudiana White Hart Lane waliwashughulikia Chelsea jambo linalofanya mechi ya leo kujaa visasi vitupu.
Chelsea chini ya Jose Mourinho itawakosa baadhi ya nyota wake akiwamo Nimanja Matic aliyefungiwa mechi mbili baada ya kupungiwa adhabu na FA kwa kadi nyekundu aliyoipata wiki iliyopita.
Hata hivyo timu hiyo inapewa nafasi kubwa ya kuwatambia wapinzani wao ambao wanauguza machungu ya kung'olewa kwenye michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) na Fiorentina ya Italia.
Ikiwa na wakali kama Ces Fabrigas, Diego Costa, Eden Hazard, Willian na wengine, Chelsea itapenda kutwaa taji hilo ili kuweka hazina kwa msimu huu baada ya awali kutolewa katika Kombe la FA.
Vinara hao wa Ligi Kuu wanapaswa kuwa makini na kinda linalotisha Harry Kane ambaye amekuwa wakiwaliza makipa hodari kama alivyoonya kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois.
Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizo zimeshakutana mara 134, Chelsea ikishinda mara 57 na wapinzani wao mara 44 na mechi 33 zikiisha kwa sare na pambano la leo litakuwa la 135 kwao katika michuano yote.
Je, ni Chelsea au Spurs atakayecheka leo katika uwanja wa Wembley? Bila shaka ni suala la kusubiri kuona ila kwa hakika ni bonge la mechi.

Arsenal, Manchester City vitani tena EPL

WAKIWA na maumivu ya vipigo walivyopata kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, klabu za Arsenal na Manchester City zitakuwa tena vitani leo kwenye viwanja tofauti katika Ligi Kuu ya England (EPL).
Arsenal walikandikwa mabao 3-1 na Monaco ya Ufaransa itakuwa nyumbani kuumana na Everton, wakati Manchester City watakuwa wageni uwanja wa Anfield kupepetana na Liverpool.
Mabingwa watetezi hao walikumbana na kipigo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Barcelona, na leo watakuwa na kazi ngumu mbele ya Liverpool ambayo imekuwa na matokeo ya kuvutia siku za karibuni.
Katika mechi nne zilizopita za ligi hiyo, Liverpool haijapoteza mchezo wowote, pia ikishinda katika Kombe la Ligi na Ligi Ndogo ya Ulaya.
Zilipokutana mara ya mwisho Agosti 25 mwaka jana katika mechi ya mkondo wa kwanza Liverpool ilinyooshwa na Manchester City kwa mabao 3-1 ugenini hivyo leo kulazimika kulipa kisasi kwa wageni wao.
Kocha wa Man City, Manuel Pellegrini amesisitiza umuhimu wa kupata ushindi katika mchezo huo wa ugenini ili kuweza kupunguza pengo la pointi dhidi ya Chelsea wanaoongoza msimamo wakiwa na pointi 60.
Katika mechi itakayochezwa Emirates, Arsenal itavaana na Everton ambayo katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Agosti 23 mwaka timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutosa sare ya mabao 2-2.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger aliyewashutumu vijana wake kwa kipigo cha Monaco atakuwa na kazi ngumu ya kuwaongoza kikosi chake kupata ushindi nyumbani ili angalau kuwafukuzia Man City.
Wenger anatambua ni michuano miwili tu mpaka sasa ndiyo wana hakika ya kutwaa taji kama watakomaa, Kombe la FA wanaotetea na watakaovaana naManchester United wiki ijayo na michuano ya ligi.
Nafasi ya kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni finyu baada ya kipigo cha Monaco wakilazimika kuhakikisha wapate ushindi wa 3-0 wiki mbili zijazo nchini Ufaransa.
Everton wenyewe wamekuwa na mwenendo wa kuchechemea msimu huu, ingawa siyo timu ya kubezwa kwani inaweza kufanya lolote katika pambano hilo la leo.

Newz Alert! Chenge, Prof Tibaijuka wapigwa 'stop' CCM

WAJUMBE WA NEC NA VIOMNGOZI WAO WAKIWA KWENYE MKUTANO
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/Anna-Tibaijuka.jpg
Prof Anna Tibaijuka

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgS27oyoYZIdbDtS0MoyijSDuiv-YrMjmoWZrojqWZkPwyqY_vw17QyE8ysEJ5E1Zc0kZ07135oIEJ1TkjFSxFGvTdXaxVJvwgpQdHdsMkac0L85zDaG5h_5MlobwaDS5lEnMj0GYtWSdc/s1600/chenge-june18-2013.jpg
Mzee wa Vijisenti, Chenge

KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetangaza kuwasimamisha Wajumbe wake wanaotuhumiwa kwenye sakata la wizi wa fedha za akaunti ya Tegete Escrow kuhudhuria vikao hivyo.
Taarifa rasmi iliyotolewa na CCM inasoma kama ifuatavyo;

KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo;
- Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.

Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.

CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.

Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.

- Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow.

@ Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka
@ Mheshimiwa William Mganga Ngeleja
@ Mheshimiwa Andrew Chenge

Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa kuhusika kwao katika kashfa hiyo.

- Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa Kamati Kuu.

Saturday, February 28, 2015

Mwili wa Kapteni Komba wahifadhiliwa Lugalo Hosp

http://api.ning.com/files/WeTmt906*BKaGszeajuNVr5dNk0HSypjN26QmHzMaFxTohOy6Y0MGC21Im0--55H01NauXCyaXGuZ4IFusMmfHQa9XH9hHlJ/CAPT.JOHNDAMIANOKOMBAMBUNGEMBINGAMANG.CCM.TEL.07442845.jpg
Kapteni Komba enzi za uhai wake
MWILI wa marehemu Kapteni John Komba umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya kijeshi la Lugalo tayari kwa taratibu za mazishi ambayo hata hivyo hayajafahamika yafanyika lini na wapi.
Marehemu Komba alikumbwa na mauti jioni ya leo katika hospitali ya TMJ alipokimbiwa na wanafamilia yake kutokana na kuugua ghafla.\
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na Presha na taarufa nyingine zikieleza ni ugonjwa kisukari.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia taarifa zaidi na itawafahamisha, ila tunaendelea kutoa pole kwa wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na kifo cha Kapteni Komba hususani wanasiasa na wadau wa muziki kwani marehemu alikuwa moja ya wapiganaji katika maendeleo ya sanaa hiyo husuani ubunifu wake wa mtindo wa ACHIMENENGULE aliotaka uwe utambulisho wa muziki wa Tanzania.

VITA YA LIGI KUU BARA BADO MBICHI KABISA!!

Simba angalau sasa inapumua
Polisi Moro
JKT Ruvu waliokuwa mapumzikoni wikiendi hii kabla ya kuvaana na Yanga Jumatano
Mtibwa Sugar wanaozidi kuporomoka
UGUMU wa Ligi Kuu Tanzania unazidi kuongezeka wakati ligi hiyo inaingia raundi ya 16 baada ya matokeo ya michezo ya leo.
Simba ambao wamepanda hadi nafasi ya tatu kwa muda wakisubiri kujua hatma ya pambano la Stand Utd na Kagera Sugar angalau sasa inapumua baada ya ushindi wa mabao 5-0 iliyopta kwa Prisons wakati wanachama na viongozi wao wakielekea kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika kesho Bwalo na Maafisa wa Polisi Oysterbay.
Hata hivyo hali ni mbaya kwa timu za Prisons ya Mbeya na Mgambo JKTambazo nafasi mbili za chini
Prisons Mbeya wana kila dalili za kurudi walipotoka kwa kuzibeba timu zote ikiwa na pointi 12 tu wakati wenzao kwa kipigo ilichopata kwa Coastal wanapointi zao 14 tu.
Ebu tazama msimamo na mbio za kuwania KIatu cha Dhahabu zilivyo mpaka sasa Mnigeria Absolom Chiidebele akiwafukizia waliopo juu yake.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                            P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01.  Yanga            15  09  04  02  21  08  13  31
02.  Azam             15  07  06  02  22  12  10  27
03.  Simba            16  05  08  03  20  12  08  23
04. Coastal Union  16  05  07  04  12  10  02  22
05. Kagera Sugar  15  05  06   04  12  11  01  21
06. Ruvu Shooting16  05  06   05  11  12   -1  21
07. Mtibwa Sugar  14  04  07   03  15  14  01  19
08. Polisi Moro      15  04  07   04  12  13   -1  19
09. JKT Ruvu        15  05  04   06  14  15   -1  19
10. Stand Utd       16  04  06   06  14  18   -4  18
11. Mbeya City      16  04  06  06   11  15   -4  18
12. Ndanda Fc       15  04  04  07   13  18   -5  16
13. Mgambo JKT    14  04  02  08   07  20  -13 14
14. Prisons            16  01  09   06   10  20  -10 12
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
7- Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
 

6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Simon Msuva (Yanga)
 

5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)Emmanuel Okwi (Simba), Absalom Chiibidele (Stand Utd)

4- Rama Salim (Coastal),  Ibrahim Ajibu (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Heri Mohammed,(Stand Utd)


3-
Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Frank Domayo (Azam), Malimi Busungu (Mgambo), Atupele Green (Kagera), Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa (Yanga), Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)
 

2- Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma, Elias Maguli (Simba), Salum Kanoni, (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Jerry Tegete, Coutinho (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi), Peter Mapunda (Mbeya City) Lutimba Yayo (Coastal Union)

Rooney aibeba Man Utd, Saint's wafa ugenini

3pm banner 10.jpg
Muunganiko wa picha kama zilizochapishwa na Daily Mail zikionyesha Man Utd walipoizamisha Sunderland
MABAO mawili kutoka kwa Mshambuliaji wa kimataifa wa England, Wayne Rooney wameiwezesha Manchester United kupata ushindi nyumbani dhidi ya Sunderland na kufufua matumaini yao ya kuwania nafasi ya ushiriki wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
Rooney ambaye kwa muda mrefu amekuwa akichezeshwa kama kiungo na kocha Louis Van Gaal, leo alichezeshwa kama mshambuliaji wa kati na kmufunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuipa Mashetani Wekundu ushindi huoi muhimu.
Nahodha huyo alifunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati dakika ya 66 kabla ya kuongeza la  pili dakika ya 84 na kupoza machungu na hasira walizokuwa nazo mashabiki wa timu hiyo baada ya wiki iliyopita kulala kwa Swansea City.
Katika mechi ya mapema West Ham United ikiwa nyumbani ilicharazwa mabao 3-1 na Crystal Palace, huku Swansea ikiendeleza ubabe katika ligi hiyo kwa kuilaza Burnley nyumbani kwao kwa bao 1-0 huku Newcastle United ikishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Aston Villa.
Nayo timu ya Stoke City iliitambia nyumbani Hull City kwa kuilaza bao 1-0 sawa na ilivyokuwa kwa West Bromwich iliyoitambia Southampton waliowafuta kwao.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili za kuakta na mundu, kwa Liverpool kuikaribisha mabingwa watetezi Manchester City na Arsenal kuialika Everton, wakati Chelsea na Tottenh ham Hotspur wenyewe wataumana kwenye mchezo wa fainali za Kombe la Ligi (Capital One)

MASKINI AZAM! YAANGA AFRIKA KAMA KMKM

Azam waliokumbwa na bahati mbaya Khartoum kwa kung'olewa na El Merreikh
KLABU ya Azam imeungana na wenzao wa KMKM ya Zanzibar kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya usiku huu kunyukwa mabao 3-0 na El Merreikh ya Sudan na hivyo kutolewa kwa jumla a mabao 3-2.
Azam walienda Sudan wakiwa na hazina ya mabao 2-0 iliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza wiki mbili zilizopita, lakini wenyeji walitumia nafasi ya kucheza nyumbani kunadili matokea kama kocha wao alivyoatamba mapema na Azam kuaga mashindano. El Merreikh walikosa pia penati baada ya kupaisha.
Hii ni mara ya pili kwa Azam kuaga michuano katika raundi ya mapema baada ya mwaka jana pia kutolewa na timu ya Ferroviaro de Beira ya Msumbiji.
Azam imetoka ikiwa ni saa chache baada ya KMKM nayo licha ya kuopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Hilal ya Sudan, ilijikuta ikitoka mashindano kwa ujumla ya mabao 2-1 baada ya mechi ya kwanza nchini Sudan kulala mabao 2-0.
Timu ya Polisi Zanzibar waliokandikwa mabao 5-0 na Mounana ya Gabon kesho itajaribu kuweka rekodi mpya Afrika kama itaweza kuifunga wapinzani wao mabaop 6-0 na kuweza kuungana na Yanga walipenya kwa mbinde jana baada ya kulala 2-1 ugenini lakini ushindi wao wa nyumbani ukawabeba na kusonga mbele.
Yanga inayotarajiwa kutua kesho usiku ikitokea Gaborone, itaumana na Platnum ya Zimbabwe kati ya Machi 13-15 katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya Wazimbabwe kuing'oa Sofapaka ya Kenya kwa mabao 4-2 kutokana na kushinda leo 2-1 kama ilivyokuwa katika mechi ya mkondo wa kwanza nchini Kenya.