STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Mgambia wa Simba kujaribiwa wiki mbili kabla ya mkataba

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/mboob.jpg
MSHAMBULIAJI mpya aliyetua Simba, Omary Mboob kutoka nchini Gambia, amepewa wiki mbili kwa ajili ya kufanya majaribio na kikosi hicho na kama akifuzu atasajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
Mboob amewasili nchini juzi kimya kimya na jana aliripoti mazoezi katika Uwanja wa Sigara, Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuanza mazoezi rasmi.
Akizungumza jana, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, alisema wamempa wiki mbili mchezaji huyo kutokana na kwamba hajawahi kumuona katika mechi zake alizowahi kucheza.
"Tumempa wiki mbili za mazoezi ili tumuone kama anafaa au hafai, akifuzu atasajiliwa," alisema Phiri.
Alisema mshambuliaji huyo ni tofauti na Mganda Dan Sserunkuma ambaye atasajiliwa moja kwa moja kutokana na kwamba wameshawahi kumuona akiwa na timu yake katika baadhi ya mechi za kimataifa na nchini yake.
Phiri alisema baada ya wiki mbili watajua kama kiwango cha mchezaji huyo kinaweza kuisaidia timu kuanzia mzunguko wa nane wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 26, mwaka huu.
Kwa upande wa mazoezi kwa ujumla, alisema yanaendelea vizuri kutokana na wachezaji kujifua kwa bidii kuelekea mechi ya 'Nani Mtani Jembe 2' dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga Desemba 13, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment