STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Al Shaabab yawatimua Wakuu wa Usalama Kenya

Aliyekuwa Waziri wa Usalama, Joseph Ole Lenku
RAIS Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi Waziri wa Usalama nchini Kenya, Joseph Ole Lenku na nafasi kumteua Joseph Nkaiseri, huku Mkuu wa Jeshi la Polisi,Inspekta Jenerali David Kimaiyo amejiuzulu wadhifa wake kutokana na shinikizo dhidi yake kutrokana na kudai kushindwa kutimiza wajibu wake kulinda Usalama nchini humo.
Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bw. Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake. Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.
Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini. Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.
Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza muda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment