STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Irene Uwoya, JB, Richie kupamba uzinduzi Family Singers J'mosi

WASANII nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya, Jacob Stephen 'JB' na Single Mtambalike 'Richie' wanatarajiwa kupamba uzinduzi wa albamu ya pili ya Kikundi cha Waimbaji wa Injili cha 'Family Singers' utakaofanyika siku ya Jumamosi.
Uzinduzi huo wa albamu hiyo iitwayo 'Usilie' utafanyika kwenye ukumbi wa PTA-Sabasaba, Temeke Dar es Salaam na utapambwa na shushuli za upimaji bure wa afya kwa wananchi mbalimbali sambamba na burudani ya muziki toka kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili na wasanii hao wa Bongo Movie.
Mkurugenzi wa kikundi hicho kilichopo chini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA), Daniel Misheto Jr, aliiambia MICHARAZO kuwa wasanii wa Bongo Movies wamethibitisha kuwapiga tafu katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Misheto alisema kuwa maandalizi kuelekea uzinduzi huo yanaendelea vema na idadi wa watakaosindikiza ikizidi kuongezeka na kudai mbali na wasanii wa Bongo Movies, pia wazee wa Buguruni nao wamethibitisha kuwepo katika uzinduzi huo ambao utaenda sambamba na zoezi la kuwapima afya na kuwatibia watu bure kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana kabla ya huduma ya uimbaji kushika kasi.
Baadhi ya waimbaji Injili watakaosindikiza onyesho hilo ni Leah Moody, mshindi wa BSS, Vocapella, Martha Mwaipaja, AIC (T) Vijana Chang'ombe, Accasia Singers, Papson Mistaki wa Kenya na Frank Hume kutoka Marekani.

No comments:

Post a Comment