STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Yanga yampa mkataba wa mwaka mmoja Mbrazil Emerson

EMERSON AKISAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUICHEZEA YANGA MBELE YA MTAALAMU WA MAMBO YA IT NA MSEMAJI WA YANGA, BARAKA KIZUGUTO.
KLABU ya soka ya Yanga imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja kiungo mkabaji mpya kutokla Brazil,  Emerson De Oliveira Neves Roque.
Tukio la usainiwaji wa mkataba huo wa mwaka mmoja lilifanyika jana baada ya kiungo huyo kuliridhisha benchi la ufundi la klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na mtandaop wa klabu ya Yanga benchi la ufundi liliridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.

Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

No comments:

Post a Comment